Tafuta

Vatican News
Mara baada ya Misa katika kikianisa cha Mtakatifu Marta Vatican tarehe 28 Machi Papa Francisko amehitimisha kwa kuabudu na kubariki na Ekaristi Mara baada ya Misa katika kikianisa cha Mtakatifu Marta Vatican tarehe 28 Machi Papa Francisko amehitimisha kwa kuabudu na kubariki na Ekaristi 

Papa Francisko amekumbuka watu ambao wameanza kuwa na njaa!

Katika misa ya asubuhi kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta,mjini Vatican Papa Francisiko amepyaisha tena sala yake kwa ajili ya familia ambao wameanza kuteseka kutokana na matokeo ya janga la Covidi-19.Katika mahubiri Papa Francisko amekumbuka mapadre na watawa ambao hawasahau mahali walipotoka na kuendelea kusadia maskini,wagonjwa katika kipindi hiki.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 28 Machi 2020 ilikuwa ni misa ya ishirini inayotangazwa moja kwa moja na katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican mara baada ya kusitisha nchini Italia na nchi nyingine maadhimisho ya Ekaristi kwa ushiriki wa waamini kwa sababu ya janga la virusi vya corona. Papa Francisko kwa kuanza amesema: Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, kilio changu kikaingia masikioni mwake... (Zab 18,5-7). Katika nia za maombi ya  Papa Francisko amewafikiria  familia na wale wote ambao wamaeanza kupata madhara ya matokeo uchumi katika kipeo hiki cha kiafya.

Papa Francsiko ametazama tayari janga kwa sababu baadhi ya matokeo yanajionesha  sasa na hasa kwa upande wa njaa. Papa amesema, inaanza kujionesha hali ya watu ambao wana njaa kwa sababu hawawezi kufanya kazi, hawana kazi maalum na mambo mengine mengi. Hali halisi inaanza kuonekana tayari na ambayo itakuwa hali ya baadaye, lakini inaanza sasa. Kufuatia na hiyo, Papa Francisko misa yake ameitolewa kwa familia zote ambazo zimeanza kuhisi mahitaji kutokana na janga hili. Katika Injili ya siku kutokana (Yh 7, 40-53), inaelezea wafarisayo ambao wanahukumu Yesu na Nicodemu anayejaribu kutafuta njia. Papa Francisko amesoma tena kifungu cha Injili kuhusiana na mivutano kati ya wakuu na watu, kati ya wale ambao wamepoteza kumbukumbu ya kuwa nao wanatokana na watu hao, na watu wanaomwamini Mungu na ambao hawawezi kushindwa. Ni mivutono ya kila kipindi ambayo inaonekana hata sasa katika kipindi cha virusi vya corona, ameisitiza Papa Francisko.

Papa amasema: “nimesika siku hizi wanasema ni kwa nini watawa, mapade ambao ni wazima na wanakwenda kwa maskini kuwapa chakula na ambapo wanaweza kupata virusi vya corona? Wawambie maaskofu wasitoke mapadre, wao ni kwa ajili ya sakramenti tu, bali serikali ijali watu wake. Ni watu wa daraja la pili. Sisi ni kundi la daraja la  watawala, hatupaswi kuchafua mikono yetu kwa ajili ya maskini. Mara nyingi ninafikiri kuna watu wema, makuhani na  watawa, lakini ambao hawana ujasiri wa kwenda kuwatumikia maskini. Kuna  kitu kinakosekana” Amesema na kuongeza kukazia kwamba  daraja la kikuhani wasigeuke kamwe kuwa wasomi ambao wanajìfunga bila kutoa  huduma ya kidini ambayo iko mbali na watu, kamwe wasisahau  walikotoka yaana kwa watu na kuhudumia.

Aidha Papa Francisko amejikita kutafakari mivutano iliyokuwa kati ya wale wanamfuata Yesu na kikundi cha walimu wa sheria ambao awali ya yote wanamkana Yesu kwa mijibu wao kuwa  hatendi kulingana na sheria. “Papa amesema, kikundi hiki cha walimu wa sheria, wasomi wanaridhia kumdharau Yesu, lakini pia wanahisi dharau hata kwa watu na kusema  ni wajinga kwa maana hawajuhi kitu. Kinyume chake ni watu watakatifu na waaminifu wa Mungu na wanamuamini Yesu, wanamfuata na wakati huo huo  katika kikundi hiki kidogo cha wasomi, walimu wa sheria wako mbali na Yesu na hawamkubali Yesu. Hata hivyo kwa kufafanua zaidi Papa amesema  wasomi  wana dosari kubwa, ambayo wao wamepoteza kumbukumbu ya walikotoka yaani kwa watu. Mvutano huu kati ya wasomi na viongozi wa dini na watu ni mchezo wa kuigiza ambao unatoka mbali. Watu wa Mungu wanayo neema kubwa, ya kujua ni wapi kuna  Roho. Lakini ni akili ya kujua njia za wokovu. Shida ya wasomi, ya makuhani imekuwa kubwa, imeongezeka   kupitia katika daraja la kijamii na wanahisi wao kuwa viongozi.

Papa Francisko amewaalika waamini kufikiria watu, wanaume wengi na wanawake wenye taaluma katika  kuhudumia Mungu na ambao kweli wanahudumia maskini, makuhani wengi ambao hawajibagui na watu wao. Aidha amesimulia juu ya kuona picha ya Paroko mmoja anayeishi katika mlima, sehemu ambayo wakati mwingine kuna theruji na katika theruji anapeleka Mostrance katika vijiji ili kuwabariki. Hakujali theruji wala kuumizwa na baridi inayoumiza mikono yake ambayo imeshikilia Mostarance.

Kwa kuhitimisha Papa Francisko ameomba kujifikiria sisi binafsi ni sehemu gani tuliyopo, ikiwa tuko katikati ya kukosa maamuzi au kinyume chake tukiwa ni watu waamini wa Mungu ambao hawawezi kushindwa, au wasomi ambao wanajibagua na watu wa Mungu. Labda itakuwa vizuri kwa wote kupata ushauri wa Paulo anaowapatia wafuasi wake hasa kijana Askofu Timoteo juu ya kukumbuka mama na bibi yake. Ikiwa Paulo alikuwa anashuri hivyo ni kwa sababu alikuwa anatambua vizuri hatari iliyokuwa inapelekea ya kujiona wasomi katika utawala wetu.

28 March 2020, 10:40
Soma yote >