Tafuta

Misa ya Papa Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican tarehe 9 Machi 2020 Misa ya Papa Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican tarehe 9 Machi 2020  (@Vatican Media)

Misa ya Papa ya moja kwa moja imetolewa kwa wagonjwa wa virusi vya corona!

Papa Francisko wakati wa kuadhimisha Misa Takatifu katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican tarehe 9 Machi 2020,ameomba iweze kutangazwa moja kwa moja,kama itakavyokuwa hata kwa siku zijazo ikiwa ni kutaka kuonesha ukaribu wake wa kila siku kwa wale waliokumbwa na maambukizi ya mafua ya virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameadhimisha Misa Takatifu  tarehe 9 Machi 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican kwa uamuzi wa kuitangaza moja kwa moja na kama itakavyokuwa hata siku sijazo akitaka kuonesha ukaribu wake kwa wote ambao wamekumbwa na mlipuko wa Virusi vya Corona.  Katika kuungana na Papa kwenye kipindi kigumu na zaidi kuungana na Kristo na  kuungana kati yetu. Tayari Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana  Jumapili 8 Machi 2020 alikuwa amewakumbuka kwa namna ya pekee wenye maambukizi ya Corona na wahudumu wao. Akianza mahbiri yake Papa Francisko amesema: “Katika siku hizi nitatolea misa yangu kwa ajili ya wagonjwa wa mlipuko wa virusi vya  corona,  kwa ajili ya madkatari na wakunga, watu wa kujitolea ambao wanawasaidia sana, familia zao, kwa ajili ya wazee ambao wako katika vituo vya huduma , kwa ajili ya wafungwa ambao wako jela. Tusali pamoja kwa wiki hii sala ya nguvu kwa Bwana: “niokoe ee Bwana na kunirehemu. Mguu wangu umesisima mahali panyofu, katika makutano yako nitakusifu ee Bwana."

Papa Francisko katika tafakari yake akiangaziwa na somo la kwanza kutoka  Kitabu cha Nabii Danieli anakumbuka ulazima wa kujitambua dhambi. “Katika somo hili Danieli ni muungamishi wa dhambi. Watu wanatambua kuwa wamekosa … “Bwana umekuwa mwaminifu kwetu sisi, lakini sisi tumekutendea dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako. wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.” Papa Francisko katika sala hiyo anafafanua kwamba: Kuna kuungama dhambi, utambuzi wa kujua dhambi tulizo nazo. Tunapotaka kujiandaa kupokea sakramenti ya kitubio, lazima kufanya tafakari ya dhamiri zetu na kuona nini ambacho tumefanya mbele ya macho ya Mungu  yaani kuona dhambi ya kweli kutambau dhambi binafsi Lakini utambuzi wa dhambi hauwezi kufanyika kwa njia ya  kiakili tu na kuorodhasha dhambi kwa kusema utamwambia Baba kuwa umekosa na yeye akakuhurumia.

Siyo lazima kumfanya hivyo na siyo haki. Hii ingekuwa ni kama  ni kufanya orodha ya mambo ambayo unatakiwa kuyatenda au unapaswa kuwa nayo au umefanya vibaya  na kubaki nayo kichwani. Ungamo la kweli la dhambi limapaswa libaki ndani ya moyo kwa kina. Kwenda kwa muungamishi ni  kwenda kumwambia Padre juu ya orodha ya dhambi tulizo nazo  na baadaye unaondoka ukifikiri umesamehewa. Kumbe siyo hivyo maana  tendo hili linahitaji kufanyika  kwa hatua moja baada ya nyingine ambayo inakupelekea  kuungamana makosa kutoka ndani ya moyo, yaani kila aina  ya ubaya na ukatili ambao umeufanya unaotoka ndani ya moyo. Ni kwa njia hiyo Nabii Danieli alifanya na kusema “ Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo”.

Papa Francisko amebainisha kwamba: “Ikiwa ninautambuzi wa dhambi ambayo sikuweza kusali vizuri  ninahisi ndani ya moyo kunisuta na kuhisi haya mbele ya uso wa Bwana. Hata hivyo   “haya ya dhambi zetu ni neema ambayo tunatakiwa kuiomba na  kusema: “ Ee Bwana nifanye niwe na aibu. Mtu ambaye amepoteza haya anapoteza hata mamlaka ya kimaadili, anakosa hata heshima kutoka kwa wengine.  Mwenye aibu, anaoneshwa na Nabii Daniel leo hii akisema  “Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake."

Ikiwa sisi tutakuwa si tu na kumbu kumbu ya dhambi zetu ambazo tumefanya, lakini hata hisia za aibu, tabia ambayo inagusa moyo wa Mungu, na  Yeye atajibu kwa huruma. Safari ya kwenda kukutana na huruma ya Mungu ni kujionea aibu ya mambo mabaya, ya ukatili ambao tumeufanya. Kwa njia hiyo mimi kweli ninaweza kwenda kuungana na kusema kile ambacho nimetenda na siyo orodha ya dhambi; ni hisia ya kweli ya kuona  aibu ya kumtenda mabaya Mungu ambaye ni mwema sana kwetu, mwenye huruma na mwenye haki nyingi.Amehitimisha Papa Francisko.

09 March 2020, 10:32
Soma yote >