Tafuta

Vatican News
Bwana hawezi kuingia katika mioyo migumu; katika mioyo ya kiitikadi hawezi kuingia Bwana. Bwana huingia tu katika mioyo ambayo ni kama moyo wake yaani moyo yenye huruma,moyo wenye upendo na  moyo uliyo wazi. Bwana hawezi kuingia katika mioyo migumu; katika mioyo ya kiitikadi hawezi kuingia Bwana. Bwana huingia tu katika mioyo ambayo ni kama moyo wake yaani moyo yenye huruma,moyo wenye upendo na moyo uliyo wazi.  (Vatican Media)

PapaFrancisko:Dawa dhidi ya ugumu wa moyo ni kumbu kumbu!

Papa Francisko wakati wa tafakari yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 18 Februari 2020 amesema dawa ya kutibu ugumu wa moyo ni kuwa na kumbu kumbu. Moyo unapogeuka kuwa mgumu,unasahu;unasahamu neema ya wokovu,unasahau zawadi ya bure.Moyo mgumu unapelekea ugomvi,vita,ubinafsi, unapelekea kumwaribu ndugu,kwa sababu moyo huo hauna uhuruma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mikate ya kutosha inakosa kwa wafuasi ambao walipanda mtumbwi na Yesu na wao wanaaanza kuwa na wasiwasi wa zana za uendesha wa siku. Wao kwa mujibu wa Injili ya Marko 8,14-21, walikuwa wakijadiliana kati yao, kwa sababu hawakuwa na mikate. Kufuatia na hiyo, Yesu akawa ametambua hayo na kuwakaripia kwanini wanabishana kwamba hawana mikate, Je  hamjatambua bado na hamuelewi? Mnakuwa na mioyo migumu? Mnayo macho, hamuoni na masikio hamsikii? hamkumbuki nilipogawa mikate mitano  kwa watu elfu tano, vikapu vingapi vilibaki vimejaa na kupelekwa?

Pasipo na huruma kuna mawazo ya miungu na itikadi

Kwa kufafanua Injili hiyo Papa Francisko ametaka kuelewesha kwamba kuna jambo moja linaolongiliana  kati ya moyo kuwa mgumu kama ule wa wafuasi wa Yesu na moyo wa huruma kama wa Bwana, ambao unajielezea Mapenzi yake.  Mapenzi ya Bwana ni huruma. Yeye anasema ninataka huruma na siyo dhabihu. Moyo bila huruma ni moyo wa kimiungu, ni moyo unajitosheleza na kuongozwa na ubinafsi, ambao unakuwa na nguvu tu kutokana na itikadi za mawazo yake. Akitolea mfano amesema “tukumbuke makundi manne ya mawazo ya kiitikadi ya wakati ule wa Yesu”.  “Walikuwapo wafalisayo, wasadukayo, waeseni na wazeloti”. Ni makundi manne yaliyokuwa na moyo mgumu katika kupelekea mbele mpango ambao haukuwa wa Mungu; hapakuwapo na nafasi ya mpango wa Mungu, hapakuwa na nafasi ya huruma, Papa amesisitiza.

Yesu ni kofi la dhidi ya moyo ulio mgumu

Lakini kuna hata dawa ya kudhibiti ugumu wa moyo ambayo ni kumbu kumbu. Kwa maana hiyo katika Injili ya leo na katika sehemu nyingi za Biblia Papa Francisko amerudia kutoa ushuri kama kiitikio kwamba  hata mwisho wa wokovu mkuu katika kumbu kumbu na  ambayo ni neema ya kuomba ili kuweza kutunza moyo ubaki wazi na mwaminifu. Moyo unapogeuka kuwa mgumu, yaani moyo ukiwa mgumu unasahau… unasahamu neema ya wokovu, unasahau zawadi ya bure. Moyo mgumu unapelekea ugomvi, unapelekea vita, unapekelea ubinafsi, unapelekea kumwaribu ndugu, kwa sababu moyo huo hauna uhuruma. Ujumbe wa wokovu ulio mkubwa ni kwamba Mungu alipata huruma kwa ajili yetu sisi. Ni kiitikio cha Injili wakati Yesu anapoona mtu, hatika hali ya uchungu, yeye anaona uhuruma. Yesu ni huruma ya Baba; Yesu ni kofi dhidi ya kila moyo ulio mgumu.”

Kuwa na moyo ulio wazi maana mungu hawezi kuingia katika moyo mgumu

Papa anasema ni lazima kuomba neema ya kuwa na moyo usio na mawazo potofu na, ulio wazi na wenye huruma mbele ya kile kinachoonekana katika dunia hii, kwa maana tutahukumiwa siku moja, na  katika hukumu si kutokana na mawazo yetu au itikadi zetu. Hata yatajionesha katika : “Nilikuwa na njaa, hamkunipatia chakula; nilikuwa mfungwa, hamkunitlembea, nilikuwa na mateso hamkunifariji, kwa mujibu wa Injili  ndiyo huruma inayotakiwa  na siyo ugumu wa Moyo Papa amesisitiza. Unyenyekevu, kumbu kumbu za mizizi yetu na wokovu wetu vitatusaidia kuhifadhi hayo”. Sala ya Papa Francisko kwa kuhitimisha amesema: “Kila mmoja wetu ana kitu ambacho kinamuuma na kumsababisha awe mgumu wa moyo. Tufanye kumbu kumbu na Bwana ndiye atupatie moyo wenye haki na wa dhati, kama tulivyoomba  katika maombi ya pamoja, mahali anakoishi Bwana. Bwana hawezi kuingia katika mioyo migumu; katika mioyo ya kiitikadi hawezi kuingia Bwana. Bwana huingia tu katika mioyo ambayo ni kama moyo wake yaani moyo yenye huruma, moyo wenye upendo na  moyo uliyo wazi. Bwana atupe neema hii”.

ZAWADI YA HURUMA NA UPENDO
18 February 2020, 16:16
Soma yote >