Tafuta

Kiukweli katika Heri zinasisitiza kuwa safari ya unyenyekevu ndiyp ya kumwinga Bwana mwokozi wa ulimwengu. Kiukweli katika Heri zinasisitiza kuwa safari ya unyenyekevu ndiyp ya kumwinga Bwana mwokozi wa ulimwengu.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Unyenyekevu ndiyo njia ya kumfuasa Yesu!

Papa Francisko akitafakari kuhusu Injili ya leo,anawashauri wakristo wafuate njia iliyoelekezwa na Yesu na Yohane yaani ya unyenyekevu.Hata kwa wachungaji anawashauri wasiteleza katika vishawishi vya kidunia.

Na Sr.Angela Rwezaula  - Vatican

Usiwe na hofu ya kujinyenyekeza hivyo  tuombe Mungu aweze kututumia mtua wa kutunyenyekesha ili tumwige vema Yesu. Ndiyo maombi na ushauri wa Papa Francisko wakati wa kuhitimisha mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 7 Februari 2020. Akianza na tafakari yake kuhusiana na Injili ya Siku, Papa ameeleza jinsi Yohane Mbatizaji alivyokuwa ametumwa na Mungu kuonyesha  barabara, yaani njia ya Yesu. Nabii wa mwisho alipata nafasi ya kuonyesha:“ tazama huyp  ndiye Masiha,” amekumbusha Papa. Kazi ya Yohane Mbatizaji haikuwa kutangaza kuwa Yesu anakuja na kuandaa watu tu  bali alikuwa anatoa ushuhuda wa Yesu Kristo na kutoa maisha yake mwenyewe. Kutoa ushuhuda wa njia iliyochaguliwa na Mungu kwa ajili ya wokovu ni njia ya unyenyekevu. Paulo anaeleza wazi katika barua yake kwa Wafilipi kwamba, “Yesu alijinyenyekeza mwenyewe akatii hadi mauti ya Msalaba”. Hii ndiyo kifo cha msalaba, ndiyo njia ya unyenyekevu hata ni njia yetu ambayo Mungu anaonesha kwa wakristo ili kwenda mbele.

Safari ya unyenyekevu ndiyo hiyo

Mtakatifu Yohane na Yesu walikumbana na kishwishi cha ubatiri na kiburi. Yesu katika jangwa na ibilisi, mara baada ya kufunga, na  Yohane mbele ya waandishi wa sheria waliokuwa wanauliza kama yeye ni masiha, Papa amefafanua.  Hata hivyo angeweza kuwajibu kuwa ni mhudumu wake, lakini akajinyenyekeza. Na wote wawili walikuwa na uwezo mkubwa mbele ya watu, kwa maana mahubiri yao yalikuwa na mamlaka. Wote wawili walikumbana na kipindi kigumu cha shinikizo la kibinadamu na kiroho kwa maana Papa anaonesha mfano halisi wa Yesu katika bustani ya Getsemani na  Yohane akiwa gerezani  na mashaka makubwa kama kweli Yesu ni Masiha.

Yohane na Yesu waliishia mtindo mmoja: kifo msalabani na kukatwa kichwa gerezani

Wote wawili waliishia katika mtindo mmoja wa unyenyekevu zaidi. Yesu alikufa kifo msalabani, kifo kama mnyang’anyi mkuu, cha kutisha kimwili hata kiroho, akiwa utupu mbele ya watu na mama yake. Wakati huo huo, Yohane Mbatizaji alikatwa kichwa gerezani na askari kwa amri ya mfalme mdhaifu na tabia mbaya, iliyotokana na uharibifu na uwezo wa kucheza na chuki ya mzinifu, akimaanisha Herodia na binti yake. Yohane anasisitiza ni Nabii mkubwa, mtu mkubwa aliyezaliwa na mwanamke kama alivyo msifu Yesu, na Mwana wa Mungu aliye chagua njia ya unyenyekevu. Hii ni njia ambayo inatuonesha kwamba sisi wakristo tunapaswa kuifuata Papa anasisitza. Kiukweli katika Heri zinasisitiza kuwa safari ya unyenyekevu ndiyo hiyo.

Njia ya kidunia, hakuna unyenyekevu bila kuabishwa

Huwezi kuwa mnyenyekevu bila kunyenyekeshwa, na kwa maana hiyo mwaliko wake kwa wakristo ni kwamba ili waweze kuongozwa na ujumbe wa Neno la Mungu la Siku kwa ajili ya utambuzi zaidi. “Tunapotaka kufanya Kanisa lionekane, katika Jumuiya , ili kuwa na nguvu moja au nyingine hiyo ni njia ya kidunia, ni barabara  ya malimwengu, na siyo njia ya Yesu”. Na hata wachungaji wanaweza kupatwa na kishawishi cha kupanda hasa katika kufikiria kuwa: “hii ni dhuluma, hii ni fedheha, siwezi kuvumilia”. Lakini “ikiwa mchungaji hafuati njia hiyo, Yeye ni mtu mwenye kupanda altareni na mavazi ya kikuhani, tu lakinisiyo mwanafunzi wa Yesu”. Kwa maana hakuna hakuna unyenyekevu bila kuabishwa.

07 February 2020, 13:03
Soma yote >