Tafuta

Katika kipindi ambacho tunakwenda mbali na Mungu tuhisi kwa hakika sauti isemayo: “Mwanangu kwa nini? Katika kipindi ambacho tunakwenda mbali na Mungu tuhisi kwa hakika sauti isemayo: “Mwanangu kwa nini?  (ANSA)

Papa Francisko:Mungu analia kwa ajili yetu tunapokwenda mbali naye!

Kilio cha Daudi kwa ajili ya Mtoto wake katili aliyekuwa amemguka ni unabii wa upendo wa Mungu Baba.Upendo ambao ni msukumo hadi kifo cha msalaba wa Yesu.Amethibitisha hayo Papa Francisko wakati wa mahubiri yake kwenye Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican na kwamba Bwana ni baba na kamwe hakani ubaba wake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako,Absalomu, mwanangu, mwanangu! Ni kilio cha uchungu wa Daudi kwa machozi baada ya kupata habari za kifo cha mwanae. Katika somo la kwanza la kitabu cha Pili cha Samueli kinaeleza juu ya mwisho wa vita vilivyodumu muda mrefu kati ya  Absalomu dhidi ya baba yake, mfalme Daudi  ambaye alikuwa ampatia kiti cha ufalme. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Papa Francisko akielezea juu ya historia ya Daudi aliyeteseka kutokana na vita vilivyonzishwa na mwanae dhidi yake na kuwashawishi watu wapmabe dhidi yake  na kumsababisha Daudi akimbilie Yerusalemu ili aokoe maisha yake. Bila viatu na kujifunika kichwa watu wengi walianza kumdhiahaki hata kumtupia mawe kwa sababu watu hao walikuwa wamemuunga mkono mwanae aliyekuwa amewadaa kwa ahadi zake.

Kilio cha Daudi kinaonyesha moyo wa Mungu

Somo hili  linalisimulia  Daudi akiwa anasubiri kusikiliza habari zaidi kutoka vitani, na mwisho mjumbe anamwambia Absalomu amekufa katika mapigano. Mara baada ya kupata taarifa hizo, Daudi kwa simanzi anaanza kulia aksema:  “ Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu! Kwa hakika aliyekuwa karibu na  Daudi hapo alianza kushangaa Papa anasema.  Kwa nini analia? Yeye alikuwa ni adui na alikuwa amekana ubaba wake, amemkutakana, amemtesa, badala ya kufanya sikukuu kwa ajili ya ushindi, kumbe ni kilio? Lakini Daudi alisema tu Mwanangu, Mwanangu na kulia sana. Papa Francisko amebainisha. Kilio cha Daudi ni tuki la kihisotria laini ni unabii

Kilio cha Daudi ni tukio la kihisotria lakini pia ni unabii. Ni kutufanya tuone moyo wa Mungu, anavyofanya kwetu sisi  na hasa  tunapokwenda mbali na Yeye. Ndicho anafanya Bwana tunapojiharibu sisi wenyewe, kwa dhambi zetu, kukosa mwelekeo na kupotea. Bwana ni baba, na kamwe hakini ubaba wake maana anarudia kusema: “ Mwangu, Mwanangu”. Papa anabainisha kwamba kilio hicho cha Mungu  tunakutana nacho tunapokwenda kuungama dhambi zetu, kwa maana si kama kwenda katika chumba cha kufua ngu na kutoa madoa, bali ni kwenda kwa Baba anayelia kwa ajili yangu kwa kuwa ni Baba. Papa Francisko amesisitiza.

Kamwe Mungu hakani ubaba wake

Sentesi aliyosema Daud kuwa “Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu” ni unabii na Mungu anajifanya hali halisi. Yeye ana upendo mkubwa kwa kuwa ni baba na Mungu aliyo nao kwetu hadi kufa kwa ajili ya nafasi yetu. Yeye alijifanya mtu na akafa kwa ajili yetu. Ikiwa tutazama msalaba, tufikirie hili kwamba “ Laiti ningekufa mimi badala yako”. Tatahisi sauti ya Baba ambaye anasema:“ Mwanangu, Mwanangu”. Mungu kamwe hakani wanae, Mungu hafanyi mchakato wa ubaba wake bali yeye ni Baba tu.

Kwa njia ya Yesu Mungu  alikufa kwa ajili ya nafasi yetu

Upendo wa Mungu ulifikia kikomo cha hali ya juu anasema Papa. Kile ambacho ni msalaba, ni Mungu, Mwana wa Baba aliyetumwa ili kutoa maisha kwa ajili yetu. Papa Francisko ametoa ushauriwa kutafakari hasa wakati wa kipindi kigumu na kibaya cha maisha yetu ambacho mara nyingi tunakumbana nacho. Kipindi cha dhambi na wakati wa kwenda mbali na Mungu, inawezekana kuhisi katika moyo sauti isemayo:“ Mwangu, huko unafanya nini? “Usijiue tafadhali”. Mimi nimekufa kwa ajili yako. Yesu alilia akitazama mji wa Yerusalemu. Yesu alilia ili sisi tuweze kujiachia kupendwa na Yeye. Katika kuhitimisha Papa ametoa mwaliko kwamba: Katika kipindi cha majaribu, katika kipindi cha dhambi, katika kipindi ambacho tunakwenda mbali na Mungu tuhisi kwa hakika sauti isemayo: “ Mwanangu kwa nini?

 

04 February 2020, 17:19
Soma yote >