Tafuta

Papa Francisko tarehe 7 Januari 2020 ameanza tena maadhimisho ya Ibada Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican Papa Francisko tarehe 7 Januari 2020 ameanza tena maadhimisho ya Ibada Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican  

Roho Mtakatifu anakufanya ukae kwa Bwana.Ni dhama na nguvu ya kukaa naye!

Tarehe 7 Januari 2020 Papa ameanza kwa mara nyingine tena Ibada ya Misa za kila asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican ambapo kwa njia ya somo la Mtakatifu Yohane Mtume amekumbusha kuwa Roho Mtakatifu ni uhakika kwamba Mungu anakaa nasi na tusiwe na imani katika roho ya ulimwengu ambayo hutufanya kukosa fahamu hadi kufikia hatua ya kutojua kutofautisha mema na mabaya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameanza kwa upya Misa za kila asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, Jumanne tarehe 7 Junuari 2020 ambapo katika mahubiri yake akidadavua somo la kwanza la Liturujia ya siku la Mtakatifu Yohane Mtume, Mwinjili akionesha Yesu wakati anawapatia ushauri wake kwamba wabaki katika Mungu. Maisha ya Mkristo ni kubaki katika Mungu kwa kufuata Roho Mtakatifu na siyo roho ya ulimwengu ambayo inapelekea njia za ufisadi  na hutufanya kukosa fahamu hadi kufikia hatua ya kutoweza kutofautisha mema na mabaya.

Wakristo wengi leo hii wanafikiri Roho Mtakatifu ni njiwa

Papa Francisko amesmea mmoja anaweza kuwa katika miji ya dhambi zaidi, katika jamii isiyo mjua mungu zaidi, lakini iwapo moyo unabaki katika Mungu, iwe kwa mwanamke huyo au mwanamme anapata wokovu. Na zaidi amekumbuka tukio linalosimuliwa katika Kitabu cha Matendo ya Mitumekuhusu walipofika katika mji na kukutana na wakristo waliobatizwa na Yohane. Wao waliuliza kama, “ walipokea Roho Mtakatifu”,  lakini hawa walikuwa hawajuhi roho ni kitu gani wanaambiwa. Kwa maana hiyo  Papa Francisko ametoa takari ya kujiuliza: “Ni Wakristo wangapi, hata leo, wanamtambua Roho Mtakatifu kwa kufikiria ni njiwa tu, na hawajui kuwa ndiyo anakufanya ukae kwa Bwana,; ambaye ni dhamana na ni nguvu ya kukaa ndani mwa Bwana".

Roho ya ulimwengu inakuondolea fahamu

Akiendelea na mahubiri, Papa Ffancisko amezungumzia  juu ya roho ya ulimwengu ambayo ni kinyume na Roho Mtakatifu na kusema: “Katika Karamu kuu ya mwisho, Yesu hakuomba Baba yake awaondoe mitume ulimwenguni, kwa sababu maisha ya kikristo yako duniani, bali Yeye aliwaombea walindwe dhidi ya roho ya ulimwengu ambayo ni kinyume” . Kwa kusisitiza  zaidi ameongeza " roho hii ni mbaya zaidi kuliko kutenda dhambi. Ni hali  ambayo inakufanya upoteze fahamu, inakupeleka kwenye hatua ambayo huwezi kutambua wema na mabaya.

Roho Mtakatifu ni dhamana ya kukaa na Mungu

Ili kubaki ndani ya Mungu ni lazima  kuomba zawadi hiyo ya Roho Mtakatifu, ambayo ndiyo dhamana. Kwa maana hiyo Papa anasema : “tunajua kubaki katika Bwana.  Lakini tunawezaje kujua ikiwa tunayo Roho Mtakatifu au roho ya ulimwengu? Lakini Mtakatifu Paulo anaelezea na kutupatia ushauri: "Msihuzunishe Roho Mtakatifu. Tunapokwenda katika roho ya ulimwengu tuna huzunisha Roho Mtakatifu na kuupuuzia, tunaiacha roho kandoni na maisha yetu tunayapeleka katika njia nyingine.

Wakristo na sherehe za Mwaka mpya  huku wakifuja fedha

Roho wa ulimwengu ni kusahau kwa sababu dhambi inakufanya uende mbali na Mungu na ikiwa hakuna kugutuka na  kuomba msamaha. Vile vile roho ya ulimwengu unakufanya usahau nini maana ya dhambi na kuona kuwa unaweza kufanya kila kitu. Katika mantiki hiyo Papa ametoa mfano wa kuonesha Clip moja ya video na Padre mmoja iliyokuwa inaonesha juu ya Wakristo wanaadhimisha sikukuu ya mwaka mpya kwenye mji wa kitalii katika nchi ya kikristo. Hawa amesema walikuwa wanasheherekae mwaka mpya kwa kwa malimwengu ya kiajabu huku wakifuja fedha kwa mambo mengi. Yaani roho ya ulimwengu.

Je hiyo ni dhambi? ni ufisadi

Huo ulikuwa ni ufisadi  zaidi ya dhambi, amebainisha Papa kwani  Roho Mtakatifu anakupeleka kwa Mungu na unapotenda dhambi, Roho Mtakatifu anakulinda na kukusaidia ili uamke kwa upya, lakini Roho wa ulimwengu anakusukuma katika ufisadi hadi kufikia hatua ya kishindwa kutambau yaliyo mema na mabaya, Yote hayo ni sawa sawa na yanafanana.

Kutazama kama majaribu yanatoka kwa Mungu au ulimwengu

Papa Francisko aidha amekumbuka wimbo mmoja nchini Argentina usemao:“Nenda,nenda,nenda … yote yanafanana ambapo huko  juu motoni tutakutana”.Na katika kufafanua amesema ndiyo hiyo roho ya ulimwengu inayo kundolea fahamu na kushindwa kutofautisha ubaya. Je ni kwa namna gani ninaaweza kutambua kama niko njia ya ulimwengu au ninafuata Roho ya Mungu? Katika kujibu amesema: "Mtume Yohane anatupatia ushauri kuwa, “Wapendwa msifuate hisia ya kila roho (yaani kila hisia, kila tamanio, kila wazo) bali jiwekeni katika majaribu ya roho hizo, ili kuona kama kweli yanatoka kwa Mungu au katika ulimwengu").  Hii ina maana gani ya kujiweka katika jaribu la Roho? Kwa kujubu Papa amesema "Kwa urahisi ni kwamba iwapo wewe unahisi jambo, au  unakuwa na hamu ya kufanya jambo au wazo, au hukumu  ya kitu, jiulize kwanza: Je hisia ninayohisi inatoka katika Roho wa Mungu au inatoka katika roho ya ulimwengu?

07 January 2020, 13:33
Soma yote >