Papa Francisko:wakristo waoneshe furaha bila kufungwa na kasumba!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Hisia za kuwa na furaha ya mkristo ndizo zimekuwa kipaumbele cha mahubiri Papa wakati wa Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, Jumanne tarehe 28 Januari 2020. Ushauri huu umetokana na somo la kwanza la Kitabu cha Pili cha Samueli mahali ambapo kuna simulizi ya Daudi na watu wote wa Israeli wakifanya shangwe kuu kutokana na kurudishwa kwa sanduku la Agano la Mungu huko Yerusalemu
Siku kuu ya watu ni kwa sababu Mungu yuko karibu
Sanduku lilikuwa limetekwa nyara, anaeleza Papa na sasa linaporudi ni shangwe kuu kwa watu hao. Watu walihisi kuwa Mungu yuko karibu na ndiyo maana wanafanya siku kuu. Wakiwa na Mfalme Daudi alifanya maandamano nao, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana kwa kuwachinja ngómbe na kikono, watu walikuwa na cheleko, kelele, nyimbo na michezo. Ilikuwa ni siku kuu, furaha ya watu wa Mungu kwa maana Mungu alikuwa nao Papa amesisitiza. Na Daudi? Papa anajibu kwama “Akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote kwa wote, alielezea furaha yake bila aibu; ni furaha ya kiroho ya kukutana na Bwana. Mungu amerudi kwao, hiyo inawapatia furaha kubwa.
Daudi alifanya shangwe kwakuwa alikuwa anampenda Bwana
Daudi hakufikiria kama yeye ni Mfalme na kama mfalme kwa kawaida alipaswa kuwa mbali na watu, yaani, ukuu wake na umbali… Lakini Daudi anampenda Bwana na kuwa na furaha ndiyo maana ya tukio hili la kupeleka sanduku la Bwana Papa Francisko amesisitiza. Tukio alilofanya Daudi linaelezea furaha hiyo, kwa kucheza na kuimba kwa hakika kama watu wote. Aidha Papa Francisko amebainisha kwamba tendo hilo ni kama lile linatokea hata kwetu kuhisi furaha hasa tunapokuwa na Bwana na labda katika parokia au katika nchi yoyote inapotokea sikukuu ya watu. Kadhalika ametaja tukio jingine la historia ya Israeli walipopata kitabu cha Sheria, wakati wa enzi za Nabii Neemia, hata wakati huo watu walilia kwa furaha na kufanya siku kuuu.
Kudharau ghafla dhidi ya furaha
Maandishi ya Nabii Samweli yanaendelea kuelezea jinsi ya kurudi kwa Daudi nyumbani kwake, ambapo alimkuta mmoja wa wake, zake Mical, binti Sauli. Yeye alimkaribisha kwa dharau. Alipomuona mfalme akicheza, alimuonea aibu na kumkosoa akisema: Lakini je! hukuona aibu kwa kucheza kama mtu mchafu, kama mmoja wa watu?”. Kwa maana hiyo Papa Francisko anongeza: “ hii ni dharau halisi la kidini, dharau la ghafla dhidi ya furaha na Bwana. Daudi alimweleza mwanamke kwamba hii ilikuwa ni furaha ya ghafla kwa ajili ya Bwana. Ni furaha katika Bwana kwa kuwa tumerudisha Sanduku nyumbani! Lakini yeye aliendelea kudharau. Biblia inasema kuwa mwanamke huyo Mical, hakuweza kupata mtoto kwa tendo hili. Bwana alimpatia adhabu. Unapokosa furaha ya kuwa mkristo Papa amesema, huwezi kuzaa matunda; unapokosa furaha ya moyo hakuna matunda.
Inahitaji uinjilishaji wa furaha ili kwenda mbele
Papa Francisko akiendelea na mahubiri yake amebainisha kuwa, furaha haijifafanui kwa njia ya kiroho tu, bali inageuka ya kushirikishana. “Daudi siku hiyo baada ya kuwabariki akawagawia watu wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake”. Na ili kila mmoja aweze kufanya sikukuu katika nyumba yake. Kwa maana hiyo Papa anasema: “ Neno la Mungu halionewi aibu katika siku kuu”. Ndiyo mara nyingine kuna hatari ya furaha kuzidisha na kuamini kuwa ndiyo kila kitu lakini katika mantiki hii kwa hakika ilikuwa ni hali ya furaha ya siku kuu. Hata Mtakatifu Paulo VI anakumbusha katika Wosia wake wa Kitume wa “Evangelii Nuntiandi”, ambao anazungumzia mantiki hiyo na kushauri kuwa na furaha.
Kanisa na Injili vitajikita mbele ya safari kwa furaha na ujazo wa maisha
Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema: “Kanisa halitakwenda mbele na Injili haitakwenda mbele kwa njia ya uinjilishaji usio na furaha, au wenye uchungu, hapana. Kanisa litakwenda mbele kwa njia ya uinjilishaji wa furaha na uliojaa maisha. Furaha katika kupokea Neno la Mungu, furaha ya kuwa mkristo, furaha ya kwenda mbele, kuwa na uwezo wa kufanya siku kuu bila aibu na siyo kuwa kama yule mwanamke Mical yaani kuwa Mkristo au Wakristo rasmi, wakristo wafungwa wa sheria na kasumba.