Tafuta

Vatican News
Je ni kipimo gani ninatumia kupima wengine? Ni kipimo gani najipima mimi mwenyewe? Ni kipimo cha ukarimu kilicho kamili cha upendo wa Mungu au ni kipimo cha ngazi ya chini? Je ni kipimo gani nitahukumiwa? Je ni kipimo gani ninatumia kupima wengine? Ni kipimo gani najipima mimi mwenyewe? Ni kipimo cha ukarimu kilicho kamili cha upendo wa Mungu au ni kipimo cha ngazi ya chini? Je ni kipimo gani nitahukumiwa?  (Vatican Media)

Papa Francisko:tutahukumiwa kwa kipimo tunacho hukumu wengine!

Mtindo wetu wa maisha,namna yetu ya kufikiria wengine kwa hakika iwe ya kikristo kwa maana ya ukarimu na upendo mkuu usioogopa kunyenyekeshwa maana tutahukumiwa kadiri tunavyo hukumu wengine katika maisha yetu. Ni katika tafakari ya Papa Francisko wakati wa misa,akibainisha kile ambacho kimeoneshwa katika Injili ya Mtakatifu Marko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sentesi na ushauri wa Yesu leo hii aliopendekeza ni wenye utajiri  katika Injili ya Marko  ( Mk 2, 21-25). Na kati ya sentensi zilizotolewa  Papa Francisko amechagua mojawapo ili kutafakari kama kila mara afanyavyo kwa waamini katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, tarehe 30 Januari 2020. Kwa kipimo ambacho mnapima ninyi. Sisi sote katika maisha yetu ya kila siku, Papa amesema, tunatenda wakati uliopo, lakini zaidi  hayo tutafanya hata wakati wa mwisho wa safari yetu ya maisha, na ndiyo sentesi ya Yesu ambayo anathibitisha jinsi itakavyokuwa wakati ule, yaani itakavyokuwa hukumu ya mwisho

Kipimo ni mtindo wa kikristo

Hii ni kwa sababu ikiwa katika Heri za mlimani ambazo ni sawa sawa  na sura ya 25 ya Injili ya Matayo inayoonesha mambo ambayo tunatakiwa kuyatenda, namna gani ya kutekeleza, na  ambao tunapaswa kuishi, na  ndiyo kupimo  hicho ambacho Bwana anasema hata hapa”, amefafanua Papa Francisko.  Maswali ya kujiuliza ni kama haya: Je ni kipimo gani ninatumia kupima wengine? Ni kipimo gani najipima mimi mwenyewe? Ni kipimo cha ukarimu kilicho kamili cha upendo wa Mungu au ni kipimo cha ngazi ya chini? Je ni kipimo gani nitahukumiwa? Hakitakuwa kingine,   tofauti na ninavyo fanya. Ni kwa ngazi ipi ninajiweka? Ngazi ya juu? Papa anashauri ni lazima kufikiria hilo. Na hii hatuioni tu katika mambo mema tunayotenda au mambo mabaya tutendayo lakini katika mtindo unaoendelea wa maisha.

Mungu aliyejinyekeza ndiyo mtindo

Hata hivyo kila mmoja Papa Francisko amesema, anao mtindo wak , kwa namna ya kujipima binafsi, mambo na wengine na itakuwa ndivyo Bwana anatutumia kipimo hicho. Mwenye kipimo cha ubinafsi, atahukumiwa katika kipimo hicho; hasiye na huruma hata kama anapanda maisha, au anauwezo wa kukanyaga vichwa vya wote, atahukumiwa kwa namna hiyo ya ukosefu wa huruma. Papa Francisko anaongeza kufafanua mtindo wa maisha kuwa  kama mkristo ni lazima kujiuliza ni jiwe gani la kusimamia, jiwe la kufananisha ili kutambua iwapo niko katika ngazi ya kikristo au ngazi ambayo Yesu anapenda? Papa anatoa jibu kwamba ni uwezo wa kufedheheshwa na ni uwezo wa kudhalilishwa. Mkristo ambaye hana uwezo wa kubeba fedhaha  anakosa kitu. Yeye ni mkristo wa  rangi ya kupaka au kwa ajili ya faida binafsi. Akitoa mfano anasema : “Lakini kwanini Padre huyu?” Ni kwa sababu Yesu alifanya hivyo, alijinyenyekeza mwenyewe, anasema Paulo: “alijinyenyekeza  mpaka kufa na kifo cha  msalaba”. Alikuwa Mungu lakini hakushikamana na hilo: alijinyenyekeza. Huo ndio mfano.”

Ni kidunia, wadhambi, wajasiriamali au wakristo?

Kama maisha ambayo yanajieleza ya kidunia  na uwezo wa kufuata mtindo wa Yesu, Papa anatoa mfano na kutaja  kuhusu malalamiko wanayo mwambia Maaskofu wanapokuwa na matatizo hasa ya kufanya kuhamisha makuhani katika parokia na kwamba mara nyingi ina chukuliwa kama kuwekwa kwenye jamuiya ya chini na sio ya juu ambayo wangependa kupelekwa na hivyo makuhani kufanya uzoefu wa kuishi uhamisho kama adhabu. Kwa njia hiyo  Papa Francisko amebainisha kwamba: “kuna njia ya kutambua mtindo wangu, njia yangu ya kuhukumu, ya tabia ninayochukua mbele ya kunyenyekeshwa”. Aidha kuna njia ya kuhukumu kidunia, njia ya kumhukumu mwenye dhambi, njia ya kuhukumu mjasiriamali, njia ya kuhumu  Kikristo”.  Lakini kumbuka kuwa “kwa kipimo ambacho unapima wewe, kitakuwa ni  kipimo kile kile”. Ikiwa ni kipimo cha Mkristo, anayefuata Yesu, katika njia yake, itakuwa  vivyo hivyo hukumu.; ikiwa ni  kwa, huruma nyingi, na upendo mwingi  vile vile itakuwa hivyo. Lakini ikiwa kipimo changu ni cha kidunia na ninatumia imani ya kikristo tu kwa maana ninakwenda kanisani na kumbe ninaishi kidunia, vile vile nitapimwa na kipimo hicho. Amesisitiza Papa Francisko na kwa kuhimisha: “  Tumwombe Bwana  neema ya kuishi Ukristo na zaidi ya yote bila kuogopa  msalaba na  fedheha, kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Yesu amechagua kutuokoa na hii ndiyo inayohakikisha kwamba kipimo changu ni cha Kikristo hasa chenye  uwezo wa kubeba msalaba na uwezo wa kuteswa kwa  aibu fulani.

30 January 2020, 14:18
Soma yote >