Papa Francisko anasema ni haki ya kuponyesha magonjwa ya mwili lakini pia ni lazima kufikiria afya ya roho Papa Francisko anasema ni haki ya kuponyesha magonjwa ya mwili lakini pia ni lazima kufikiria afya ya roho  (ANSA)

Papa Francisko:msingi wa maisha ni uhusiano wetu na Mungu!

Magonjwa ya moyo yanapaswa kuponyeshwa na dawa ni kuomba msamaha.Ni maneno ya Papa Francisko aliyosema wakati wa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican akitafakari Injili kuhusu Yesu anayemponyesha kiwete.Ni haki ya kuponyesha magonjwa ya mwili lakini ni lazima kufikiria afya ya roho,maana kuna tabia ya kusahau bila kwenda kwa tabibu wa kweli.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Somo la Injili ya Siku kutoka Marko linawakilisha tukio la Yesu anapomponyesha Kiwete. Yesu yupo Kafarnaumu na watu wengi wamemzunguka. Kutokana na paa la nyumba kufunguliwa, watu waliokuwa wamebeba kiwete katika kitanda, wanamtelemsha mbele ya Yesu. Matumaini ya Yesu kumponyesha kiwete, lakini yanaacha watu bumbuwazi anapotamka: “mtoto, dhambi zako zimeondolewa”. Na baadaye anamuagiza asimame na kuchukua kitanda chake na kurudi nyumbani. Ni maneno ya tafakari ya Papa Francisko aliyosema wakati wa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, Ijumaa taraha 17 Januari 2020 akitafakari Injili iliyokuwa inahusu Yesu akiponyesha kiwete. Papa Francisko amesema, maneno yake Yesu yanaruhusu kwenda katika mambo yaliyo msingi. Yeye ni mtu wa Mungu, alikuwa anaponyesha, lakini hakuwa mganga, alikuwa anafundisha japokuwa alizidi walimu na mbele ya tukio hili anawakilisha jambo msingi zaidi. Alimtazama kiwete na kusema “ninasema, dhambi zako zimeondolewa”. Uponyaji wa kimwili ni zawadi, afya ya mwili ni zawadi ambayo sisi tunahitaji kuuhifadhi. Lakini Yesu anatufundisha kuwa afya ya moyo, yaani afya ya roho ambayo tunapaswa kuilinda.

Woga wa kwenda pale mahali ambapo kuna mkutano na Bwana.

Yesu anakwenda mahali penye msingi hata kwa mwanamke mdhambi, kama inavyo zungumza Injili mbele ya machozi. Dhambi zako zimesamehewa. Wengine walianza kukashifu wakati Yesu anapokwenda mahali pale penye maana, wanakashifu kwa sababu pale kuna unabii, pale kuna nguvu.   Na kwa mtindo huo Yesu anasema ‘nenda lakini usitende dhambi tena,’ alisema kwa mtu yule ambaye alikuwa hawezi kuingia katika Birika kuu la maji ili aweze kupona. Alimwambia Msamaria aliyekuwa anamuuliza maswali mengi na utafikiri kama mtaalimungu, Yesu alimuuliza mme wake yuko? Kwa maana hiyo Yesu anakwenda katika kiini, mambo muhimu ya maisha ambayo msingi ni ule uhusiano wako na Mungu. Na sisi tunasahau mara nyingi suala hili utafikiri tunayo hofu ya kwenda pale mahali ambapo kuna makutano ya Bwana, na Mungu.

Mambo mengi ya kufanya na kusahau afya za roho zetu

Sisi tuna mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya afya yetu ya mwili, tunapata ushauri kutoka kwa madaktari na madawa, ambapo ni jambo jema, lakini je tunafikiria hata afya ya moyo? Ni swali la Papa Francisko. Kuna neno moja la Yesu ambalo linaweza kutusaidia, amesema Papa Francisko. “mtoto dhambi zako zimesamehea”. Je sisi tumezoea kufikiria dawa hii ya msamaha wa dhambi zetu, na makosa yetu? Je mimi ninapaswa kuomba msamaha wowote wa Mungu? Kwa ujumla Papa amebainisha kuwa “jibu ni ndiyo kwa maana sisi sote tu wadhambi na moja baada ya nyingine lakini tunapoteza nguvu ya unabii ambayo Yesu alionesha kwa kwenda awali ya yote katika jambo msingi. Kwa maana hiyo leo hii, Yesu anamwambia kila mmoja kuwa: “ninataka kukusamehe dhambi zako.”

Msamaha ni dawa ya afya ya moyo

Kwa kuhitimisha: Papa ameendelea kusema kuwa labda mtu haoni dhambi ndani yake na kukiri kwa sababu inakosekana ndani mwake dhamiri ya dhambi. Ya dhambi halisi, ya magonjwa ya roho ambayo yanahitaji kuponywa na dawa ya kuponya ni msamaha. Ni jambo rahisi ambalo Yesu hutufundisha wakati anakwenda kwenye vitu vya msingi. Muhimu ni afya, yote: ya mwili na roho. Tuthamini ile ya mwili, lakini pia ile ya roho. Na tumwendee daktari huyo anayeweza kutuponya, anayeweza kutusamehe dhambi. Yesu alikuja kwa ajili ya hii, alitoa maisha yake kwa hili.

17 January 2020, 12:37
Soma yote >