Tafuta

Vatican News
Kuwa Mkristo mwema maana yake ni kuwa mpole katika Neno la Bwana, kusikiliza kile ambacho Bwana anasema kuhusu haki, juu ya hisani na upendo, juu ya msamha na huruma. Kuwa Mkristo mwema maana yake ni kuwa mpole katika Neno la Bwana, kusikiliza kile ambacho Bwana anasema kuhusu haki, juu ya hisani na upendo, juu ya msamha na huruma.  (Vatican Media)

Papa Francisko:kutii Bwana inasaidia kuwa huru!

Ni imani katika Neno la Mungu linaliweza kushinda miungu,kiburi na hali ya kujiamini zaidi kuliko mapenzi ya Bwana.Ndiyo tafakari ya Papa Francisko wakati wa misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican. Papa amekumbusha kwamba kuwa mkristo maana yake ni kusikiliza kile ambacho Bwana anasema juu ya haki,hisani na upendo,juu ya msamaha na juu ya huruma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuwa mkunjufu katika Neno la Mungu ambaye daima anatoa mapya, ndiyo ushauri wa Papa Francisko wakati wa tafakari ya Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican, Jumatatu asubuhi tarehe 20 Januari 2020. Papa Francisko akitafakari kuhusu Somo la kwanza, amesisitiza juu ukidi wa Sauli baada ya Nabii Samweli kutumwa na Mungu kuhusiana na suala la ufalme.

Hatua za ufisadi

Dhambi ya Sauli ilikuwa ni ile ya kukosa upole na ukunjufu  katika Neno la Mungu, kwa kufikiria kutasiri vyake kwamba labda ndiyo inayofaa. Na hii ndiyo chanzo cha dhambi ya kukosa upole amesisitiza Papa. Bwana alikuwa amemwambia hasichukue chochote cha watu aliokuwa amewashinda ,lakini hilo halikutendeka.Samweli alipokwenda kumkemea kwa mujibu wa Bwana na tazama  Sauli akamwambia Samweli, “watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana”. Papa amaesema, Yeye hakuweka chochote mifukoni mwake, lakini wengine ndiyo. Na zaidi katika tabia hii ya kutafsiri Neno la Munguu utafikiri yeye ndiye mwenye madaraka  na anaruhusu wengine waweze kuweka kitu chchote katika mifuko yao. Hatua za ufisadi kwa kawaida uanzia na tabia ya kutotii, ukosefu wa upeo na kwenda mbele hivyo hivyo , amesema papa Francisko.

Mungu hataki dhabihu

Baada ya kuwaangamiza kabisa wale Waamaleki Papa Francisko amekumbusha kuwa  watu watu  waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana. Lakini nabii Samweli anakumbusha kuwa badala ya dhabihu, na sadaka, anapendelea utii wa sauti ya Mungu kwa kuweka wazi thamani ya kiherakia. Ni muhimu kuwa na moyo mkunjufu na kutii kuliko kutoa dhabihu  kufunga na malipizi. Kwa maana hiyo dhambi ya dhidi ya  ukunjufu ipo hapo kupendelea unacho taka kuliko mapenzi ya Bwana. Na labda ndiyo dhambi ya kujifanyia miungu amesema Papa.  Ni kama vile kusema unaamini Mungu na kumbe unakimbilia kwa wapiga ramli ili kusoma miko yako kujua yatakayotokea.Kutotii Bwana ni ukosefu wa ukunjifu na kama kuamini miungu.

kukaidi mbele ya mapenzi ya Bwana ni kuasi

Unapokaidi mbele ya mapenzi ya Bwana wewe ni muasi, kwa sababu unapendelea ya kwako, ule muungu , dhidi ya mapenzi ya Bwana. Na ukosefu wa utii huo ulimgharimu sana na akakosa kuwa mfalme. Kwani Nabii Samweli anamwambia Sauli kuwa: “kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”. Jambo hili linapaswa kutufanya tufikiri kidogo juu ya ukunjufu wetu. Mara nyingi tunapendelea tafsiri yetu kuhusu Injili au ya Neno la Bwana la Injili. Mapenzi ya Bwana yako wazi, na yanaonekana katika Amri za Mungu kwenye Biblia na kufanya zionekane kwa njia ya Roho Mtakatifu ndani ya moyo. Lakini inapojitokza ukaidi na kubadili Neno la Bwana katika mawazo ya kiitikadi, basi ukakuwa ni muungu na siyo tena upole na utii.

Injili inakumbusha mapya na makuu

Papa Francisko akigusia Injili ya Siku kutoka kwa Mwinjili Marko, anakumbusha jinsi mitume walivyokuwa wanasemwa kutokana na kwamba walikuwa hawafungi. Lakini Yesu akawambia, "Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi. Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya. Huo ndiyo upya wa Neno la Bwana kwa sababu Neno la Bwana daima ni mambo mapya ambayo yanatupeleka mbele na kushinda daima na kuwa bora. Neno la Bwana linashinda miungu, linashinda kiburi, linashinda tabia ya kujiaminisha, na si kwa ajili ya Neno la Bwana, bali kwa ajili ya itikadi ambazo umejenga kuzungukia Neno la Bwana. Hata hivyo Papa amesema kuna sentesi moja nzuri ambayo Yesua anatumia na ambayo inatoka kwa Mungu katika Agano la kale isemayo: “Ninataka huruma na siyo dhabihu”.

Imani kwa Mungu

Kuwa Mkristo mwema maana yake ni kuwa mpole katika Neno la Bwana, kusikiliza kile ambacho Bwana anasema kuhusu haki, juu ya hisani na upendo, juu ya msamha na huruma, na siyo kutokuwa na busara katika  maisha, kwa kutumia itikadi za mawazo katika kutawala na kwenda mbele. Ni kweli kwamba wakati mwingine Neno la Mungu linatuweka katika matatizo lakini  pia hata shetani anafanya hivyo kwa kuadaa, amesema Papa. Kuwa mkristo kwa hakika ni kuwa katika huduma kwa njia ya kuwa na imani katika Mungu.

20 January 2020, 12:13
Soma yote >