Papa anashauri kusali:Bwana kama unataka,nihurumie na kuisali kwa moyo wa imani kwa Bwana ambaye yupo karibu nasi na kwa huruma yake atabeba matatizo yetu,dhambi zetu,magonjwa yetu ya ndani na kila kitu Papa anashauri kusali:Bwana kama unataka,nihurumie na kuisali kwa moyo wa imani kwa Bwana ambaye yupo karibu nasi na kwa huruma yake atabeba matatizo yetu,dhambi zetu,magonjwa yetu ya ndani na kila kitu  (ANSA)

Papa:Bwana yuko karibu nasi anabeba matatizo,dhambi na magonjwa yetu ya ndani!

Bwana yuko karibu nasi, kwa huruma yake na atabeba matatizo yetu,dhambi zetu na magojwa yetu ya ndani.Ndivyo Papa Francisko amethibitisha katika mahubiri yake wakati wa maadhimisho ya misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 16 Januari 2020,akitafakari juu ya Injili ya siku ambayo imekita juu ya uponyeshwaji wa mkoma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Bwana kama wataka. Ni sala rahisi na  ni tendo la imani na wakati huo ni changamoto ya kweli ambayo mkoma anamwomba Yesu ili amponye. Urahisi huo unakuja kutoka ndani ya kina cha mwoyo wake na ambao unaelezea wakati huo huo namna ya kutenda kwa Bwana mbele ya kukabidhi huruma ya kuteseka na kwa ajili yetu, ya kubeba mateso ya wengine juu yake, kutuliza na kuwaponya kwa jina la upendo wa Baba. Ndivyo Papa Francisko amethibitisha katika mahubiri yake wakati wa maadhimisho ya misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 16 Januari 2020 huku akitafakari juu ya Tukio la Injili ya siku ambalo limekita juu ya uponyeshwaji wa mkoma na kushauri waamini watazame kwa huruma ya Yesu aliyekuta kutoa maisha kwa ajili yetu sisi wadhambi.

Changamoto ya kweli

Katika tafakari yake Papa Francisko anaweka mkazo wa historia rahisi ya mkoma ambaye anamwomba Yesu amponye. Katika hilo kuna sala ambayo inashawishi Mungu na kupata suluhisho. Ni changamoto, anakiri Papa Francisko lakini pia ndiyo tendo la imani kuu. Na hii ni kwa sababu  Mimi ninatambua kuwa Yeye anaweza na hivyo nina mwamini Yeye”.  Je ni kwa nini mtu huyo alihisi ndani yake kufanya maombi ya namna hiyo? Papa anauliza na kujibu. Ni kwa sababu alikuwa anamwona Yesu anavyotenda. Mtu huyo alikuwa ameona huruma ya Yesu. Huruma na siyo adhabu”,  ndiyo  kiitikio cha Injili ambacho kilioneshwa katika uso wa mjane wa Naini, Mwanamke Msamaria, na Baba mwenye mtoto mpotevu, amebainisha Papa.

Huruma inamzunguka na ambayo inatoka ndani ya moyo wake na kumpelekea kutenda jambo. Huruma ni kuteseka na kukubaba mateso ya mwingine juu yake na ili kuweza kupata suluhisho kwa ajili ya kumponyesha. Na hii ilikuwa ni utume wa Yesu. Yesu hakuja kwa ajili ya kuhubiri sheria na baadaye kuondoka. Yesu alikuja kwa huruma, yaani ya kuteseka nasi na kwa ajili yetu na kutoa maisha yake. Upendo wa Yesu ni mkubwa hadi kumfikisha msalabani na kutoa maisha yake

Yesu hanawi mikono na kwenda zake, yuko nasi daima

Papa Franciski akiendelea na tafakari ametoa wito ili kuweza kurudia sentesi fupi. Yesu alishikwa na huruma, anauwezo wa kushirikisha maumivu, katika shida za wengine kwani yeye amekuja kwa hii, na sio kunawa mikono yake na kutengeneza mahubiri matatu, manne na kuondoka  zake, hapana.  Yeye yuko nasi kila wakati. “Kama wataka Bwana waweza niponesha, kama unataka unaweza nisamehee, kama wataka unaweza kunisaidia. Ndizo sala fupi anazopendekeza Papa na pia anasema ukitaka ongezea nyingine: “ Bwana mimi ni mdhambi, nihurumie”. Ni sala rahisi ambayo kila mmoja anaweza kurudia mara nyingi kila siku na kusema: “Bwana mimi ni mdhambi na ninakuomba unionee huruma”. Ni kwa kurudia mara nyingi kwa siku, ndani ya moyo na bila kutoa sauti kubwa bali kimoyo moyo tu.  “Bwana kama wewe wataka, unaweza. Na nionee huruma”.

Sala ya miujiza

Kwa sala yake rahisi na miujiza mkoma aliweza kupona na hii ni shukrani kwa huruma ya Yesu anabye anatupenda hata katika dhambi. Yesu hatuonei aibu kama vile mtu ambaye anaweza kusema: “ Tazama Padre mimi ni mdhambi, je nitawezaje kwenda na kusema hili na lile? Bora kwenda! Papa anaongeza, “kwa sababu Yeye alikuja kwa ajili yetu wadhambi, na kadiri dhambi ilivyo kubwa, ndivyo Bwana anazidi kuwa karibu nawe na amekuja kwa ajili yako, kwa ajili ya dhambi kubwa…, kwa ajili yangu mdhambi mkubwa… na kwa ajili yetu sote”. Papa Francisko amehimisha akisema “ kuweni na tabia hii ya kurudia sala iliyo rahisi isemayo:“Bwana kama unataka, nihurumie na kuisali kwa moyo wa imani kwa Bwana ambaye yupo karibu nasi na kwa huruma yake atabeba matatizo yetu, dhambi zetu, magonjwa yetu ya ndani na kila kitu.

16 January 2020, 13:25
Soma yote >