Tafuta

Vatican News
Katika siku hizi kabla ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, tumsifu Bwana kwa sababu ya zawadi yake ya bure ya wokovu na  kwa ajili ya zawadi ya bure ya maisha na kwa ajili ya zawadi zote za bure anazotujalia Katika siku hizi kabla ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, tumsifu Bwana kwa sababu ya zawadi yake ya bure ya wokovu na kwa ajili ya zawadi ya bure ya maisha na kwa ajili ya zawadi zote za bure anazotujalia  (ANSA)

Papa Francisko:Mungu ana uwezo wa kubadili yote.Tumshukuru wa neema zake!

Mungu ni mwenye uwezo wa kubadili yote na anatoa bure kwa maana anafanya kuchanua yasiyowezekana na kama jangwa lililojaa mchanga mkavu.Tumshukuru kwa ajili ya zawadi zake za bure maana yote ni kwa neema tu kutoka kwake.Ndiyo ujumbe wa Papa Francisko wakati wa mahubiri yake ya asubuhi Alhamisi tarehe 19 Desemba 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jangwa litachanua, amerudia rudia kusema Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake kwenye misa ya asubuhi tarehe 19 Desemba 2019 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, huku akiangaziwa na  masomo ya siku zaidi kwa Nabii Isaya. Na hiyo ni kutokana na Liturujia ya siku ambayo masomo yake yameonesha juu ya subir ana matumainia ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na ni masomo ambayo yametuweka mbele ya majangwa mawili, yaani kuhusu wanawake wawili waliokuwa  tasa kama Elisabeti mama yake Yoanhe Mbatizaji na mama yake Samsoni,amasema Baba Mtakatifu Francisko.

Bwana anafanya kuchanua maua katika jangwa

Ni Bwana anayefanya kuchanua maua katika jangwa amethibitisha Baba Mtakatifu. Wanawake wote wawili walipata mimba na kujifungua watoto. Kwa maana hiyo katika maswali hiyo si kwamba ni miujiza, bali  huo ni msingi wake Mungu  na ndiyo msingi wa imani yetu! Wanawake wawili waliweza kutunga mimba kwa sababu Mungu anao uwezo wa kubadili kila kitu hata sheria za asili; ana uwezo wa kutengeneza njia kwa kutumia Neno lake. Zawadi za Mungu ni za Bure. Maisha ya wanawake wawili hao, ni kielelezo cha zawadi ya bure ya Mungu, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha.

Yote ni neema tu, kutoka kwa Mungu

Akitoa mfano kuhusu tabia za wale wanaodai kuwa ni wakatoliki kwa sababu wanakwenda kila Domika katika misa, au wanahusika katika chama chochote cha kiparokia Baba Mtakatifu Francisko ameuliza masawali kuwa, je hao wanafanya nini? Wananunua wokovu wao? Je wanaamini kwamba hayo yatawaokoa wanayofanya? Na kumbe, jibu ni kwamba utaokoka tu kwa sababu wewe unaamini kutoka zawadi za Mungu  bure. Yote ni kwa neema tu!  amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Kwa kuhitimisha amesema kwamba, “ katika siku hizi kabla ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, tumsifu Bwana kwa sababu ya zawadi yake ya bure ya wokovu, kwa ajili ya zawadi ya bure ya maisha na kwa ajili ya zawadi zote za bure anazotujalia. Yote ni kwa neema tu kutoka kwa Mungu!

19 December 2019, 14:24
Soma yote >