Je Mungu akiamua kutuweka pembeni na kunawa mikono tutakuwa wa nani? Je Mungu akiamua kutuweka pembeni na kunawa mikono tutakuwa wa nani?  (ANSA)

Tusimweke Mungu pembeni kwa maana Yeye akifanya hivyo hatutaona mbingu!

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 16 Desemba 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican amesisitiza juu ya tabia mbili za ubaridi wa kikristo kwanza kama ile ya makuhani katika hekalu ya kumweka Mungu pembeni,pili ile ya kunawa mikono yao ambayo ni tabia mbaya sana hivyo ni vema kufikiria ni jambo gani lingetokea iwapo Bwana angetufanyia hivyo hivyo!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Katika mahubiri ya Baba Mtakatrifu Francisko Jumatatu tarehe 16 Desemba 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, amesisitiza juu ya tabia mbili za ubaridi wa kikristo kwanza kama ile ya makuhani katika hekalu ya kumweka Mungu pembeni na ya kunawa mikono yao na ambayp anasema ni tabia mbaya sana na hivyo ni vema kufikiria ni jambo gani lingetoke iwapo Bwana anagefanya hivyo hivyo kwetu sisi!Yesu anakabiliana na makuhani katika hekelu. Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kwamba Yesu alikuwa anawashauri watu, alikuwa anawaponya, anawafundisha na kufanya miujiza na kwa sababu hiyo viongozi hao walikuwa wamekasirika, kwa sababu ya utamu wa maneno yake na kujitoa kwa watu wakea mbaye aliwez anawavutia wote kwenda kwake. Wakati wao na wafanyakazi wao walikuwa wanaheshimiwa na watu tu, lakini walikuwa hawawezi kuwakaribia kwa sababu hawakuwa na imani kwao. Kutokana na hiyo makuhani hao wanakubaliana wao kwa wao kumweka Yesu pembezoni. Na wanajifanya kumuuliza ni kwa mamlaka gani anafanya mambo hayo? Na kwa hakika Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba  wao wanasema “wewe siyo kuhani, siyo mwalimu wa sheria, hukusoma katika vyo vikuu vyetu. Wewe ni kitu bure.”

Kufuatia na jibu la Yesu, wao wananawa mikono

Yesu kwa akili yake anajibu kwa swali jingine na kuwaweka makuhani hao pembeni, akiwauliza juu ya Ubatizo wa Yohane Mbatizaji alikuwa anatumia mamlaka gani, kutoka mbinguni yaani kwa Mungu au kwa watu. Mwinjili Matayo anaelezea bayaba juu ya mawazo yako akisema “ iwapo tutasema kutoka mbinguni, Yeye atauliza  ni kwa sababu gani hamkuamini? Na iwapo tutasema ni kutoka kwa watu, waamini watakuja juu dhidi yao. Kwa maana hiyo wananawa mikono yao na kusema: “Hatujuhi” Kwa jibu hilo, Baba Mtakatifu anabainiusha kwmba  hii ni tabia ya kutokuwa na akili nyingi kwa maana ni wahongo wa imani. Hata hivyo siyo tu hao pia Pilato alinawa mikono yake, kwa njia hiyo hata hawa wanawanawa mikono yao.  wakisema “Hatujuhi”. Hawa hawaingii katika historia ya watu na wala kujihusisha na matatizo, na wala hawawezi kupambana kwa ajili ya wema na wala kupambana kwa aili ya kuponesha watu wengi wenye kuhitaji. Ni bora kutofanya hivyo na wala bila kuthubutu wahataki kujichafua.

Tabia mbili za mkristo ni kama maji juu ya ua la waridi

Kwa mana hiyo  Yesu anawajibu sawasawa na jibu lao kwamba “ hata mimi siwambii ni kwa mamlaka gani ninafanya hivyo”. Kuna aina mbili za tabia ya wakristo walio baridi ndani mwetu, akimtumia Bibi yake kuwa alikuwa anasema watu kama hao ni kamawakristo wa maji juu ya ua la waridi. Ikiwa na maana ya wakristo wa namna hivi hivi , bila kuwa na msimamo. Ni tabia ambayo inamweka Mungu pembeni. Yaani  “ninafanya hili au nitakwenda kanisani. Lakini je Yesu anajibu nini ? nenda, nenda jijue…. Baba Mtakatifu amefafanua.

Wakristo wote amabo wanaingia katika chama cha Mtakatifu Pilato

Tabia nyingine wa wakristo baridi anabainisha Baba Mtakatifu ni ile ya kunawa mikono kama wale wafuasi wa Emau  kwa siku ile ya asubuhi ya Ufufuko wa Bwana. Hao waliwaona wanawake wote wakiwa na furaha kwa sababu ya kumwona  Bwana, lakini hawakuwaamini et kwa sababu walikuwa ni wanawake, wenye kuwa na hisia nyingi na hivyo wakanawa mikono yao. Kwa njia hiyo Baba Mtakatiu amesema waliingia katika chama cha Mtakatifu Pilato! Wakristo wengi wananawa mikono yao mbele ya changamoto za utamaduni za historia chanagamoto za watu wa wakati wetu; hata mbelee ya changamoto ndogo zaidi. Mara ngapi tunasikia wakristo walio wabahiri  mbele ya watu ambao wanaomba omba na awawapi chochote. Kwa kudai kuwa “Hapana, hapana kwa sababu hawa baadaye watakwenda kulewa”. Wananawa mikono yao  kwa kudai kwamba mimi sitaki watu walewe na hivyo siwapatii chochote.

Je watu wasio kuwa na chakula: ni vema kutengeneza nafasi ndani ya miyo kwa ajili ya Bwana

Hata hivyo Baba Mtakatifu anauliza swali, je watu hawa wana chochote cha kula…. Jibu ni kwamba watajijua, mimi sitaki kwamba walewe. Tunasikia mara nyingi habari hizo anathibitisha. Kumweka Mungu pembeni na kunawa mikono ndiyo tabia mbaya sana kwa sababu ni kama kumchangamotisha Mungu. Baba Mtakatifu anatoa tafakari, ili tufikirie ni kitu gani kingetokea iwapo Bwana angetuweka pembeni. Kamwe tusingeweza  kuingia mbinguni.Je ni kitu gani kingetokea iwapo Bwana angenawa  mikoni yake dhidi yetu? Sisi ni maskini. Tabia ya unafiki kwa walioelimishwa ni ile ya kusema hapana , sijichanganyike anathibitisha Baba Mtakatifu. Na kwa maana hiyo sauti ya wanafiki walioelimisha wanaweka watu pembeni, kwa sababu watu hao ni wachafu, na mbele yao watu hao wananawa mikono, na  kwa sababu wanasema  watajijua. Kwa kuhitimisha amesema iwapo ipo hali halisi hiyo ya tabia kama hizo basi ni vema kutengeneza nafasi ndani ya mioyo kwa ajili ya Bwana anayekuja!

16 December 2019, 12:56
Soma yote >