Tafuta

Mtume Paulo alimpenda Yesu upendo wa dhati hadi kuhisi Bwana anamsidikiza daima katika yote yawe mambo mazuri na mabaya Mtume Paulo alimpenda Yesu upendo wa dhati hadi kuhisi Bwana anamsidikiza daima katika yote yawe mambo mazuri na mabaya  (ANSA)

Ni kwa jinsi gani ilivyo ngumu kuelewa upendo wa Yesu!

Katika misa takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta,Baba Mtakatifu anashuri kutambua upendo wa Mungu katika Yesu na kama ilivyo kwa kila mmoja wetu.Ni kwa njia hiyo tu,tunaweza kuwa na uelewa halisi wa upendo wa Yesu.Kinyume chake ni vigumu kuutambua.Mtakatifu Paulo alimpenda Yesu upendo wa dhati hadi kuhisi Bwana anamsidikiza daima katika yote,mambo mazuri na mabaya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika misa yake  asubuhi tarehe 31 Oktoba 2019, katika Kanisa la  Mtakatifu Marta amehimiza kuwa na utambuzi  wa upendo wa Mungu katika Kristo na kushauri kuomba roho Mtakatifu ili atufanye tuelewa upendo wa Yesu na kujandaa mioyoni mwetu ili tuache tupendwa na Bwana. Akiangazwa na somo la kwanza kutoka katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi.  Baba Mtakatifu ameelezea ni kwa jinsi gani Mtume wa watu utafikiri alikuwa anajigamba sana na kiburi cha kujiamini, hasa anaposema kuwa yawe mateso, uchungu, njaa, utupu, hatari na upanga havitaweza kumtengenisha kamwe na upendo wa Kristo!

Njia ya upendo upeo anaotuonesha Paulo

Lakini pamja na  hayo yote, Mtakatifu Paulo anaonesha kwamba sisi ni washindi kwa njia ya upendo wa Bwana. Mtakatifu Paulo alikuwa hivyo tangu wakati ule akiwa njia kuelekea Damasko ambapo alielewa fumbo la Kristo. Na tangu hapo alimempenda Kristo kwa upendo wa nguvu na siyo upendo wa mchezo. Mtume Paulo alimpenda Yesu upendo wa dhati hadi kuhisi Bwana anamsidikiza daima katika  yote, yawe mambo mazuri na mabaya. Paulo alitambua katika maisha yake binafsi upendo mkuu wa Kristo na ndiyo njia anayotufanya kuiona Paulo yaani  njia ya pendo na kuendelea mbele, Baba Mtakatifu amefafanua.

Kutoa maisha kwa ajili ya wengine kama vile mama na mwanae

Upendo wa Kristo siyo rahisi kuufafanua kwa maana ni jambo kubwa , anabainisha Baba Mtakatifu. Ni yeye aliyetumwa na Baba ili kutukumboa na alifanya hivyo kwa upendo upeo hasa wa kutoa maisha kwa ajili yetu. Hakuna upendo zaidi kama ule wa kutoa maisha kwa ajili ya mwingine. Baba Mtakatifu anatoa mfano wa kutazama mama. Upendo wa mama daima ni kwa ajili ya maisha ya mwanae, kwamna  anamsikindikiza daima katika maisha, na  katika kila hali ya vipindi view vigumu  na rahisi. Ni upendo ulio karibu nasi na siyo upendo wa kubabaisha kwa Bwana bali kuwa na upendo kama wa Yesu alioutoa kwa kila mmoja wetu.

Machozi ya kila mmoja wetu

Katika Injili ya Luka Baba Mtakatifu Francisko amebainisha jambo moja la upendo wa dhati alionao Yesu. Anabainisha hayo wakati wa kuzungumza juu ya Yerusalemu ambayo Injili inathibtisha kwamba Yesu aliwapokea na kuwakumbatia watoto wake kama vile kuku akihatamia vifaranga vyake. Na kwa maana hiyo alilia Yerusalemu. Upendo wake Yesu unampelekea kutoa machozi na machozi ambayo ni ya kila mmoja wetu…Yesu angeweza kuhukumu Yerusalemu anasema baba Mtakatifu na kuongeza yaani kuisemea mabaya… analalamika kutokana na kwamba hawakutaka kupendwa kama vifaranga vilivyoko kwenye kiota. Huruma ya Mungu katika Yesu ndiyo aliyo itambua Mtakatifu Paulo. Na iwapo sisi hatufikii kuhisi na kutambua huruma na upendo wa Mungu katika Yesu kama ilivyo kwa kila mmoja, kamwe hatutoweza kutambua maana ya Upendo  halisi wa Kristo. Upendo daima unasubiri, unavumilia, upendo unacheza karata ya mwisho hata kwa Yuda. Rafiki ambaye Yesu alitaka kumpatia fursa ya ya hatari ya kifo hadi mwisho. Hata kwa wadhambi wakubwa Yesu  anapenda hadi mwisho.  Baba Mtakatifu ameuliza: sijuhi kama hata sisi tunafikiria Yesu namna hii, ambaye alilia, kwa jinsi gani alilia mbele ya kaburi la Lazaro na kama alivyo ililia akitazama mji wa Yerusalemu.

Upendo ambao unatoa machozi

Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko ameshauri kuomba Yesu ile neema ya kulia. Yeye ambaye alitupatia mambo mengi na wakati sisi mara nyingi tunachagua kwenda njia nyingine. Upendo wa Mungu unakuwa ni machozi, machozi ya huruma ya Yesu . Na ndiyo maana Mtakatifu Paulo alikuwa amependa Kristo na hakuna yoyote angeweza kumtengenisha na Yeye.

31 October 2019, 13:00
Soma yote >