Tafuta

Vatican News
Papa anasema matumaini ni jambo gumu kulielewa na ndilo la kinyenyekevu kati ya fadhila Papa anasema matumaini ni jambo gumu kulielewa na ndilo la kinyenyekevu kati ya fadhila  (Vatican Media)

Matumaini ya mkristo yawe kama nanga iliyotupwa katika forodha!

Ili kuwa watu wenye matumaini lazima kuwa kama nanga yenye kushikamana na kamba nzito ili kwenda kukutana na Bwana.Ukipoteza mtazamo huo maisha yanasimama na mambo hayaendi na kuharibika.Ndiyo ushauri wa Baba Mtakatifu wakati wa mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican tarehe 29 Oktoba 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Franciso  katika mahubiri yake kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 29 Oktoba 2019 ametumia mfano wa kuwa na matumaini kama vile kutupa nanga katika forodha, huku akiwashauri waamini waishi kwa nia ya kukutana na Bwana la sivyo ni kuishia katika maisha mabaya na ambapo  maisha ya kikristo yanatarishwa  na mafundisho ya kifalsafa. Tafakari yake imeanzia katika Somo la liturujia ya siku kutoka Mtakatifu Paulo kwa Waroma  8, 18-25, mahali ambapo Mtu anaimba wimbo wa matumaini.

Baadhi ya waamini walikuwa wamelalamika

Kwa uhakika baadhi ya waroma walikwenda kulalamika na hivyo Paulo anawashauri watazame mbele. “Nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu”. Aidha Baba Mtakatifu amesema kwamba  anasena pia hata akizingumzia juu ya kazi ya uumbaji unaotazama kwa shauku nyingi kufunuliwa. Haya ni matumaini ya kuishi kwa ajili ya kufunguliwa kwa Bwana na kukutana naye. Kwa maana hiyo Baba  Mtakatifu anathibtisha kuwa inawezakana kupata mateso na matatizo, lakini hayo ni ya kesho, wakati leo hii kuna ahadi ambayo ni Roho Mtakatifu na ambaye anasubiri,  anafanya kazi tayari muda huu. Matumaini kwa hakika ni kama vile kutupa nganga katika  ambayo imefungamana na kamba kubwa na nzito. Hata hivyo siyo sisi kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu , kuingia katika utukukuf wake. Na hata sisi tuna kipaumbele dhamana ya  Roho, japokuwa tunaugua kwa undani huku tukuwa huru  na kuondolewa katika utumwa wa uharibifu.

Hatuwezi kutengeneza kiota duniani,tunaelekea kwa mbinguni

Matumaini ndivyo yalivyo yalivyo daima na hatuwezi kutengeneza kiota duniani. Maisha ya kikristo yana mtazamio mwingine zaidi. Iwapo Mkristo anapoteza mantiki hiyo, maisha yake yanasimama na mambo hayawezi kwenda mbele na yanaharibika. Kwa mfano huo zaidi amesema Baba Mtakatifu kuwa  tazama maji yaliyotuama, ambayo hayatiririki yanaharibika. Mkristo yoyote hasiyekuwa na uwezo wa kuwa na matarajio,  nia ya kuelekea forodhan nyingine, anakosa jambo na ataishia kuharibika. Kwa upande wake, maisha yatakuwa kama mafundisho ya kifalsafa na kuishi hivi hivi baadaye atasema anayo imani na kumbe hata matumaini hana.

Ni vigumu kugundua matumaini

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha ni kwa jinsi gani ilivyo ngumu kujua matumaini. Iwapo tunazungumza juu ya imani, anasema tunamaanisha  imani kwa Mungu aliyetuumba, katika Yesu aliyetukomboa na kusali sala ya nasadiki kwa utambuzi wa mambo ya imani kwa dhati. Iwapo tunazungumza juu ya upendo, unajikita juu ya kuwatendea yaliyo mema jirani na katika matendo mengi mengi ya upendo kwa wengine. Lakini matumaini ni jambo gumu kulielewa na ndilo la kinyenyekevu kati ya fadhila na ambazo ndiyo za kimasikini ambazo tunaweza kuwa nazo.

Lazima kuwa masikini bila kushikilia chochote

Iwapo tunataka kuwa wanaume na wanawake wa matumaini lazima kuwa maskini, na tusioshikilia kitu chochote. Tunapaswa kufunguka kuelekea katika forodha nyingine au au upande mwingine. Matumaini ni unyenyekevu na fadhila inayofanya kazi, kila siku . Na Kila siku lazima kuwa nayo, kila siku lazima kukumbuka na kuwa kama nanga ambayo imesimika pale na ipo mikononi. Kila siku ni lazima kukumbuka kuwa tunayo dhamana ambayo ni roho Mtakatifu anayefanya mambo mengi  na yaliyo madogo. Ili kutambua kuishi matumaini, Baba Mtakatifu Francisko amejikita kutazama mafundisho ya Yesu kupitia Injili ya siku  (Lk 13,18-21) anapofananisha na Ufalme wa Mungu kama mbegu ndogo iliyotupwa shambani. Tukisubiri kila siku kuona kama inakua anasema haitawezekana kamwe. Bali ni kuisubiri kukua kwa njia ya vumilivi , kama asemavyo Mtakatifu Paulo kwamba , matumaini yanahitaji subiri.  Ni subira  ambayo inatoka kwa Mungu tu kwani mpanzi anapanda na Mungu anafanya mbegu.

Matumaini ya mpanzi ni madogo

Matumaini ya mpanzi ni madogo sana, kwasababu  ni kupanda mbegu na kuacha ili ardhi iweze kukuza mbegu hiyo.Yesu katika kuzungumzia matumaini katika  Injili ya Siku anatuma picha pia  ya chachu, ambayo mwanamke amechanganya katika unga. Hiyo ni chachu isiyotunzwa kwenye friji bali inajikita katika maisha  ya kila siku, kama ilivyo mbegu iliyofunikwa chini ya ardhi.

29 October 2019, 14:12
Soma yote >