Tafuta

Sala inatoa nguvu na kuamsha dhamiri ya zawadi ambazo hatupaswi kudharau maana ndiyo huduma ya mtumishi wa Mungu. Sala inatoa nguvu na kuamsha dhamiri ya zawadi ambazo hatupaswi kudharau maana ndiyo huduma ya mtumishi wa Mungu.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Maaskofu wawe na ukaribu na mapadre,mashemasi na watu wa Mungu!

Katika misa ya Baba Mtakatifu Francisko,kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican tarehe 20 Septemba 2019 amekazia kuhusu aina nne za ukaribu katika huduma ya kiaskofu,ikijumuishwa ile ya baraza la Maaskofu,ukaribu wa Mungu na sala;ukaribu wa mapadre kwa maaskofu wao,Askofu kwa mapadre wake;ukaribu wa Mapadre kati yao na Maaskofu kati yao pamoja na ukaribu wa watu wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maaskofu wawe karibu na Mungu kwa sala, wawe karibu na mapadre na kati yao na miwhso wawe karibu watu wa Mungu. Ndiyo njia aliyoelekeza Baba Mtakatifu Francisko asubuhi tarehe 20 Septemba 2019 wakati wa misa yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Tafakari yake, kimetokana na Somo la Litirujia ya tarehe 19 na 20 Septemba inayojikita na ushauri wa Mtume Paulo akimpatia kijana Askofu Timoteo, ahata hivyo ni ushauri ambao baadaye umefuata katika Somo la Injili.

Alhamisi 19 Septemba kiini cha tafakari kilikuwa kinahusu ushauri uliotolewa wa kutodharau huduma kama zawadi. Na Ijumaa 20 Septemba moyo wa tafakari yake Baba Mtakatifu Francisko umejikita kuhusu fedha, lakini pia hata tahadhari ya mateto, majadiliano yasiyo na maana ambayo Baba Mtakatifu amesema  kuwa, yote hayo yanadhoofisha maisha ya utoaji wa huduma ya kikuhani. Iwapo kuna padre, shemasi na askofu anaanza kushikilia fedha, anajifunga katika mzizi ya mabaya yote, kwa mujibu wa Somo la Kwanza ambalo Mtakatifu Paulo amegusia kuhusu  onyo la upendeleo wa fedha  ni mizizi wa mabaya yote (1Tm 6,2-12). Baba Mtakatifu kwa akikumbusha alivyo sema mara nyingi kwamba wazee wa zamani walikuwa wanasema kuwa fedha “ni ibilisi anaingia katika mifuko”.

Akikazia mahubiri yake Baba  Mtakatifu kwa maana hiyo inajikita na ushauri wa Mtume Paulo kwa Timoteo na suala la huduma katika Barua zote mbili. Wale ambao wanapaswa kuwa karibu wanaalikwa, siyo maaskofu tu lakini pia mapadre na mashemasi. Kufuatana na hilo, Baba Mtakatifu,ameelekeza ukaribu wa aina nne wa uotiaji wa huduma kwa upande wa Askofu. Kwanza  Askofu ni mtu wa karibu na Mungu. Na kwamba ili mitume waweze kuhudumia vema wajane na yatima waliavumbua na kuanzisha  njia ya huduma ya ushemasi kwa maana  Petro anathibitisha ya kwamba “mitume wanapaswa kusali na kutangaza Neno”. Kwa maana hiyo, zoezi la kwanza ni kusali, Sala inatoa nguvu na kuamsha hata dhamiri ya zawadi ambazo hatupaswi kudharau maana ndiyo huduma, Baba Mtakatifu amekazia.

Njia ya pili ya ukaribu Askofu anaalikwa kuwa na wajibu wa mapadre ni wake, mashemasi na wahudumu wake ambao wako karibu naye zaidi. “wewe unapaswa  kupenda jirani ambao ni mapadre wako na mashemasi wako”. Anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwalenga maaskofu. Akitoa mfano amesema, ni huzuni sana iwapo askofu anasahau mapadre. Ni huzuni kusikia manung’uniko ya mpadre wakisema: “nimemwita Askofu, maana ninashida ya kukutana naye na kumwambia kitu na katibu wake amesema hakuna nafasi hadi miezi…”. Askofu anayehisi ukaribu wa mapadre wake, anapoona padre  wake amemwita siku hiyo, au angalau siku inayofuata, anapaswa kumtafuta, kwa maana anayo haki ya kujua na kutambua kuwa yeye ni baba. Ukaribu wa mapadre ni muhimu. Na mapadre wanapaswa kuishi na ukaribu kati yao na siyo kuwa na migawanyiko. Shetani anaingia pale penye migawanyiko kwa ajili ya kugawa makuhani hao. Katika kugawanyika, inawezekana pia kutengeneza makundi kufuatana na mawazo ya kiitikadi.

Ukaribu wa aina ya tatu ni ule wa mapadre kati yao, na wa nne ni ule wa watu wa Mungu: Katika Barua ya Pili ya Mtume Paulo unaanza kusema kuwa Timote hakusahau mama yake na bibi yake yaani hakusahau mahali alipotoka, mahali ambao Bwana alimtoa. Usisahau watu wako, usisahu mzizi yako. Na kama Askofu na kama padre, anahitaji kuwa na ukaribu daima na watu wa Mungu. Iwapo Askofu anajitenga na watu wa Mungu, anaishia kuleta hali za mawazo tofauti ambayo haina maana na na wala kuhusiana na  utumishi, na siyo utumishi bali ni kutumikiwa. Kwa maana hiyo Askofu amesahau zawadi ya bure ambayo alipewa.

Akihitimisha Baba Mtakatifu Francisko amerudia kuhimiza ili wasisahau aina nne za ukaribu,ikijumuisha ile ya baraza la Maaskofu. Hata hivyo anashauri kuwa na mang’amuzi na kuwaalika wasali ili maaskofu na mapadre waweze kuwa na ukaribu kati yao, hata kwa ajili ya wakubwa wao ambao wanawasaidia kufikia njia ya wokovu. Lazima kusali kwa ajili ya mapadre wao, kwa ajili ya paroko, makamu wake na siyo kuwateta. Papa ni Askofu na ili waweze kutambua kutunza zawadi na siyo kuidharau zawadi ambayo walipewa ya ukaribu na muumba.

20 September 2019, 13:00
Soma yote >