Tafuta

Vatican News
Bwana alijawa na huruma kubwa kuwaona watu kama vile wasiokuwa na mchungaji Bwana alijawa na huruma kubwa kuwaona watu kama vile wasiokuwa na mchungaji  (Vatican Media)

Papa Francisko:Jambo la kuwa na huruma pia ndiyo lugha ya Mungu!

Kuwa na huruma ni kama kuwa na miwani ya moyo inayokufanya utambue ukuu wa hali halisi,lakini pia ndiyo lugha ya Mungu na wakati huo huo mara nyingi lugha ya kibinadamu ni ile ya sintofahamu.Ndiyo moja ya tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri wakati wa Misa Takatifu kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta,Vatican,tarehe 17 Septemba 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika misa yake ya asubuhi tarehe 17 Septemba 2019, kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, ametoa mwaliko wa kufungulia moyo wa huruma na siyo kujifungia binafsi katika sintofahamu. Huruma kwa dhati inapelekea katika njia ya haki ya kweli katika kutukomboa dhidi ya ubinafsi wetu. Tafakari yake imetokana na sehemu ya Injili ya Mtakatifu Luka katika Liturujia ya siku  (Lc 7,11-17) ambapo Mtakatifu Luka anasimulia kisa cha mwanamke mjane wa Naim aliyekuwa anaomboleza kwa sababu ya kifo cha mwanae wa pekee wakati wanakwenda kwenye mazishi.

Mwinjili hasemi kwamba Yesu alikuwa na huruma bali anathibitisha kwamba, “Bwana alijawa na huruma kubwa” anabainisha Baba Mtakatifu Francisko na kwamba ni kama kusema Bwana aliathiriwa na huruma. Kulikuwa na umati mkubwa uliokuwa unamsindikiza mwanamke huyo, lakini Yesu aliona hali halisi hiyo. Mwanamke alikuwa amebaki peke yake na wakati huo Yesu akamrudishia mwanae. Ni huruma kwa dhati ya kukufanya utambue kwa kina hali halisi. Huruma inakufanya utazame uhalisia ulivyo; aidha kuwa na huruma ni kama kuwa na miwani ya moyo, inayotufanya tutambue ukuu wa hali halisi ilivyo. Katika Injili mara nyingi Yesu anashikwa na huruma,na kwa maana hiyo kuwa na huruma pia ni lugha ya Mungu, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Huruma siyo kamba inaanzia katika Biblia tu, pia anaoinesha Yesu mwenyewe. Kwa kutoa mfano zaidi Baba Mtakatifu Francisko amesema, Mungu alianza kumwambia Musa, “nimeona uchungu wa watu wangu (Kut 3,7);  na kwa maana hiyo ni huruma ya Mungu ambaye anamtuma Musa kwenda kukomboa watu wake. Mungu wetu ni Mungu wa huruma na huruma hiyo inaweza kufafanuliwa kama kwamba ni udhaifu wa Mungu, lakini pia kusema kuwa ni nguvu yake. Kilicho bora zaidi yetu ni kwa sababu yeye alikuwa na huruma ambayo ili msababisha amtume mwanae kati yetu. Huruma ni lugha ya Mungu! Huruma siyo hisia tu ya kijuu, ya kuhisi kwa mfano, wa kuona mbwa amekufa njiani na kuanza kuwa na huruma kidogo na kusema maskini. Huruma hii inajihusisha na tatizo la wengine hasa katika uthubutu wa maisha. Bwana kwa hakika anathubutu katika maisha na kwenda pale.

Mfano mwingine ambao Baba Mtakatifu ameutoa katika Injili ni kutoka sehemu nyingine kuhusu  wingi wa mikate, ambapo Yesu aliwambia mitume wake wawapatie chakula waliokuwa wamemfuata kabla ya kuwaaga. Baba Mtakatifu anasema, mitume walikuwa na busara, kwa kufikiria jibu alilowambia mitume kuwa, “wapeni chakula ninyi”.  Jibu lake lakini lilikuwa la kubeba matatizo ya watu bila kufikiria baada ya siku hiyo kuweza kwenda vijijini kununua mikate. Katika Injili inasema, Bwana alikuwa na huruma ya kuona watu wale kama kondoo bila mchungaji. Kwa upande mwingine ishara ya Yesu ni ya huruma na kwa upande mwingine, kuna ubinafsi wa mitume wanaotafuta suluhu, lakini bila ahadi ya kutotaka kuchafua mikono yao, ya kwamba wajijue wenyewe. Na ndipo inajionesha huruma yaani ndiyo lugha ya Mungu. Mara nyingi lugha ya binadamu ni ya sintofahamu. Kuubeba mzigo bila kufikiria lolote zaidi.

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua juu ya suala la sintofahamu amesema mmoja wa wapiga Picha wa Osservatore Romano alipiga picha ambayo iko kwenye ofisi ya sadaka ya kitume na picha hiyo inatwa Sintofahamu. Baba Mtakatifu aidha amekumbusha alivyo kwisha zungumza mara nyingi kuhusu suala hili. Kwa maana hiyo anasimulia kuwa moja ya usiku wa baridi, mbele ya hoteli ya kitajiri, mwanamke mmoja aliyekuwa anaishi barabarani, alimyoshea mkono wa kuomba mwanamke mmoja aliyekuwa anatoka katika hoteli hiyo amejifunika vizuri na mwanamke huyo alitazama pembeni. Baba Mtakatifu amesema amesema hiyo ndiyo inaitwa sintofahamu! Amewaalika waaamini watazame picha hiyo, picha ya sintofahamu. Sintofahamu zetu. Ni mara ngapi tunatazama sehemu nyingine… na tunafunga milango ya huruma. Hata hivyo Baba Mtakatifu pia amependa Neno la Injili ya siku ambapo Yesu anamwambia mama huyo asilie. Anambembeleza kwa huruma. Yesu anagusa jeneza na kuwaambia kijana aamke. Kijana huyo aliamka na kuanza kuzungumza na baadaye alimrudishia mama mtoto wake. Kurudishia ni tendo la haki Baba Mtakatifu amesisitiza. Katika neno jingine linalotumika kama haki ni kurudishia. Huruma inatufikisha katika njia ya haki ya kweli. Daima kuna haja ya kurudishia haki wale wenye kustahili haki yao na ndiyo kinacho tukomboa dhidi ya ubinafsi, sintofahamu, na kujifunza sisi binafsi. Baba Mtakatifu amewaombea kuendelea katika liturujia ya ekaristi na wazo hili: “Bwana alishikwa na huruma kubwa”, na ili aweze kuwa na huruma ya kila mmoja wetu kwa maana wote tunahitaji

17 September 2019, 13:33
Soma yote >