Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu wakati wa Misa takatifu asubuhi amehimiza kusali hata kwa ajili ya watawala na wanasiasa ili waweze kupeleka mbele wito wao kwa hadhi. Baba Mtakatifu wakati wa Misa takatifu asubuhi amehimiza kusali hata kwa ajili ya watawala na wanasiasa ili waweze kupeleka mbele wito wao kwa hadhi.  (ANSA)

Papa Francisko amesisitiza kuombea wakuu wa nchi na wao pia waombee watu wao!

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican,tarehe 16 Septemba 2019,ametafakari juu ya somo la Mtakatifu Paulo kwa Timotheo akisisitiza kunyosha mikono juu na kusali hata kwa ajili ya watawala.Katika mada hiyo ameangazia nchi ya Italia ambayo imeishi kipeo cha serikali hivi karibuni na kuuliza swali kama watu kweli wameombea viongozi,serikali na bunge.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kusali hata kwa ajili ya watawala na wanasiasa ili waweze kupeleka mbele wito wao kwa hadhi, ni moja kati ya maombi ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa yake ya asubuhi tarehe 16 Septemba 2019, katika Kanisa la Mtakatifu Marta mara baada ya kipindi hiki cha likizo ya kiangazi. Baba Mtakatifu Francisko akitafakari juu ya Somo la Barua ya kwanza ya  Mtakatifu Paulo kwa Timotheo, amefafanua ni jinsi gani aliwashauri watu wa Mungu wasali katika maombi ulimwengu. Lakini ni  kufanya hivyo bila hasira na wala manungu’uniko, aidha Baba Mtakatifu akirudia barua ya Mtakatifu Paulo anasema ni dua, na sala, na maombezi na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka na ili kuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahimilivu.

Paulo anasisitizia mazingira ya mtu aliye mwamini

Katika kuendelea na ufafanuzi wake, Baba Mtakatifu Francisko amesema, Paulo anachosisitiza kidogo katika mazingira ya mtu mwamini ni sala. Ni sala ya maombi ili wote wasali kwa ajili ya wote, ili wote waweze kuwa na maisha mema ya utulivu na hadhi huku wakimtegemea Mungu. Kusali kwa namna hiyo ili kila kitu kiwezekane, lakini Baba Mtaakatifu amependa kubainisha jambo moja kuhusiana na kusali kwa ajili ya  watu wote hasa kwa ajili ya wafalme wanaoshika madaraka. Ni kwa maana ya kusali kwa ajili ya wanasiasa na watu ambao wanahusika kupeleka mbele taasisi za kisiasa, nchi na wilaya.

Kusali kwa ajili ya wanaofikiria tofauti

Hata hivyo kwa kufanya hivyo Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba kuna uthibitisho wa uwepo wa upendeleo hata kashfa. Na hii ni kutokana kuwa wakati mwingine wanasiasa hata mapadre na maaskofu wanasemwa vibaya na labda wengine anastahili, japokuwa sasa imekuwa ukawaida hata akitazama juu ya kashfa ya rosari au maneno machafu yasiyo na maana ambayo yamejitokeza. Licha ya hayo aliyeko madarakani, anasema, ana uwajibu wa kuongoza Taifa, lakini je ni vema kumwacha peke yake, bila kumwombea Mungu aweze kumbariki? Baba Mtakatifu amebainisha kuwa na uhakika kwamba watu awasali kwa ajili ya watawala tu, kwa maana labda ingekuwa sala ya utani. Na kumbe ndiyo maisha ya uhusiano na yule aliye madarakani.

Hii ni kuonesha kuwa Mtakatifu Paulo anaeleza wazi juu ya kuomba sala kwa ajili ya kila mmoja, ili waweza kupeleka mbele maisha kwa utulivu na amani ya watu wao. Kwa maana hiyo  amekumbuka nchi ya Italia ambayo hivi karibuni wameishi kipeo cha kiserikali na kuuliza swali, je ni nani amesali kwa ajili ya serikali? Je ni nani amesali kwa ajili ya Bunge? Ili viongozi waweze kukubaliana na kupeleka nchi yao mbele? “Utafikiri roho wa uzalendo haifiki katika sala hiyo”ndiyo katika “uchaguzi, chuki, mapigano, na kuishia hivyo” anatoa mfano Baba Mtakatifu na kuongeza kutaja maneno ya Mtakatifu Paulo asemaye: “Basi, nataka wanaume wasali kila mahali, huku wakiinua mikono yao juu  pasipo hasira wala majadiliano”. Ni lazima kufanya majadiliano na ndiyo kazi ya bunge, lazima kujadiliana, lakini siyo kumkashifu mwingine; badala yake lazima kusali kwa ajili ya mwingine na kwa ajili ya maoni tofauti ya mwingine, baba Mtakatifu amehimiza.

Watu wote wanaalikwa katika uongofu

Mbele ya yule anayefikiri kwamba siasa ni ile ya ukomunisti mwingi au ufisadi, Baba Mtakatifu Francisko emetazma Injili ya Siku ya Mtakatifu Luka, ambayo  inaonesha kwamba hakuna mjadala na siasa, bali ni msisitizo wa sala. Hata hivyo amesema kuna anayesisitiza kuwa siasa ni chafu. Lakini Mtakatifu Paulo VI, alikuwa anasema  kuwa, “siasa ni mtindo wa hali ya juu wa upendo”. Inawezekana kuwa mchafu kama ilivyo kila mmoja katika toba. Ni sisi tunaochafua jambo, lakini siyo jambo lenyewe kuwa chafu. Baba Mtakatifu anaamini kwamba, wote tunapaswa kuongoka na kusali kwa ajili ya wanasiasa wote, wa rangi zote! Ni kusali kwa ajili ya watawala.

Na ndiyo Mtakatifu Paulo anaomba ma zadi Baba Mtakatifu anasisitiza  kwamba, wakati anasikiliza Neno la Mungu amewaza jambo moja zuri la Injili, kuhusu Akida ambaye aliyekuwa anamwombea  mtumwa wake. Kwa maana hiyo ni wazi kwamba hata watawala wanapaswa kusali kwa ajili ya watu wake na ndiyo maana hiyo alisali kwa ajili ya mtumwa wake na kumwombea. Ndiyo ni mtumwa wake yeye anao wajibu wake, Baba Mtakatifu ansisitiza. Watawala ni wawajibikaji wa maisha ya nchi! Ni vizuri kabisa kufikiria kwamba iwapo watu wanasali kwa ajili ya watawala wao, na  watawala wao watakuwa na uwezo pia wa kusali kwa ajili ya watu wao kama alivyofanya Akida huyo kusali kwa ajili ya mtumwa wake.  

16 September 2019, 13:00
Soma yote >