Tafuta

Vatican News
Misa ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Roma Misa ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Roma  (ANSA)

Papa:utumishi ni zawadi inayopaswa kutunzwa na siyo mkataba wa kazi!

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko alhamisi tarehe 19 Septemba 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta,amesisitiza juu ya kutobinafsisha zawadi na kujiweka katika kitovu sisi wenyewe binafsi ambapo tunageuka kuwa kama wenye mkataba wa kazi ya umma.Kwa kufanya hivyo ni kupoteza moyo wa utumishi,uaskofu au ukuhani wowote ule.Ukosefu wa kutafakari zawadi ya Bwana husababisha kuzaliwa kwa njia za mikatisho.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akiwa amezungukwa na maaskofu wengi na mapadre wakati wa kuadhimisha Misa ya asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, kwenye mahubiri yake amekumbuka hasa wale wanaoadhimisha jubilei ya miaka 25 na Kardinali Edoardo Minchelli, Askofu Mkuu msaidizi wa Ancona mwenye umri wa miaka 80. Baba Mtakatifu kwa kutazama hawa amejikita kuelezea juu ya utumishi wa kikuhani kwamba ni zawadi ya Bwana ambaye “alituita na kusema nifuateni”, kwanza  kutoa huduma na siyo kuwa kama mtumishi wa umma au mkataba wa kazi.

Baba Mtakatifu Francisko amewaalika wote kuanzia na yeye mwenyewe katika kutafakari vema Somo la liturujia ya siku kutoka Barua ya Kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Timeteo,na ambayo imejikita juu ya neno la zawadi, na katika huduma kama zawadi ya kutafakari hasa kwa kufuata ushauri wa Mtakatifu Paulo aliokuwa akiutoa kwa kijana mtume ya kwamba, “usichezee zawadi uliyo nayo”. Baba Mtakatifu anasema: “Siyo mkataba wa kazi. Mimi ninapaswa kufanya nini?, ni kufanya kwa mjibu wa mpango gani?; mimi ninapaswa kupokea zawadi na kuitunza kama zawadi na tangia hapo ndipo kila kitu kinajitokeza hasa katika kutafakari zawadi”. Baba Mtakatifu aidha amesisitiza kwamba: “Tunapo sahahu hili, tunatumia zawadi yetu binafsi na kuigeuza kuwa kama kazi, ambapo tunapoteza moyo wa utoaji wa huduma, tunapoteza mtazamo wa Yesu anayetazama wote na ambaye alitueleza kwamba: ‘nifuate’!  Ni kupoteza zawadi ya bure”. baba Mtakafitu amefafanua.

Kufuatia na ukosefu wa kutafakari kwa kina juu ya zawadi katika utoaji wa huduma Baba Mtakatifu Francisko anatoa onyo kwamba, njia zote za mikato zinaanzia hapo na ambazo zinatambulika, kuanzia zilizo mbaya sana na zisizo elezeka, hadi zile za kila siku, ambazo zinajikita kutazama huduma binafsi na siyo kuitazama kama zawadi ya bure na upendo  kwa Yule aliyetoa zawadi ni zawadi kwa ajili ya huduma. Baba Mtakatifu Francisko akimtaja Mtume Paulo anasema, zawadi inayotolewa  katika neno la kinabii kwa njia ya kuwekewa mikono kwa upande wa makuhani, pia hiyo ni kwa ajili ya maaskofu na mapadre wote. Kwa  maana hiyo kuna umuhimu wa kutafakari utumishi kama zawadi na siyo kama kazi. Ni lazima kufanya kile kiwezekanacho, anaweka bayana Baba Mtakatifu kwamba ni kwa mapenzi mema na kutimia akili, hata kwa kutumia uelevu, lakini daima iwe ni kutunza zawadi hiyo.

Mfarisayo alisahau zawadi za ukarimu na makaribisho. Kusahau chanzo cha zawadi ni jambo la kibinadamu, huku akitoa mfano Baba Mtakatifu amemtumia  mfalisayo katika Injili ya Luka ambaye alimkaribisha Yesu katika nyumba yake , huku akidharau  sheria nyingi za  ukarimu, yaani kudharau zawadi anasisitiza Baba Mtakatifu. Yesu anamkumbusha akimwonesha mwanamke ambaye alitoa yote ambayo mwenyeji alikuwa amesahau: kwanza maji kwa ajili ya kunawa miguu, busu kwa ajili ya ukarimu na mafuta ya kupaka kichwa.  Ndiyo Baba Mtakatifu anongeza kusema,  alikuwa ni mtu mwema na mfalisayo mwema, lakini alikuwa amesahau zawadi ya ukarimu, zawadi ya namna ya kuishi na ambayo ndiyo zawadi. Daima kuna kusahau zawadi na hasa inapotokeza kwamba nyuma yake kuna jambo fulani la kutafuta, hasa  ninapotaka kufanya kile, na kile... Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha. aidha amesema kwamba lazima mapadre na kwa  wote kufanya mambo na mazoezi, ikiwa la kwanza ni kutangaza Injili, lakini inahitaji kuhifadhi, hasa kuhifadhi chanzo, ambacho ni kisima, mahali ambamo utume  huo unabubujika na ndiyo zawadi ya kwanza tulyoipokea bure kutoka kwa Bwana.

Bwana atusaidie tusigeuke kuwa makandarasi: Baba Mtakatifu Francisko akihitimisha tafakari  ameomba kwa Bwana ili atusaidie kutunza  na kuona huduma ya utumishi wetu kwanza, kama ni zawadi na baadaye kutoa huduma na ili kutoiharibu  na kugeuka kama  watumishi wa kikandarasi ambao wanahangaika sana na mambo mengi ya kufanya na ambayo yanaweza kufanya kwenda mbali na tafakari ya zawadi ya Bwana, ambaye alitupatia zawadi ya utumishi. Ameomba neema hiyo kwa ajili ya wote, lakini zaidi kwa wale ambao wameadhimisha miaka 25 tangu kupata daraja la kikuhani.

19 September 2019, 13:16
Soma yote >