Tafuta

Vatican News
Watuwanaishi kwa kulalamika, wanaishi kwa manung’uniko na masengenyo na wakati huo huo wanaishi bila kutosheka Watuwanaishi kwa kulalamika, wanaishi kwa manung’uniko na masengenyo na wakati huo huo wanaishi bila kutosheka 

Papa Francisko:watu wengi hawana uvumilivu,wala subira ya fufuko wa Yesu!

Wakati wa misa ya asubuhi tarehe 9 Aprili 2019, katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican,Baba Mtakatifu Francisko ametafakari kuhusu somo la kwanza kutoka kitabu cha Hesabu (Hes 21,4-9),na kugusia juu ya roho ya uchovu ambao unaondoa matumaini.Kwa maana hiyo wapo watu wengi wasio kuwa na uvumilivu na subira ya ufufuko.

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake tarehe 9 Aprili 2019, kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican amejikita kutafakari juu ya uchovu uliotolewa katika Somo la siku kutoka Kitabu cha Hesabu ( Hes 21,4-9). Katika somo linaelezea ni kwa jinsi gani  watu wa Mungu walikuwa hawana uvumilivu tena wa safari. Shauku na matumani yao ya kukimbia kutoka utumwani nchini Misri ilikuwa imepotea, walikuwa wameanza kugeuka hata sura wakiwa forodhani na baadaye kufika katika jangwa … anasema Baba Mtakatifu Francisko na kuongeza, lakini, wakati huo huo walianza kulalamika na kumshutumu Musa. Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, wakati mwingine hata wakristo wanapendelea kushindwa na kuacha nafasi za kulalamika na kutotosheka, na kumbe kambi hii kamili, mpanzi ni shetani.

Roho ya uchovu inaondoa matumaini

Roho ya uchovu inatuondolea matumaini, anasititiza Baba Mtakatifu na uchovu unachagua daima na kutufanya tuone kila kitu ni kibaya tukiwa tunaishi na kusahau  mambo mema tuliyopokea. Tunapokuwa na upweke, hatuna uvumulivu wa safari na tunafuta kimbilio au mihungu au masengenyo au mambo mengine mengi…. Huo ndio mtindo wetu anasema Baba Mtakatifu. Na roho hiyo ya uchovu katika ukristo inatupelekea hata kuwa na  mtindo mwingine wa kutotosheka. Yaani kuwa na roho isiyo tosheka. Kila kitu hatukipendi , na kila kitu kinakwenda vibaya, na wakati huo huo hata Yesu mwenyewe alitufundisha hili anaposema, roho isiyo tosheka ambayo imo ndani mwetu kama watoto wanaocheza.

Mpanzi ni shetani

Baadhi ya wakristo anaongeza, Baba Mtakatifu wanakubali kushindwa bila kujua kwamba kambi kamilifu, mpanzi anayepanda ni shetani. Mara nyingi wanaogopa kutulizwa, wanaogopa kuwa na matumaini, wanaogopa ukarimu wa Bwana na kuongozwa na maisha ya kipuuzi. Haya ndiyo maisha ya wakristo wengi anathibitisha Baba Mtakatifu. Watu hawa  wanaishi kwa kulalamika, wanaishi kwa manung’uniko na masengenyo na wakati huo huo  wanaishi bila kutosheka. Watu hao hawakuweza kuwa na uvumilivu katika safari, lakini mara nyingi hata sisi wakristo hatuna uvumilivu wa safari. Kwa upande wetu upendeleo ni ule wa kushikilia kushindwa, yaani kujibagua. Kujabgua huko ni nyoka. Yaani kuwa kama nyoka wa kizamani, ambaye aliomekana mbinguni. Ni ishara ambayo inaonekana ikimlaghai Eva na ndiyo mtindo wa kuona nyo ka ambaye yumo ndani anauma na daima anajibagua.

Hofu ya matumaini

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari anasema kadiri unavypitia maisha ya kulalamika mara nyingi hujitokeza kwa wengi ambao wanashindwa na hawana uvumilivu na subira na matumaini, hawa uvumilivu wa kusubiri ufufuko wa Yesu. Baba Mtakatifu amehitimisha mahubiri yake kwa kuhimiza wakumbuke juu ya maneno  haya kwamba:watu hawakuwa na uvulivu wa safari.Wakristo hawana uvumilivu wa safari.Wakristohawana uvumilivu wa matumaini.Wakrsto hawana uvumilivu wa uponyoaji.Wakristo hawana uvumilivu wa faraja.Sisi tumeshikilia kutotosheka, uchovu na kushindwa,hivyo Bwana atuokoe na ugonjwa huo.

09 April 2019, 12:41
Soma yote >