Tafuta

Misa ya Baba Mtakatifu Francisko Misa ya Baba Mtakatifu Francisko   (Vatican Media)

Papa:Majilio yasiwe ya kiulimwengu,ni fursa ya kutakasa imani!

Katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican,Baba Mtakaifu Francisko ameadhimisha Misa Takatifu tarehe 3 Desemba, ambapo amezungumzia juu ya kipindi cha majilio kwamba ni fursa ya kutambua kwa dhati Sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu huko Yerusalem na ili kukuza uhusiano binafsi na Mwana wa Mungu

Sr Angela Rwezaula – Vatican

Kuna aina tatu za ukuu wa kipindi cha Majilio, ambapo ni wakati uliopita, uliopo na ujao. Ndiyo mwanzo wa ufafanuzi wa Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mahubiri yake, katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, siku ya Jumatatu tarehe 3 Desemba 2018, akikumbusha waamini  juu ya kuanza kipindi cha majilio na ambacho anasema ni fursa ya dhati ya kujitakasa roho na kufanya imani  ikue kwa njia ya utakaso. Baba takatifu amezungumza hayo wakati wa  kutafakari Neno la Mungu akiongozwa na Injili ya siku kutoka Mtakatifu Marko 8,5-11, mahali ambapo Yesu alipoingia Kapernaumu, alikumbana na akida mmoja akamsihi amponye mtumishi wake aliyekuwa amelala nyumbani, na mgonjwa sana wa kupooza. Baba Mtakatifu katika kufafanua hili amesisitiza kuwa: “Hata leo hii, inawezekana kuwa na hali hiyo ya kulala na kubaki na ukawaida wa imani  kwa kusahau uhai wake,  hasa katika mazoea ya kupoteza nguvu ya imani ambayo ndiyo uhai kamili wa  imani inayotakiwa kupyaishwa daima!

Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana isiwe ya malimwengu

Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua juu ya ukuu wa majilio amesema kwanza, ni wakati uliopita ili kutakasa kumbukumbu. Ametoa mfano, " kumbukeni Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana siyo  mti uliozaliwa na ambao kwa hakika ni ishara nzuri, lakini ni kukumbuka kuwa, alizaliwa Yesu Kristo”. Alizaliwa Bwana, alizaliwa Mkombozi ambaye alikuja kutukomboa". Na tunatambua ya kuwa mara nyingi katika sikukuu, zipo hatari na hazitakosekana daima kwetu, hasa katika vishawishi vya ulimwengu wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Vishawishi hivyo ni pale ambapo wanapoacha kutafakari uzuri wa familia, wa kumweka Yesu awe kitovu na badala yake wakafanya sikukuu ya ulimwengu inayojikita katika kununua na kutoa zawadi na mambo mengine,  wakati huo huo  Bwana anabaki amesahauliwa, lakini Bwana alizaliwa katika maisha, hata huko Betlehemu na zaidi majilio ni kipindi cha kujitakasa na kufanya kumbu kumbu ya wakati uliopita na ukuu wake.

Kutakasa matumaini

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ufafanuzi wake katika ukuu wa matumaini amesema, kipindi cha Majilio zaidi kinasaidia kutakasa matumaini kwa kujiandaa kukutana hatimaye na Bwana. Hiyo ni kutokana na kwamba Bwana aliyekuja wakati ule, atarudi tena na kutuuliza kwa  jinsi gani tumeweza kukaa katika maisha haya? Huo utakuwa ni mkutano binafsi. Sisi tutakutana na Bwana binafsi, kama tunavyokutana naye katika Ekaristi, lakini hatutaweza kukutana naye kama alivyozaliwa miaka 2000 iliyopita, ndiyo tunayo kumbukumbu ile, lakini ni pale ambapo Yeye binafsi atakapo kuja tena na kukutana nasi. Yeye anasafisha matumaini.  

Bwana anabisha hodi kila siku katika mioyo yetu na kusafisha njia  na kukesha

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini wote kukuza ukuu wa imani kila siku, japokuwa wanakumbana na mahangaiko mengi ya maisha na kupoteza ulinzi kina wa moyo ambao ni nyumba binafsi.  Mungu wetu kwa hakika ni Mungu wa mshangao, kwa maana hiyo  wakristo wanapaswa kugundua kila siku ishara za Baba wa Mbingu ambaye anazungumza nasi leo hii. Ukuu  wa tatu ambao Baba Mtakatifu Francisko, ameufafanua ili kujiandaa vema kila siku katika kipindi hiki cha majilio ni kusafisha njia au kukesha. Kukesha na sala ndiyo maneno mawili kwa ajili ya majilio, kwa sababu Bwana alikuja katika historia ya Betlehemu; atakuja mwisho wa dunia, hata katika mwisho wa kila mmoja, zaidi lakini Bwana anakuja kila siku, kila wakati katika mioyo yetu, kwa hisia za Roho Mtakatifu.

03 December 2018, 11:50
Soma yote >