Mungu anainama, Mungu anaingia katika historia na kufanya uwe mtindo wa maisha asili, kwa njia ya mshangao Mungu anainama, Mungu anaingia katika historia na kufanya uwe mtindo wa maisha asili, kwa njia ya mshangao  (Vatican Media)

Papa Francisko:Mungu anajishusha na kubadili historia ya maisha!

Wakati wa Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican,tarehe 20 Desemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko amejikita kuelezea juu ya fumbo la hupashanaji wa habari njema ya Malaika kwa Bikira Maria. Amebainisha kuwa ni kipindi ambacho kinabadili kabisa historia ya binadamu, kwa maana ni Mungu anajishusha!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hii ni sehemu katika Injili ya Luka (Lk 1,26-38) iliyo ngumu kuweza kuihubiri, mahali ambapo Mungu wa mashangao, anamfanya bubu binadamu. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza hayo wakati wa Misa yake ya Asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 20 Desemba 2018. Amethibitisha hayo akifafanua zaidi juu ya kupashwa habari njema kwa Mama Bikira Maria.

Mungu wa mshangao na anatushangaza kwa mara nyingine tena

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake, anasema, Injili ya siku iliyosikika, inasimulia kipindi muhimu cha kihistoria na cha mapinduzi zaidi. Ni hali ya mabadiliko ya kila kitu, kwa maana historia inageuzwa. Ni vigumu kuhubiri sehemu hii ya Injili anathibitisha Baba Mtakatifu na kuongeza kusema kuwa: Wakati wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana au katika Sikukuu ya kupaswaha habari, tunaposali sala ya Imani, kuthibitisha hilo ni kwa njia ya kupiga magoti.

Ni kipindi cha mabadiliko ya kila kitu kutoka ndani ya mzizi. Kiliturujia, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, leo hii ni siku ya mzizi. Utenzi wa wa siku unathibitisha kuwa katika mzizi au ukoo wa Yese kulichupuka kichipukizi. Mungu anainama, Mungu anaingia katika historia na kufanya uwe mtindo wa maisha asili, kwa njia ya mshangao. Mungu wa mchangao, anatushangaza kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu anathibitisha.

Baba Mtakatifu amerudia kusoma jibu la Malaika alilompatia Maria katika Injili

Ili kuwafanya waamini waliounganika kusali naye waweze kutafakari kwa kina juu ya somo la hupashanaji habari, Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mahubiri yake, amerudia kwa upya kusoma Injili ya Siku hasa sehemu ya jibu la Malaika  Gabrieli kwa Maria kwamba:

 “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Na hapo Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Na kisha malaika akaondoka akaenda zake”.

20 December 2018, 11:20
Soma yote >