Ninajenga maisha yangu juu ya mwamba wa Mungu au juu ya mchanga wa ulimwengu na ubatili? Ninajenga maisha yangu juu ya mwamba wa Mungu au juu ya mchanga wa ulimwengu na ubatili?   (Vatican Media)

Papa:Bwana ni mwamba wa kujenga maisha!

Kusema na kutenda. Mchanga na mwamba. Juu na chini, ndiyo makundi matatu ya maneno aliyofafanua Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 6 Desemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake kwenye misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta, amejikita kueleza maneno mawili mawili yanaykwenda kinyume kama vile: kusema na kutenda, mchanga na mwamba, juu na chini ili kulifafanua vema Neno la Mungu kutoka katika Injili ya Mtakatifu Matayo na somo la kwanza kutoka kitabu cha Nabii Isaya lililosomwa tarehe 6 Desemba 2018.

Kusema na kutenda

Akianza kufafanua kundi la meneno mawili “kusema na kutenda”, ni maneno mawili yanayo tofautiana katika safari na ambayo anasema kuwa  yamewekwa katika maisha ya kikristo kwani, kusema ni namna ya kuamini, japokuwa ni kijujuu, kama vile katikati ya safari. Baba Mtakatifu anasema: mimi ninasema ni mkristo, lakini sifanyi yale ya ukristo. Ni kama kupamba ukristo mafuta katika mgongo wa chupa. Na kwa maana hiyo ni maneno bila matendo. Mapandekezo ya Yesu  daima ni ya dhati.  Iwapo mtu anakaribia na kumwomba ushauri daima anatenda kwa dhati. Na Matendo ya huruma daima ni ya kweli!

Mchanga na mwamba

Hata kundi la pili la maneno ya mchanga na mwamba, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa ni maneno mawili yanayokwenda kinyume. Nchanga siyo mgumu na matokeo yake  ni kama yale yale ya kujipaka ukristo katika kujenga maisha bila msingi. Mwamba kinyume chake ni Bwana. Yeye ndeye nguvu. Japokuwa Baba Mtakatifu anongeza, mara nyingi anayemtumaini, wakati mwingine hatoke na hata kuwa na mafanikio, amejificha, lakini mtu huyo ni mwenye msimamo na hayumbi. Mtu huyo hana tabia ya ubatili, kiburi, na kupenda madaraka katika maisha (… ) Kwa maana Bwana ni mwamba. Uthabiti wa maisha ya kikristo unatufanya twenda mbele na kujenga  ule mwamba ambao ni Mungu pia  ni Yesu. Katika msimamo wa Mungu na siyo kijuu juu tu au ubatili, ukiburi na upendeleo, badala yake ni ukweli, amesisitiza Baba Mtakatifu.

Juu na chini

Kundi la tatu la  na la mwisho ambalo Baba Mtakatifu amelifafanua ni maneno  ya juu na chini na kwamba hata yenyewe yana mwelekeo tofautia ambao unakenda kunyem na hatua za kubiri na ubatili kwa wale walio wanyenyekevu. Katika somo la kwanza la siku Kutoka Isaya, Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza kuwa, Bwana aliwangusha chini wale waliokuwa wanaishi juu na kuwaangusha miji yote iliyokwa juu hadi chini ya ardhi. Miguu iliaanza kukanyaga. Waliokuwa wanateseka na kuelewa, ni hatua za maskini. Somo la  Nabii Isaya linakwenda sambamba na utenzi wa Mama Maria magnificat, yaani Bwana anawashusha waliojii na kuwatazama wanyenyekevu ambao wanaishi ukweli wa kila siku na kuwaangusha wenye kiburi ambao wanajenga maisha yao  juu ya ubatili na ukiburi, na hawadumu.

Maswali ya kujiuliza katika kipindi cha majilio

Katika kipindi cha majilio ni kujiuliza maswali ambayo yatatusaidia: je mimi ni mkristo wa kusema au kutenda? Ninajenga maisha yangu juu ya mwamba wa Mungu au juu ya mchanga wa ulimwengu na ubatili? Je mimi ni mnyenyekevu, ninatafuta daima kwenda chini bila kiburi na ili kuhudumia Bwana?

 

 

06 December 2018, 13:20
Soma yote >