Misa Takatifu ya Baba Mtakatifu katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta:Ametazama kwa karibu sura ya Mtakatifu Yosefu anayelinda na kukuza Yesu kwa ukimya Misa Takatifu ya Baba Mtakatifu katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta:Ametazama kwa karibu sura ya Mtakatifu Yosefu anayelinda na kukuza Yesu kwa ukimya  (Vatican Media)

Papa anasema Yosefu ni mtu wa ndoto na anasindikiza kwa ukimya!

Wakati wa Misa takatifu ya Baba Mtakatifu Francisko, katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 18 Desemba 2018 amezungumzia juu ya sura ya Mtakatifu Yosefu. Kadhalika wakati wa maombi, Baba Mtakatifu amewaombea watoto walemavu wa nchi ya Slovakia ambao wametengeneza badhi ya mapambo ya Sikukuu ya Noeli

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Yosefu ni mwanaume anayetambua kusindikiza kwa ukimya, ni mwanume wa ndoto. Baba Mtakatifu Francisko ametumia mifano hii miwili kwa kutazama tabia ya Mtakatifu Yosefu wakati wa mahubiri ya Misa Takatifu katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 18 Desemba 2018. Baba Mtakatifu anasema, katika kipindi hiki cha Majilio pia anawakumbuka kwa sala watoto wote walemavu wa nchi ya Slovakia ambao wametengeneza mapambo yaliyowekwa katika mti wa Sikukuu ya Noeli ambao umepambwa mbele ya Altare.

Hekima ya wazazi wenye akili

Katika maandiko matakatifu, tunatambua Yosefu alivyokuwa mwanaume mwenye haki, alikuwa anatimiza sheria, anafanyakazi, mnyenyekevu na alimpenda sana Maria. Lakini katika kipindi cha kwanza hasa mbele ya kutoelewa nini kinatukia juu ya Maria, Yeye alipendelea kujiweka pembeni, japokuwa baadaye Mungu analimwonesha utume wake. Na kwa maana hiyo Yosefu anakumbatia jukumu lake, nafasi yake na kusindikiza makuzi ya Mwana wa Mungu kwa ukimya, bila kuhukumu, bila kusema, na hata bila mazungumza hovyo. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kufafanua sura ya Mtakatifu Yosefu anasema, yeye anasaidia kukua na kuendelea na kwa maana hiyo alitafuta nafasi ili mtoto huyo apate kuzaliwa; alimtunza, alimsaidia akue; alimfundisha kazi na mambo mengine mengi… Yote hayo aliyatenda kwa kimya. Kamwe hakuweza kummiliki kama mwanae; alimwacha akue kwa ukimya.

Baba Mtakatifu anaongeza kusema Yosefu, alimwacha  mtoto akue ndiyo neno ambalo litusaidie sana hata sisi kwa namna ya pekee kwa sababu ya uasili wetu daima unapendelea kuweka kuweka pua  zetu kwa kila kitu, hasa katika maisha ya wengine. Ni kwa sababu gani anafanya hivyo na asifanye kama wengine…? Kwa sababu wengine wengi wana maneno sana, wana mambo mengi ya kuzungumza… wakati Mtakatifu Yosefu anaacha mtoto anakua, anamlinda, anamsaidia, lakini yote hayo anayatenda kwa ukimya. Kawaida ya mtu wenye hekima ambaye Baba Mtakatifu Francisko anatambua kwa wazazi walio wengi ni ule uwezo wa kusubiri, bila ya kuhamaki mbele ya makosa. Ni jambo msingi hasa wa kutambua kusubiri kabla ya kusema neno lenye uwezo wa kujenga na kukua. Kusubiri kwa kimya kama anavyo fanya Mungu na watoto wake, ambapo wanamfanya awe na uvumilivu. Ameshauri Baba Mtakatifu.

Mwanaume wa ndoto

Aidha Katika mahubiri Baba Mtakatifu anaweka bayana kwanini Mtakatifu Yosefu alikuwa mwanaume wa dhati, pia mwenye kuwa na moyo ulio wazi, mwanaume mwenye ndoto na siyo anayeota ndoto. Ndoto ni sehemu mwafaka wa kutafuta ukweli kwa sababu pale hatuwezi kujilida na ukweli. Ndoto zinakuja tu na Mungu pia anazungumza hata katika ndoto. Baba Mtakatidfu amebainisha kuwa si mara nyingi kwa sababu kawaida ni dhamiri zetu ambapo ndoto zinakuja tu, lakini mara nyingi Mungu alichagua kuzungumza kwa njia ya ndoto. Alifanya mara nyingi katika Biblia, kwani inaonesha  hizo ndoto, amethibitisha Baba Mtakatifu. Yosefu alikuwa ni mwanaume wa ndoto, japokuwa, hakuwa siyo mwota ndoto, hakuwa ni wa kufikirika tu.  Mwota ndoto ni jambo jingine:ni yule ambaye anaamini… na anakwenda, yupo hewana na wala haweki miguu chini ya ardhi.  Lakini Yosefu alikuwa ameweka miguu chini ya ardhi, pia alikuwa wazi.

Usipoteza radha ya kuota

Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko anaomba kutopoteza uwezo wa kuota ndoto, uwezo wa kujifungulia ya kesho kwa imani, licha ya matatizo ambayo yanaweza kutokea. “Usipoteza uwezo wa kuota wakati ujao, kila mmoja wetu kuota ndoto juu ya familia, juu ya watoto na wazazi wetu. Kutazama jinsi gani mimi hasa ninataka maisha yangu yawe. Na hata kwa mahukani, baba Mtakatifu amesema, waote ndoto  juu ya waamini wao ya kwamba  wanataka wawafanyie nini. Kuota kama vijana wanavyoota, na ambao wamejazwa na ndoto nyingi sana na pale wanaweza kupata njia. Hakuna kupoteza uwezo wa kuota ndoto, kwa sababu, kuota ni kufungulia mlango wakati ujao. Na hivyo ni kuzaa matunda ya wakati ujao. Baba Mtakatifu amethibitisha!

 

18 December 2018, 13:11
Soma yote >