Tafuta

Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa:Yesu anatualika katika karamu ya Ufalme,jihadhali na hapana

Ufalme wa Mungu mara nyingi unalinganishwa kama karamu. Yesu anatualika kufanya sikukuu na yeye, lakini Papa anauliz: je ni mara tunatafuta sababu za kukataa mwaliko huo? Lakini Yesu ni mwema na mwenye haki. Ndiyo sehemu ya tafakari ya tarehe 6 Novemba 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Somo la Injili ya siku ni kutoka katika sura ya kumi na nne ya Luka ambayo inajikita kutazama juu ya chakula, yaani karamu ambayo mkuu wa wafalisayo aliandaa na kumwalika  hata  Yesu pia. Injili ya jana na leo inataka kuonesha  ni jinsi gani walikuwa wanamtafuta Yesu kwa maana, alikuwa amemponya mgonjwa, Yeye pia alikuwa anatazama jinsi gani wengi walikuwa wakitafuta kukaa nafasi za kwanza na alikuwa amewashauri wafarisayo watoe mwaliko kwa watu walio wa mwisho ambao hawawezi kurudisha lolote. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya siku ya Papa Francisko, tarehe 6 Novemba 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican

Kukataa mara mbili

Akiendelea na mahubiri anasema: “Kwa ghafla katika Karamu, ndipo inaanza sehemu ya Injili ya siku ya Luka kwamba,  mmoja wa walioalikwa akasema,“ heri yule atakayeketi na kula katika ufalme wa Mungu”. Katika Somo la Injili kuna aina mbili za kukataa Papa anaasema na kuoengeza kufafanua kuwa: “Yesu anasimulia historia ya mtu aliyeandaa chakula na kuwaalika watuwengi”. Watumishi wake wakasema,“njoni kwa maana meza iko tayari! Lakini wote walianza kutoa sababu ili wasiweze kwenda.

Baba Mtakatifu anasema: "Majibu yalikuwa kama vile: uupo ambaye amenunua shamba, yupo aliyenunua ng’ombe watano na mwingine  amepata posa punde. Wote hao, walikuwa ni kutafuta sababu ya kutaa. Papa anasema: Kusema samahani ni neno la kistaarabu, ili usisema hapana moja kwa moja, lakini wanakataa kwa namna hiyo. Na ndiyo maana  Bwana anawatuma watumishi wasimame barabarani kuwaita masikini, wagonjwa, viwete,  vipofu na wafika wote katika sikukuu.

Somo la Injili

Papa anathibitisha, linahitimishwa  neno la kukataa mara ya pili, lakini kwa mara hii ni kutoka kinywani mwake Yesu (…) “ Anaye mkataa Yesu, Yesu anasubiri, anatoa fursa ya pili, labda ya tatu, ya nne, ya tano… lakini mwishowe anakataa Yeye”.  Lakini kutaa huko, lazima kutufanye tufikirie, kwani mara nyingi Yesu anatuita; anatutafu ili kufanya sikukuu na Yeye na kuwa karibu naye na kubadili maisha.  Fikiria kwamba anatafuta marafiki zake wa moyo na wao wanamkataa!

Baadaye anawatafuta wagonjwa… na wanakwenda; labda kuna hata anayekataa.  Ni mara ngpi tunahisi wito wa Yesu ili kwenda kwake, ili kufanya matendo ya upendo, kusali na wakatu huo tunakataa na tunasema, samahani Bwana mimi nina mambo mengi ya kufanya na sina muda. Au ndiyo lakini labda kesho, leo siwezi …. Pamoja na hayo Yesu anabaki pale,Baba Mtakatifu amethibitisha.

Ni mara ngapi tunatunga samahani kwa Yesu

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake, ameuliza swali: Je ni mara ngapi unasema samahani, hasa unapoitwa na Yesu kukutana naye, kuzungumza naye na kufanya mzungumzo mema. Ndiyo mara ngapi, sisi tunakataa mwaliko wa Yesu. Kila mmoja afikirie katika maisha binafsi, mara ngapi umehisi, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kufanya matendo ya upendo na kukutana na Yesu katika tendo lile la upendo, kwenda kusali, kubadili maisha na mambo mengine ambayo hayaendi? Lakini daima kumekuwapo na sababu ya kukataa.

Yesu ni mwana lakini ni mwenye haki

Hata hivyo Papa Francisko anasema, mwisho wa hayo yote ataingia katika ufalme wa Mungu yule ambaye hakumkataa Yesu au yule ambaye hakukataliwa naye. Amesema hayo, kutokana na yule anayetafsiri kuwa, Yesu kwakuwa ni mwema na mwishowe atasamehe yote, lakini Papa anathibitisha ni kinyume, kwa maana ndiyo ni mwema na mwenye huruma, lakini pia ni mwenye haki. Iwapo wewe unafunga mlango wa moyo wako, Yeye hawezi kuufungua kwa sababu anaheshimu mioyo yetu. Kukutaa Yesu ni kufunga mlango kutoka ndani mwako na Yeye hawezi kuingia. Hakuna yoyote anayefikiria jambo hili wakati anakataa Yesu ya kwamba ninafungia mlango Yesu kutoka ndani.

Na katika kifo chake, yeye alilipa karamu

Kwa kuhitimisha tafakari yake, Baba Mtakatifu Francisko ameonesha sehemu nyingine ya kuwa makini hasa ni nani anayelipa katika karamu? Ni Yesu! Mtume Paulo, katika Barua yake ya kwanza ya siku anaonesha jumla ya gharama, akizungumza juu ya Yesu, “alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wawanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba”. Kwa maisha yake, Papa Francisko anasema alilipa sikukuu. “ na mimi ninasema: Siwezi (…) na hivyo:  "Bwana atupatie neema ya kutambua fumbo hili la ugumu wa moyo, kichwa kigumu, kukutaa na neema ya kulia”.

06 November 2018, 15:05
Soma yote >