Cerca

Vatican News
Katika mahubiri ya Papa Francisko tarehe 9 Novemba anatoa onyo kuwa Kanisa lisigeuke kuwa soko Katika mahubiri ya Papa Francisko tarehe 9 Novemba anatoa onyo kuwa Kanisa lisigeuke kuwa soko  (Vatican Media)

Papa:msiweke orodha ya bei katika sakaramenti!

Katika Mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, amejikita kufafanua tukio la kiinjili linalohusu kulisafisha hekalu. Amewaalika waamini kutafakari juu ya tabia, mwenendo na heshima leo hii tunayoitoa katika Makanisa yetu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Makanisa yawe ni nyumba ya Mungu na siyo masoko au kumbi za kijamii zinazotawaliwa na mambo ya kidunia. Ndiyo tafakari kuu ya Baba Mtakatifu Francisko, iliyojionesha wakati wa mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 8 Novemba 2018. Akianzia na sehemu ya Injili ya Siku kwa mujibu wa Yohane, (2,13-22), Papa anaeleza sababu zilizomfanya Yesu atumie nguvu kwenye soko ndani ya Hekalu. Na kwa maana hiyo anathibitisha kuwa “Mwana wa Mungu alisukumwa na upendo wote wa dhati kwa ajili ya nyumba ya Bwana, kugezwa kuwa soko”.

Miungu inatumikisha

Alipoingia ndani ya hekalu watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi, Yesu alitambua kuwa mahali ambapo watu walikuwa wengi, kulikuwa na miungu, na watu wako tayari kuitumikia “fedha”badala ya “Mungu”. Nyuma ya fedha kuna miungu, Baba Mtakatifu anabainisha na kuongeza kusema, miungu daima ni dhahabu. Miungu inawatumikisha”.Baba Mtakatifu anasema: Hiyo inavutia na kutufanya tufikiri jinsi gani sisi tunavutiwa mahekalu yetu, makanisa yetu; iwapo kweli ni nyumba ya Mungu, nyumba ya sala, nyumba ya mkutano na Bwana; iwapo padre anakuza hilo. Au iwapo tunafanana na wale watu wa masoko!

Akiendelea na ufafanuzi wake anatoa mfano na kubainisha kwamba, "ninatmbua… mara nyingi niliona… siyo hapa Roma, lakini sehemu nyingine, niliona orodha ya bei kwa vitu vya kununua. Lakini ni jinsi gani ya kununua Sakramenti? “Hapana, hii ni sadaka”. Lakini watu wanapotaka kutoa sadaka, wataiweka katika masunduku ya sadaka na tena inayofichika bila mtu mwingine kujua ni kitu gani ameweka.  Hiyo ni hatari iliyopo Baba Mtakatifu anasema, japokuwa wanatoa sababu, kwamba, “ tunapaswa kutunza Kanisa.  Ndiyo ni kweli, waamini watunze lakini, katika masanduku ya sadaka yasiwekewe orodha ya bei.

Kanisa lisigeuke kuwa soko

Kutokana na suala hili, Papa ametoa onyo juu ya kishawishi cha dunia hii. “Tufikirie baadhi ya maadhimisho ya Sakramenti, kama vile katika maadhimisho mbalimbali, mahali ambapo ukiienda na kuona; huwezi kujua kama sehemu ya liturujia ni nyumba ya Mungu au ni ukumbi wa kijamii. Kuna baadhi ya maadhimisho yanaelekea katika dunia. Ndiyo ni maadhimisho na yanapaswa yawe mazuri, lakini yasigeuke kuwa ya kidunia, kwa sababu malimwengu yanategemea na miungu fedha. Na hiyo ni moja ya ibada ya sanamu pia, Baba Mtakatifu amethibitisha. Hii inatufanya tufikiri pia  na sisi ni  jinsi gani tunaweka bidii yetu kwa ajili ya  makanisa yetu, heshima tuliyo nayo wakati tunapoingia ndani.

Hekalu la Moyo

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari yake, anagusia Somo la Kwanza la siku kutoka Mtakafu Paulo kwa Wakorinto, akibainisha  juu ya moyo mmoja unaowakilishwa na hekalu, yaani hekalu la Mungu. Papa anasema: “Pamoja na utambuzi  wa kuwa sisi ni wenye dhambi, kwa namna hiyo, kila mtu anapaswa kuhoji moyo wake ili kuona kama kama ni  “wa kidunia na wa kuabudu miungu”. Akihitimisha tafakari yake amesema: Mimi siulizi ni dhambi gani uliyo nayo, au dhambi zangu. Ninauliza iwapo ndani yako “kuna miungu na iwapo yupo Bwana fedha. Kwa sababu dhambi inapokuwapo, yupo Bwana Mungu wa huruma ambaye anasemahe, iwapo unakwenda kwake. Lakini kama kuna bwana mwingine, fedha, wewe ni mwenye kuabudu muungu, yaani mfisadi: si tu kuwa tayari mdhambi, bali wewe ni mfisadi pia.  Msingi wa rushwa ni ibada ya sanamu na  ni ile ya kuwa tayari umeuza roho kwa muungu fedha, kwa muungu nguvu. Yeye ni muabudu muungu”.

 

 

 

09 November 2018, 13:40
Soma yote >