Tafuta

Vatican News
Yesu ni mwema, badala ya kuwahukumu mafarisayo na waandishi wa sheria kwa ajili ya kunung'unika anawauliza swali Yesu ni mwema, badala ya kuwahukumu mafarisayo na waandishi wa sheria kwa ajili ya kunung'unika anawauliza swali  (Vatican Media)

Papa:kushuhudia kunavunja ukawaida ili kutambua huruma ya Mungu

Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Novemba 2018 imejikita katika Injili ya Siku,kutoka Mtakatifu (Lk 15,1-10) inayoanza na ushuhuda:Watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia Yesu wamsikilize.Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ushuhuda, manung’uniko na maswali. Ni maneno matatu ambayo Baba Mtakatifu Francisko amejikita nayo, asubuhi  tarehe 8 Novemba 2018 wakati wa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatian. Tafakari yake imejikita katika Injili ya Siku, kutoka Mtakatifu  (Lk 15,1-10) inayoanza na ushuhuda ikisema: “Watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia Yesu wamsikilize. Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao”.

Ushuhuda unafanya Kanisa likue

Baba Mtakatifu anasema, kwanza kuna ushuhuda wa Yesu, na mbao ulikuwa ni jambo jipya kwa wakati ule, kwa sababu ya kwenda kwa wenye dhambi, ilikuwa inakufanya uwe najisi, kama vile kumgusa mwenye ukoma. Kwa maana hiyo waandishi wa sheria walikuwa wakikaa mbali nao. Papa Francisko anabainisha kwamba, ushuhuda katika historia haujawahi kupokelewa vema na mara nyingi wengi wanalipa gharama ya maisha yao, hata wenye nguvu. Kushuhudia ni kuvunja ukawaida, ni kuvunja  namna ya kuwa ni kuvunja na  ili kuweza kuwa bora na  kubadilika. Kwa maana hiyo Kanisa linakwenda mbele kwa njia ya ushuhuda. Kile kinachovutia ni ushuhuda Baba Mtakatifu anasisitiza na siyo maneno ambayo yanasaidia, lakini ni ushuda ambao unavutia na kufanya Kanisa likue.

Kwa kufanya hivyo, Yesu anaonesha ushuhuda: Ni jambo jipya, lakini si jipya kwa sababu huruma ya Mungu ilikuwapo hata katika maandiko ya Agano la Kale.  Japokuwa wandishi wa sheria hawakujua kamwe ni nini maana ya: “ninataka huruma na siyo sadaka”. Wao walikuwa wakisoma tu, lakini hawakuwa wanajua ni nini maana ya huruma. Na Yesu kwa namna ya kutenda kwake, anatangaza huruma hiyo kwa ushuhuda, na kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu amebainisha kwamba ushuhuda daima unavunja mazoea na hata wakati mwingine kuwa hatarishi.

Badala ya kutoa suluhisho ya hali za migogoro, wananung’unika

Akiendelea na tafakari, Baba Mtakatifu anasema, ushuhuda wa Yesu unasababisha manung’uniko, kwani Mafarisayo, waandishi na walimu wa sheria walisema: “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao. Lakini hawakusema, “tazama mtu huyo tunafikiri ni mwema kwa sababu anafanya wangoke wadhambi”.  Na hiyo ni tabia ambayo inahusisha daima kutoa mazungumzo hasi, ili kuharibu ushuhuda”. Dhambi hiyo ya manung’uniko ni ya kila siku, iwe ndogo au kubwa kwa maana katika maisha binafsi tabia hiyo hupatikana kwa sababu ya kutopenda hicho au kile na badala ye  kuzungumza au kutafuta namna ya kupata suluhisho la hali ya migogoro, wao katika kujificha , ni kunung’unika daima kwa sauti ya chini, kwa maana hakuna hata ujasiri wa kuzungumza wazi. Hayo ndiyo yanajitokeza katika jamii ndogo na katika parokia Papa anasema. Ni manung’uniko mangapi yaliyoko katika Parokia? Ni mambo mangapi yapo, Papa anasema, akionesha wazi kwamba inapotokea ushuhuda wa mmoja kusema simpendi mtu, basi huanzia hapo manung’uniko…

Na katika jimbo? Mapambano kati ya majimbo

Baba Mtakatifu ameonesha wazi kuwa yapo mapambano ya ndani ya majimbo; ninyi mnajua hayo. Na hata katika siasa. Lakini hiyo ni mbaya.  Iwapo katika serikali haina uaminifu, hujaribu kuwachafua wapinzani wake kwa kunung'unika. Iwe ni kuchafua jina, kusengenya ni hutafuta daima. Baba Mtakatifu ameongeza: “na ninyi mnajua serikali za udikteta vizuri, kwa maana nini mliishi hali hiyo, serikali ya udikteta inafanya nini? Inachukua vyombo vya habari vya kuwasiliana na sheria mikononi mwake na tokea hapo, huanza kushusha wengine kwa kunung'unika na kuwachepesha wote kwamba ni hatari kwa serikali. Kunung'unika ni mkate wetu wa kila siku iwe kwa ngazi binafsi, familia, parokia, jimbo, ngazi ya jamii ... amethibitisha Baba Mtakatifu

Baba Mtakatifu anaonesha juu ya swali la Yesu

Ni kikwazo cha kutoangalia ukweli, yaani kutoruhusu watu kufikiri. Yesu anajua, lakini ni mwema na badala ya kuwahukumu kwa ajili ya kunung'unika, anauliza swali. “anatumia njia ile ile wanayoitumia wao”,ya kuuliza maswali. “Wao walifanya hivyo ili kumjaribu Yesu, kwa nia mbaya”, na ili “kumfanya aanguke”: kwa mfano, katika maswali kuhusu kodi ya kulipwa kwa ufalme au kutoa talaka kwa mke. Yesu anatumia njia ile ile, “lakini Papa Francisko anaonya kwamba wataona tofauti iliyopo”. Yesu anawaambia: “Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aenda akamtafute yule aliyepotea hata amwone?  Kama Injili inavyoonesha ya siku.  Na kama jambo la kawaida lingekuwa wao kutambua, lakini wao wanaishia kuhesabu: “ninao 99 kama amepotea mmoja na sasa jua limezama, na ni giza”; “Hebu tusahau huyo na katika bajeti itakwenda kaatika kupata na kupoteza, lakini tuweze kuwaokoa hawa”.  Papa anasisistiza: “Hii ndiyo mantiki ya Mfarisayo. Hii ni mantiki ya waandishi wa sheria. “Ni nani kati yenu?”.  “Na wao walichagua kinyume cha Yesu. Kwa sababu hiyo hawaendi kuzungumza na wenye dhambi, hawaendi kwa watoza ushuru, hawaendi kwa sababu wao ni bora hawawezi kujichafua watu hawa pia ni hatari”.

Mantiki ya Injili ni kinyume na mantiki ya ulimwengu 

Lakini Yesu ni mwenye akili kwa kuwauliza swali, kwa maana anaingia katika kesi yao, lakini anawaacha katika nafasi tofauti kulingana na haki. Swali ni hili je “Ni nani kati yenu?”. Lakini hakuna mtu anasema, “Ndio, ni kweli”, japokuwa  kila mmoja anasema: “Hapana, siyo mimi, siwezi kufanya”. Na kwa sababu hiyo hawawezi kusamehe,  kuwa na huruma, hata kupokea.

Mwisho Baba Mtakatifu amekumbuka maneno matatu ambayo yanafungamana katika tafakari yake: kwamba ni “ushuhuda,ambao unasababisha Kanisa likue, “manung’uniko ambayo ni “kama mlinzi wa mambo yangu ya ndani kwa sababu ushuhuda haunidhuru”, na “swali” la Yesu. Kadhalika anakumbusha neno jingine yaani,  furaha, sikukuu, ambayo watu hawa hawajui: “watu wote wanaofuata njia ya waandishi wa sheria hawajui furaha ya Injili”, anasisitiza Papa akihitimisha kwa kusema: Na Bwana atufanye  kuelewa mantiki hii ya Injili kinyume na mantiki ya ulimwengu.

 

08 November 2018, 14:15
Soma yote >