Tafuta

Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta   (Vatican Media)

Papa:ole wao wakristo wanafiki ambao wanaacha Yesu Kanisani!

Baba Mtakatifu katika mahubiri yake anasema, “Yesu alishikwa na uchungu wa kukataliwa na watu wake, wakati miji ya kipagani kama Tiro na Sidoni kama wangeona miujiza hiyo labda wangesadiki. Kwa maana hiyo kila mmoja, afikirie, je mimi ni Korazin, mimi ni Betsaida au Kafarnaum?

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Fransisko katika mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta, anawaalika kutafari juu ya unafiki kwa wenye haki ambao wanaishi ukristo kama vile mazoea ya kijamii na hawana Yesu katika maisha yao ya kila siku na kwa maana hiyo ni vigumu kuuondoa unafiki huo katika mioyo yao. Na kwa kufanya hivyo, “sisi ni wakristo lakini wanaoishi kama wapagani”.

 “Sisi tunaoishi katika jamii ya kikristo ipo hatari ya kuishi ukristo kama mazoea ya kijamii ambayo ni katika mtindo wa unafiki wa wenye haki, na ambao wanaogopa kupenda”. Kila inapomalizika madhimisho ya Ibada ya Misa takatifu, wanaacha Yesu katika Kanisa, hawarudi ya Yeye nyumbani na katika maisha yao ya kila siku. Ole wetu! Kwa maana tunamfukuza Yesu katika mioyo yetu. Sisi ni wakristo lakini tunaishi kama wapagani”.

Ndiyo tafakari ya Baba Mtakatifu Fransisko aliyotoa akiwaalika waamini wafanye tafakari ya dhamiri ndani ya mioyo. Ni wakati wa mahubiri ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 5 Oktoba 2018, ambapo ameongozwa na Injili ya siku ya Mtakatifu Luka, mahali ambapo, Yesu anawakaripia watu wa Betsaida, Corazin na Kafarnaum kutokana na kutomwamini japokuwa alitenda hata miujiza.

Yesu analia kwa ajili ya yule asiye kuwa na uwezo wa kupenda

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake anasema: “Yesu alishikwa na uchungu wa kukataliwa na watu wake, wakati miji ya kipagani kama Tiro na Sidonia kama wangeona miujiza hiyo labda wangesadiki. Yesu analia kwa sababu watu hawa hawakuwa na uwezo wa kupenda, wakati Yeye alikuwa anataka kuwafikia mioyo ya wote kwa njia ya ujumbe wake ambao haukuwa ni ujumbe wa udikteta bali ujumbe wa upendo.

Sisi tulizaliwa katika ukristo na tunasahau ya Kristo

Baba Mtakatifu hata hivyo amesema, katika nafasi ya watu wa miji mitatu, tujiweke sisi, wewe na mimi. Kwa mfano: Mimi niliyepokea mengi kutoka kwa Bwana, nimezaliwa katika jamii ya kikristo, nimemjua Kristo, nimejua wokovu, na  nimeelimishwa katika imani. Na kwa urahisi tu, ninamsahau Yesu. Na wakati huo huo tunasikia habari za watu wengine ambao kwa haraka wanasikiliza habari ya Yesu, mara moja wanamfuata”. Lakini sisi tumezoea tu, Baba Mtakatifu anabainisha.

Lakini hata hivyo mazoea hayo ni mabaya, kwani yanapunguza Injili kuwa suala la kijamii na katika elimu kijamii na siyo tena uhusiano binafsi na Yesu. Yesu anazungumza nami, na wewe, anazungumza na kila mmoja wetu. Mahubiri ya Yesu ni kwa kila mmoja wetu. Je ni kwa nini wapagani mara wanapomsikiliza akihubiri Yesu, wanamfuata nyuma, wakati mimi ambaye nimezaliwa hapa katika jamii ya kikristo, nimezoea na ukristo kama vile desturi ya kijamii na kama nguo ambayo nimevaa na ninaiacha? Kwa maana hiyo Papa anathibitisha: Yesu analilia kila mmoja na hasa yule anapoishi ukristo wa kawaida na usio wa kweli na dhati.

Unafiki wa wenye haki ni woga wa kupendwa

Lakini tunapofanya hivyo, Papa Fransisko anaweka bayana kuwa, sisi sote ni wanafiki, unafiki wa haki. Kuna unafiki wa wadhambi, lakini unafiki wa haki ni wenye woga juu ya upendo wa Mungu, hofu ya kuacha kupendwa na Yesu. Kwa dhati tunapofanya hivyo tunatafuta kuendesha mahusiano kati yetu na Yesu.  Papa anatoa mfano kuwa, wengi wanakwenda kanisani, lakini wanaporudi nyumbani Yesu harudi tena katika nyumba zao, katika familia, katika mafundisho ya watoto, shuleni na katika mitaa.

Tunajidai kuwa na Yesu wakati huo tumemfukuza

Kwa kufanya hivyo Yesu anabaki Kanisani tu, kubaki katika msalaba, au katika picha fulani. Baba Mtakatifu anasema, leo hii inawezekana kufanya tafakari ya dhamiri kwa pambizo hili: ole wako, ole wako, kwa sababu nilikupatia mengi, nimejitoa mimi mwenyewe , nimekuchagua uwe mkristo, na wewe unapendelea maisha nusu nusu, maisha ya kijuu juu: kidogo mkristo na maji yaliyobarikiwa, lakini hakuna cha zaidi. Kwa hakika unapoishi katika hali hiyo ya unafiki, chochote kile tunachofanya kinamfukuza mbali Yesu katika moyo wetu. Tunajidai kuwa naye, lakini tumemfukuza kwenda mbali. “sisi ni wakristo wenye ari ya ukristo na kumbe tunaishi kama wapagani.

Sala: wewe umenipatia mengi lakini sistahili

Kila mmoja, Papa anahitimisha, afikirie, je mimi ni Korazin, mimi ni Betsaida au Kafarnaum?  Na iwapo Yesu analia tuombe neema ya kulia hata sisi kwa njia ya sala hii: “Ee Bwana wewe umenipatia mengi. Moyo wangu ni mgumu ambao hauachi uingie. Mimi mdhambi na asiyestahili”. Na tuombe Roho Mtakatifu afungue milango ya mioyo yetu ili Yesu apate kuingia   na ili, si kusikiliza Yesu peke yake, bali hata kusikiliza ujumbe wake wa wokovu na kushukuru kwa ajili ya  mema aliyomfanyia kila mmoja wetu”.

 

 

 

 

 

 

 

 

05 October 2018, 14:35
Soma yote >