Misa ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa anaonya kuwa makini dhidi ya shetani mjanja!

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 12 Okotba amewaalika waamini kujilinda dhidi ya shetani anayekuja na ujanja wake, utafikiri kaelimika lakini baadaye ni kukupelekea uharibifu wa roho

Sr. Angela Rwezaula - Vatucan

“Sisi ni wakristo wakatoliki, tunakwenda katika misa na kusali na utafakiri kila kitu sahahii nna kawaida. Lakini tunazo kasoro zetu, dhambi zetu na utafikiri kila kitu ni kawaida.  Na shetani mwenye ujanja anakuja daima akiwa kama mwenye kuelimika, anabisha hodi akisema, “ninaweza kuingia? Na huo ndiyo mlio wa kengele.

Ni mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 12 Oktoba 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, akidadavua Injili ya Siku ya Mtakatifu Luka (11, 15-26). Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, “uwepo wa shetani ni uharibifu au moja kwa moja katika kupendelea mambo fulani, vita au hata vishawishi vya kutaka ufanye, hata kama anakuja kwa njia ya kuelimika, lakini njia hiyo inakupelekea katika roho kupenda malimwengu.

Tupo katika mapambano: ndani ya moyo wa kila mmoja kuna mapambani kati ya Yesu na ibilisi

 Shetani anapochukua nafasi ndani ya moyo wa mtu, anabaki pale kama nyumba yake na hataki kutondoka Papa anasema, na kuonesha kuwa Yesu analipo mfukuza shetani, alikwenda kutafuta makao ndani ya mtu na kumwaharibu kimwili. Mara nyingi Yesu aliwafukuza mbali mashetani na ambao ni marafiki wetu wa kweli. Mapambano kati ya wema na ubaya wakati mwingine utafikiri hauishi kamwe. Na kwa maana hiyo amesisitiza  Papa kuwa, mapambano ya kweli hawali ya yote ni mapambano kati ya Mungu na joka kuu la kizamani: kati ya Yesu na shetani. Mapambano haya pia ndiyo yapo hata ndani ya maisha yetu. Kila mmoja anapambana wakati mwingine bila kujua lakini daima tupo katika mapambano. Papa anaendelea kufafanua: “ Injili ya Siku inaanza na baadhi ya watu wanaotoa mashtaka ya Yesu kuwa, anaondoa shetani kwa njia ya Belzebul. Daima kuna midomo mibaya, Papa anasisitiza na kuongeza kusema:  “Na ndipo wanaanaza majadiliano kati ya Yesu na watu hawa”.

Wito wa shetani ni kuharibu kazi ya Mungu

Daima uwepo wa shatani unaharibu  na ndiyo Papa anathibitisha kuwa: “wito wake ni ule wa kuharibu kazi ya Mungu”. Papa Francisko amebainisha kuwa mara nyingi, hatari ni ile ya kuwa kama watoto ambao unyonya kidole wakiamini kuwa si hivyo bali ni ubunifu wa mapadre”. Shetani kinyume chake anabadili njia na  hasa anapoona hawezi kufanya hivyo uso kwa uso, labda mbele yake kuna nguvu ya Mungu ambaye analinda mtu huyo, basi yeye anakuwa mtundu kama mbwa mwitu, mjanja ambaye anatafuta njia nyingine  ya kuchukua nafasi katika mtu huyo.

Shetani anaharibu kwa njia ya upendeleo wa vita au kukupeleka katika njia ya unafiki

Kadhalika akiendelea na ufafanuzi Papa amekazia zaidi kutazama sehemu ya mwisho ya Injili ya siku ambapo amesisitiza juu ya roho mbaya iliyotoka kwa mtu yule na kukimbilia katika eneo la jangwa kutafuta makazi, kwa maana hiyo Papa  anaonesha kwamba: “ shetani anapokosa nafasi, anasema nitarudi katika nyumba yangu, mahali ambapo Yesu alikuwa amemfukuza na mahali ambapo alikuwa ameondoka. Anapokuja  anajifanya  kaelemilika, wakati alikuwa tayari amefukuzwa! Akifika anakuta njia imetengenezwa vizuri na kupambwa na anakaribisha roho saba nyingine mabaya zaidi ya kwanza na kuingia na kuchukua nafasi katika mtu ambaye anageukia kupindukia.

Papa ameonesha bayana jisni gani shetani asipofanikiwa, anajikita ndani ya upendelo wa mtu kwa njia ya vita, au mateso na daima anafikiria mkakati mwingine, na ambao mara nyingi unatumiwa na watu wote. Kwa maana hiyo: “Sisi ni wakristo, wakatoliki tunakwenda katika misa, tunasali na utafikiri kila kitu ni sawa . Ndiyo ni sawa lakini kwa makosa na dhambi zetu, utafikiri kila kitu ni sawa”.  Baba anafafanua na kuthibitisha: “ Ndiyo njia ya shetani anakwenda, anatazama na kutafuta jambo nzuri na kubisha hodi pale”. “Hodi, ninaweza kuingia? “Ndiyo kengele”.

Na hiyo ndiyo roho ya malimwengu, ndiyo roho ya dunia! Shetani anaharibu moja kwa moja kwa njia ya vita na ukosefu wa haki moja kwa moja, au kuharibu kwa ujanja na kidiplomasia na ndiyo maana Yesu ansema ,  kuweni makini wengi wanakuja hawapigi kelele, wanajifanya kuwa rafiki na kuwashawishi, hadi kukupeleka katika njia ya unafiki, kuwa mwenye ubaridi na njia kupenda malimwengu.

Roho ya ulimwengu

“Roho ya malimwengu ndiyo hii, ile inayoleta shetani aliye elimika”. Na ili kuhepukana nayo, Papa anakumbusha juu ya  sala ya Yesu, siku ile ya  Karamu Kuu ya aliyokuwa anamwomba Mungu atulinde dhidi ya roho ya kidunia na kuishi kwa kukesha na utulivu. Mbele ya shetani hawa walio elimika ambao wanataka kuingia katika mlango wa nyumba kama vile wamealikwa katika arusi, tuwambie: kesheni na tulia: Kesheni ndiyo ujumbe wa Yesu na kukesha Kikristo! Amethibitisha Papa Francisko.

12 October 2018, 14:12
Soma yote >