Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta 

Misa ya Papa:walei na wachungaji hatuogopi kuchafua mikono!

Katika Misa ya asubuhi na mapema kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta, tarehe 8 Oktoba 2018, Papa Francisko ameshauri walei na wachungaji kutafakari juu ya maana ya kuwa wakristo, na kuwashauri wawe wazi katika mshangao wa Mungu, hasa wakiwa karibu na wenye kuhitaji msaada

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mwaliko wa kuwa mkristo wa kweli, mkristo hasiye ogopa kuchafua mikono yake na nguo zake anapokuwa karibu na jirani mwenye kuhitaji, mkristo aliye wazi katika  kupokea mshangao, kama Yesu aliyelipa kwa ajili ya wengine. Ndiyo mbiu kuu ya ufafanuzi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko, katika Misa kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 8 Oktoba 2018. Mahubiri yake yametokana na Injili ya Mtakatifu Luka mahali ambapo Papa anatafakari juu ya watu waliotajwa katika somo,ambapo Yesu mbele ya walimu wa sheria wanamwema katika majaribu ya kuuliza: “je ni nani jirani?

Usipite kandoni: simama, kuwa na huruma na kutoa msaada

Wanyang’anyi walio mjeruhi mtu hadi kutoa damu, walimwacha nusu mfu: kuhani alipomwona jeruhi “alipitia kando, bila kuzingatia utume wake, kwa kufikiri mambo ya wakati   yaani, “saa ya Misa”; vilevile akafanya hivyo hivyo hata Mlawi, ambaye ni, “mtu aliyebobea katika utamaduni wa sheria”.  Kutokana na hilo, Baba Mtakatifu amejikita kufafanua katika suala linalohusu “kupitia kandoni”, mantiki ambayo anasema, “ijikite ndani ya mioyo yetu leo hii”.  Hiyo ni katika kutazama watu wawili ambao kwa dhati, anaongeza Papa, walisema rohoni mwao: “hiyo siyo shughuli yangu kumsaidia aliye jeruhiwa". Lakini ambaye hakupita kandoni, ni Msamaria na ambaye alihesabiwa ni mdhambi kwa mujibu wa watu wa Israeli”. Mwenye dhambi zaidi, Papa anabainisha, alishikwa na huruma kuu.

Katika hilo, Papa anaongeza kusema: "Si ajabu alikuwa ni mfanya biashara, akiwa safarini katika shughuli zake, au yeye hakutazama saa, na wala kufikiria damu. Alimkaribia, na kushuka juu ya punda  na kumfunga majeraha yake, na akayatia mafuta na divai”. Alijichafua mikono yake na nguo zake. Baadaye akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni” akiwa amechafuka na damu. Na ndivyo alitakiwa afike. Na akamtunza. Yeye hakusema: mimi ninamwacha hapa na waite madaktari waje, na mimi ninakwenda  zangu nimefanya kazi yangu. Hapana, yeye alimtunza, kwa maana ya kusema: sasa wewe ni wangu, na siyo kwa umiliki, bali kwa kukuhudumia. Yeye hakuwa mfanyakazi, bali alikuwa mtu wa moyo, mtu mwenye roho iliyofunguka na iliyo wazi.

Kujifungulia mshangao wa Mungu

Baba Mtakatifu akiendelea, amegusia juu ya mwenye nyumba ya wageni aliyebaki na mshangao wa kuona mgeni, mpagani namna hiyo, kwa maana tunaweza kusema, yeye hakuwa mtu wa Israeli ambaye alijithibithisha kutoa msaada kwa mtu, na kulipa dinari mbili na kuahidi chochote kitakachogharimiwa zaidi yeye atakaporudi atamlipa. Papa anaongeza kusema: “mashaka ya yule anayeishi na ushuhuda, ya yule anayejifungulia katika mshangao wa Mungu “ ndiye kama Msamaria!

Watu wote wawili hawakuwa ni wafanyakazi; Baba Mtakatifu anaongeza na kutoa mifano dhahiri akisema: “je Wewe ni mkristo? Ndiyo ndiyo, ninakwenda Misa kila Dominika na kutafuta kuwa mwenye haki, kutia gumzo kidogo kwa sababu ninapenda kuzungumza, lakini mambo mengine ninafanya vema”. Je wewe uko wazi?; uko wazi katika kupokea mshangao wa Mungu? Na wewe ni mkristo mfanyakazi aliyefungwa?  “ooh mimi ninafanya hiki na kile…, wakati wa Misa ya Dominika, ninapokea kumunio, naungama mara moja kwa mwaka, hili na lile… ninafanya kama kawaida”. Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, kwa kufanya hivyo ni ukristo wa kifanyakazi, wale ambao hawapo tayari kujifungulia mshangao wa Mungu, wale ambao wanajua mambo mengi ya Mungu lakini hawakutani na Mungu. Wale ambao kamwe hawashutuki na wala kuguswa mbele ya ushuhuda. Badala yake, hawana hata uwezo wa kutoa ushuhuda wenyewe binafsi, amesisitiza!

Yesu na Kanisa lake

Kadhalika, Baba Mtakakatifu ametoa ushauri kwa wote, “walei na wachungaji kujiuliza kama ni wakristo wanao mfungulia Bwana kile ambacho anatujalia kila siku, yaani mshangao wa Mungu ambao mara nyingi kama vile Msamaria, unatuweka katika matatizo na kulazimisha kubadili ukawaida wa sheria zilizowekwa. Baadhi ya wataalimungu fulani wa kale , Papa anakumbusha, walikuwa wanasema, kifungu hiki kinahitimisha Injili nzima”. Kwa maana hiyo: “Kila mmoja wetu ni mtu aliyejeruhiwa, na Msamaria ni Yesu, Yeye alituponesha majeraha, Alijifanya kuwa karibu nasi. Alitutunza sisi. Alilipa kwa ajili yetu. Na alisema katika Kanisa lake kuwa: Lakini kama kuna hitaji kuu zaidi, wewe lipa, nitakaporudi nitalipa”. Kwanjia hiyo Papa amehitimisha kwa kuthibitisha kuwa, sehemu kifungo hicho ndipo kuna Injili nzima!

 

 

 

 

08 October 2018, 13:02
Soma yote >