Tafuta

Vatican News
Misa Takatifu ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa Takatifu ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Misa ya Papa: Mkristo wa kweli anampenda Bwana kwa dhati!

“Marta na Maria wakiwa mstari wa mbele katika Injili ya siku, wanatufundisha jinsi gani ya kuishi maisha ya Kristo kwa kumpenda sana Bwana”. Papa Francisko amesema hayo katika mahubiri ya Misa,katika Kanisa la Mtakatifu Marta, akiwaalika kutathimini jinsi gani tunavyofanya kazi na pia kutoa muda wa kutafakari kwa kina Neno la Bwana

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ufunguo wa neno ambao hautakiwi kukosewa katika maisha yetu ya kikristo ni ule wa kupenda Bwana, pia kwake kuchota kila aina ya matendo yetu. Kama alivyokuwa Paulo, Mtume ambaye leo hii anajieleza maisha yake binafsi katika Somo lake kutoka katika barua ya Wagalatia. Kufanya ulinganifu huo kwa dhati kati ya kutafakari na huduma, ni mambo mawili muhimu ambayo yanajionesha katika Injili ya Mtakatifu Luka, inayojikita katika kutazama sura ya Marta na Maria, dada zake Lazaro huko Betania, mahali ambapo Yesu amekaribishwa katika nyumba yao. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 9 Oktoba 2018

Wakristo wanao jishughulisha lakini hawana amani: Hawa ni dada wawili ambao kwa namna yao ya utendaji kazi, Papa anafafanua, wanatufundisha ni jinsi gani ya kuendeleza maisha mbele ya kikristo. Maria alikuwa anasikiliza Bwana, wakati Marta yuko pembeni kwa sababu ya kushughuli za huduma. Lakini tazama, Baba Mtakatifu anaongeza, Marta ni kama wanawake wenye nguvu, mwenye uwezo hata wa kumkaripia kwa Bwana kwa kuwa hakuwepo wakati mauti yanawadia kwa kaka yake Razaro. Marta anatambua kujiweka mbele na kuwa jasiri , lakini wakati huo huo anakosa hata  muda wa kutafakari, yaani ukosefu wa kuwa na muda wa kutafakari kwa kina zaidi akimtazama Bwana!

Wapo wakristo wengi wanaokwenda Kanisani siku ya Jumapili, lakini wakiwa na mambo mengi ya kufanya daima. Hawana htya muda kwa ajili ya watoto wao na hata kuchea nao. Baba Mtakatifu amesema, hiyo ni mbaya! Ni katika mkusanyiko wa  mengi ya kufafanya daima, wakati kumbe inahitaji kusimama na kutazama Bwana, kuchukua Injili na kuisoma, kusikiliza Neno la Bwana ili likufungue moyo…. siyo lugha kufanya mambo mengi daima yaliyopo katika mikono yanamfanya mtu awe mwema na kumfanya awe mwanadamu mwema, hasa akikosa hata kukaa na kutafakari  na ndiyo Marta alikuwa anakosa jambo hilo muhimu sana, Baba Mtakatifu amebainisha.

Kutafakari siyo kwamba ni kukaa tu, kupumzika bila kufanya lolote: Kutafakari siyo kwamba ni kukaa tu na kupumzika bila kufanya chochote, badala yake Maria alikuwa akitamzama Bwana kwa sababu Bwana alikuwa akigusa moyo wake na mahusiano ya Bwana; hiyo ndiyo nguvu inayotoka hapo ya kuweza kuendelea mbele baadaye. BabaMtakatifu ameongeza mfano: “hiyo ndiyo kanuni ya Mtakatifu Benedikto, Ora et labora” ambayo wamonaki wa kike na kiume katika konventi zao wanajikita, kwa hakika, na  hawashindi siku nzima wakitazama juu mbinguni. Wao wanasali na kufanya kazi. Na hasa kama alivyo kumbusha Mtakatifu Paulo, katika somo la kwanza kuwa: “ Mungu alipomchagua, hakwenda kuhubiri haraka, bali alikwenda kwanza kusali na kutafakari kwa kina matendo ya Yesu Kristo ambaye aliokuwa amejionesha kwake.

Kila kitu ambacho Paulo alifanya, alifanya katika roho hiyo ya kutafakari na kutazama Bwana.  Bwana ambaye alikuwa akuzungumza ndani ya roho yake, na Paulo alikuwa amempenda sana Bwana.  Na ndiyo ufunguo wa Neno ambalo haiwezekani kukosea yaani kupenda sana.  Siyo kwa namna ya kutaka kujua, tuko sehemu gani, au kusizidisha kiasi cha kutafakari sana, hadi kufikia kutokuwapo. Au kuhangaika na kuzidi, bali tunapaswa kujiuliza swali; je ninampenda sana Bwana kiasi gani? Ninao uhakika kuwa yeye amenichagua? Au ninaishi ukristo wangu hivyo kwa kufanya mambo mengi hiki na kile lakini, je ninatafakari ndani ya moyo wangu?

Kutafakari na huduma: njia ya maisha yetu: Kutafakari na huduma ni njia ya maisha yetu Baba Mtakatifu anatoa mfano ni sawa na jinsi mwamaume anarudi nyumbani kutoka kazini, anapokelewa na mke wake kwa mikono miwili. Hiyo ndiyo upendo wa kweli, na  hamkaribishi tu na kuendelea kufanya shughuli zake, badala yake, anatumia muda wa kukaa naye. Hiyo ndiyo hatua ambayo tunachukua muda kwa ajili ya Bwana kumhudumia kwa wengine, Baba Mtakatifu amehimiza.

Kutafakari ni huduma, na ndiyo njia ya maisha. Kila mmoja afikirie ni muda gani anautumia kwa siku kutafakari fumbo la Yesu. Na vivyo hivyo hata muda wa kazi? Ninafanya kazi sana, utafikiri ndiyo mazoezi au kazi ya dhati katika imani yangu, kazi kama huduma ambayo inatokana na Injili? Kwa kufanya hivyo itakuwa vema kwa siku hii Baba Mtakatifu amehitimisha.

 

 

09 October 2018, 15:57
Soma yote >