Tafuta

Vatican News
Misa katika Kanisa la  Mtakatifu  Marta: hekima ni ile ya kutambua kukutana na mambo madogo ya maisha ya Yesu Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta: hekima ni ile ya kutambua kukutana na mambo madogo ya maisha ya Yesu  (Vatican Media)

Misa ya Papa: Matumaini ya dhati ni kuishi kwa kukutana na Yesu!

Papa Francisko katika kutafakari misa ya asubuhi 23 Oktoba ametumia mfano wa mwanamke mjamzito anayesubiri mtoto kwa matumaini ya kweli. Na matumaini ya kweli ni yale ya kukutana kwa dhati ya Yesu, kama ilivyo hekima, ni ile ya kutambua kukutana katika mambo madogo ya maisha ya Yesu

Na Sr. Angela Rwezaula

Mwanamke mjamzito anayesubiri kwa furaha kukutana na mtoto ambaye anazaliwa , na kila siku anagusa tumbo lake akibembeleza. Ndiyo sura ambayo Baba Mtakatifu ameitumia wakati wa kuanza mahubiri yake katika Misa ya asubuhi tarehe 23 Oktoba 2018, katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Ametumia mfano huo  ili kuelezea nini maana ya matumaini na kwamba ni kushi kwa matarajio ya kukutana kwa dhati na Yesu, na siyo jambo lisilokuwapo bali la dhati. Na hekima ni ile ya kutambua kufurahia mikutano midogo ya maisha ya Yesu.

Utambulisho na urithi

Baba Mtakatifu katika mahubiri yake, anaongozwa na maneno mawili ya ujumbe wa liturujia ya siku: utambusho na na urithi, meneno mawili yaliyosikika katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa waefeso (Ef 2,12-22). Na kwamba ndiy zawadi ambayo Mungu. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; akatupatia utabulisho na zawadi kuu. Mungu wa Yesu kwa dhati aliondoa sheria ili kutupatanisha na kuonda kabia uadui , na ili sisi sote tuweze kuwa ndugu mmoja kwa wengine kwa Baba na katika Roho , kwa maana hiyo amefutanya wamoja, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Kwa namna hiyo mungu anatufanya tutembee kuelekea urothi kwa uhakika huo na ule wa kuwa wazalendo na mabo Mungu yuko pamoja nasi. Urithi ni ule ambao sisi sote tunautafuta katika hija yetu , na ambao tutaupokea siku ya mwisho. Lakini ni lazima kuutafuta kila siku, ni ule ambao tunaupeleka mbele katuka safari ya utambulisho kuelekea urthi ule ule wa matumaini, labda fadhilia ambayo ni ndogo na labda pia ngumu kuitambua, papa Francisko anasisitiza.

Iwapo unatumainia,utapungukiwa kitu

Imani, matumaini na upendo ni zawadi. Imani ni rahisi kuitambua kama ilivyo pia upendo. Lakini matumaini ni kitu gani? Ni swali la Baba Mtakatifu akibainisha lakini kuwa ni kutumainia mbingu, kukutana na watakatifu katika furaha ya milelele. Je kwa upande wako mbingu ni nini? Baba ;takatifu ameuliza kwa mra nyingine tena: Akijibu: “kuishi matumaini ni kutembea kuelekea katika kupokea zawadi, kuelekea katika futaha ambayo hatuna hapa na mabyo lakini tutaipokea kule… ni fadhilia ngumu kuitambua. Ni fadhila ya kinyenyekevu sana. Lakini inaweza kuwa ya dhati kwa namna ambayo ninatambua mbingu au ile inayonisubiri? Matumaini, urithi wetu ambao ni matumaini kuelekea jambo , hina wazo , aina sehemu ambayo ni nzuri, hapia ni mkutano. Yesu daima anasisitiza sehemu hii ya matumaini, yakuwa na matarajio na kukutana, amesema Baba Mtakatifu! Mwanamke mjamzito anayesubiri kukutana na mwanae.

Katika Injili ya Lk 12:35-38

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao. Injili ya siku kutoka Mtakatifu (Luka 12,35-28) Yesu anawaambia wawe tayari kama watu wanaomgojea bwana wao atakaporudi kutoka arusini. Na hivyo dimani ni mkutano na Bwana ambao ni jambo la dhati, Na ili kufanya hivyo Papa Francisko anatoa mfano wa dhati kuwa, yeye  akifikiria juu ya matumaini, wazo limjia mara moja sura ya mwanamke mjamzito ambaye anasubiri mtoto.

Anakwenda kwa daktari na kupimwa kwa ultra soudni hasemi nimemwona sawa… hapana bali anafuraha:! Na kila siku anagusa tumo lake na kumbembeleza mtoto, kwa maana anamsubiri huyo mtoto na anaishi akitajarajia huyo mtoto. Picha hiyo inaweza kutufanya kutambua nini maana ya matumaini, yaani kuishi kwa kutarajia kukutana. Mwanamke huyo hafikiri kwanza jinsi gani macho ya mtoto wake yatakuwa, tabasamu lake, au atakuwa na nywele za kipilipili au laini,  bali anafikiria kukutana na mtoto wake.

Kutambua namna ya kufurahia mikutano midogo na Yesu

Kadhalika Baba Mtakatifu akiendelea juu ya matumaini , amethibithsa kuwa sura hiyo ya mwanamke mjamzito inaweza kweli kusaidia kujia nini maana ya matumaini na kujiuliza : je mimi ninatarajia namna hiyo kwa dhati au matarajio yangu yamechanyika, kidogo kutoamini? Matumaini ni ya kweli, ni ya kila siku kwa sababu ya kukutana. Kila mara tunapokutana na Yesu katika Ekaristi, sala, Injili, masikini , katika maisha ya jumuiya, ndiyo, hiyo ambayo  kila mara tunafanya hatua moja mbele kuelekea katika mkutano wa mwisho.

Hitimisho la Baba Mtakatifu katika mahubiri yake, anasititizia tena juu ya neno utambulisho ambao umetufanya sisi wote kuwa jummuiya na urithi na ambao kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, anayepeleka mbele matumaini, pia kuwahimiza kama wakristo kwamba tunasubiri urithi wetu huko mbinguni ikiwa na maana ya kweli ya kukutana.

 

 

 

 

23 October 2018, 14:23
Soma yote >