Misa Takatifu ya Papa Francisko wakati wa Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu Misa Takatifu ya Papa Francisko wakati wa Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu  (Vatican Media)

Papa:Ushindi wa Yesu unaangaza wakati wetu mgumu wa msalaba!

Katika Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, Papa Francisko amejikita katika mahubiri yake kutafakari juu ya kushindwa lakini hata kutukuka kwa Yesu ambaye alibeba dhambi za dunia. Shetani alifungwa minyororo lakini anakuja iwapo unamkaribia na kukuharibu.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

“Msalaba wa Yesu unatufundisha kuwa katika maisha kuna kushindwa na ushindi, na usiogope kipindi kigumu ambacho kinaweza kuangazwa na msalaba ambao ni ishara ya ushindi wa Mungu dhidi ya mabaya. Ni mbaya shetani lakini aliyeharibiwa  na kufungwa mnyororo, pamoja na hayo bado anabweka, iwapo unamkaribia na kumbembeleza, atakuharibu”. Ndiyo sehemu ya tafakari ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe14 Septemba, 2018 wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu.

Ushindi wa Yesu unaangaza wakati wetu mgumu:  Katika kutafakari msalaba, kwatu sisi wakristo ni ishala kwani ni kutafakari ishara ya kushindwa, lakini hata ishara ya ushindi. Katika msalaba ni kushindwa kwa  chochote kile ambacho Yesu alikuwa amefanya na kupoteza matumaini ya watu waliokuwa wanamfuata Yesu”.

Na wakati huo sisi tunakuwa na hofu ya kutafakari msalaba wakati wa kipindi cha kushindwa anathibitisha Baba Mtakatifu. Lakini Paulo anapotafakari juu ya fumbo la Yesu Kristo, anatoa maneno ya nguvu kwamba, Yesu alijitoa yeye binafsi, akajinyenyekeza na kuwa mdhambi hadi mwisho kwa  kubeba dhambi zetu, dhambi zote za ulimwengu: alikuwa hana sura na kuhukumiwa.  Paulo  hakuwa na hofu ya kuwaonesha kushindwa, hiyo inaweza kuangaza kidogo wakati wetu mgumu, lakini hata sisi wakristo  msalaba ni ishara ya ushindi.

Siku ya Ijumaa Kuu Takatifu, kuna mtego mkubwa wa Shetani: Katika Biblia kwenye  Kitabu cha Hesabu, Sura ya kwanza  linaeleza kipindi cha wayahudi walivyokuwa wanalalamika, hadi wakapata adhabu ya kuumwa na nyoka. Lakini Msalaba unaalika kutazama nyoka wa kizamani, Shetani, Mshitaki Mkuu, Baba Mtakatifu anakumbusha. Nyoka ambaye alikuwa anasababisha kifo, Bwana alimwambia Musa kuwa atasimamishwa na kutoa wokovu. Huo ndiyo unabii. Baba Mtakatifu anakazia,  kwa maana Yesu aliyejifanya mdhambi na alimshinda mdau wa dhambi; alimshinda shetani. Shetani alikuwa na furaha sana siku ya Ijumaa Kuu Takatifu. Baba Mtakatifu anaongeza: alikuwa na furaha kiasi cha kusahau kuwa huo ulikuwa ni mtego mkubwa wa kihistoria kwa manaa baadaye alikuwa anaanguke

Anammeza Yesu lakini hata ukuu anaupoteza

Kama wasemavyo mababa wa Kanisa kuwa Shetani alimwona Yesu kama vile samaki mwenye njaa aonapo ndoana ikilea na kukimbia kudoa chakula na kwa maana hiyo Shetani aliharibiwa daima. Hana nguvu. Na msalaba wakati huo ukawa ishara ya ushindi.

Nyoka wa azamani amefungwa lakini usimkaribie: Ushindi wetu ni msalaba wa Yesu , ushindi mbele ya adui wetu ambaye ni  nyoka mkubwa kizamani na Mshitaki Mkuu. Kwa njia ya msalaba sisi sote  tumekombolewa, kwa njia ya  mchakato ambao Yesu alitaka kufanya hadi kuinama chini, lakini akiwa na nguvu ya kimungu.

Yesu alimwambia Nikodemu “ Nitakapoamshwa chini nitawavuta wote kwangu”. Yesu aliye amshwa na Shetani akatokomezwa. Msalaba wa Yesu lazima utuvute sisi, kuutazama kwani ni nguvu ili twenda mbele. Na nyoka wa kizamani aliyeharibiwa lakini bado anabwekana kuhatarisha, maana mababa wa  Kanisa walisema, mbwa aliyefungwa mnyororo usipomkaribia hawezi kukuuma; lakini ukienda na kumkaribia, kwa maana anavutia na utafikiri ni mbwa  mwema, jiandae atakuharibu!

Mbele ya Msalaba kuna ishara ya kushindwa na kushinda: Maisha yetu  yanakwenda mbele, lakini pia Papa anabainisha kwamba ni kwa njia ya Kristo mshindi na mfufuka na ambaye anatutumia Roho Makatifu, lakini  pia kukumbuka kuwa kuna  hata mbwa aliyefungwa na ambaye “sipaswi kumkaribia kwa maana anaweza kunirarua”.

Kutokana na hilo  Baba Mtakatifu amehitimisha akisema: “tunapaswa kuwa na uwezo wa kuvumilia kushindwa na kubeba msalaba kwa uvumilivu kushindwa kwetu hata kwa dhambi zetu kwa maana yeye amelipa kwa ajili yetu.  Kuvumilia katika yeye, kuomba msaada kwake, lakini si kujiachia katika udanganyifu wa mbwa aliyefungwa na mnyororo”. Aidha leo hii itakuwa vizuri kukaa nyumbani kwa dak 5, 10,15 mbele ya msalaba ambao upo ndani ya nyumba au uliopo katika Rosari; kuutazama maana ni ishara ya kushindwana ambayo ilitokana na mateso ambayo yanatuharibu, wakati huohuo ni ishara kwetu ya ushindi kwa maana Mungu alishinda pale.

14 September 2018, 14:23
Soma yote >