Tafuta

Vatican News
Papa Francisko wakati wa Misa Takatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta Papa Francisko wakati wa Misa Takatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta 

Papa: Mbele ya yule anayetafuta kashfa ni kubaki kimya na sala!

Maadhimisho ya kwa mara nyingine tena ya Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta yameanza, ambapo Baba Mtakatifu Francisko akitafakari Injili ya siku, anasema wakati mwingine, kashfa na migawanyiko, inaweza kumalizika kwa njiaya ukimya na maombi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ukweli ni upole; Na ukweli ni ukimya, dhidi ya watu ambao wanatafuta kashfa tu na kutafuta nmna ya kugawanya tu. Njia mojawapo ya kufuata ni ile ya ukimya na maombi. Ndiyo msisitizo wa mahubiri ya Papa Francisko, wakati wa maadhimisho ya misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Jumatatu tarehe 3 Septemba 2018 mjini Vatican.

Anafungua mahubiri yake, kuanzia na Injili ya siku ya Mtakatifu Luka iliyosomwa (Lk 4, 16-30), mahali ambapo Yesu alirudi Nazareth na kupokelewa kwa wasiwasi. Baba Mtakatifu amesema, Neno la Bwana linaangaza katika kusimulia na kufanya kutafakati namna ya kutenda katika maisha yetu ya kila siku hasa panapojitokeza ile hali ya kutoelewana, wakati huohuo, kuwa na utambuzi  ya kwamba kuna baba wa uongo, mshtaki, yaani shetani anayetenda kwa kuharibu umoja wa familia  na umoja wa watu.

Hakuna nabii anayepokelewa katika nchi yake

Yesu mara baada ya kufika katika Sinagogi, alipokelelewa kwa mashaka makubwa: Wote walitaka kuona kwa macho yao yale matendo makubwa ambayo ameweza kutenda katika maeneo mengine. Lakini Mwana wa Baba wa mbinguni Baba Mtakatifu Francisko anafafanua, anatumia Neno la Mungu, na hiyo ni tabia yake ambayo anaitumia, hata alipotaka kumshinda shetani. Hiyo ndiyo tabia ambayo ni ya unyenyekevu ambao unaacha nafasi kwanza  katika ngazi ya Neno  anathibitisha Papa Francisko na kusisitiza kuwa, ni Neno ambalo linapanda wasiwasi, na ambalo linapelekea mabadiliko katika hali ya amani kwenye  kvita, la kuleta mshangao katika chuki. Kwa ukimya wake,Yesu anashinnda hata mbwa mwitu, anashinda shetani ambaye alikuwa amepanda hila na uongo katika moyo.

Wale hawakuwa ni watu, bali walikuwa ni mbwa mwitu, na ambao walimfukuzia katika mji wao. Hawakuwa na mawazo bali walikuwa wakipiga kelele. Na Yesu akiwa kimya… baadaye wakaondoka wakamtoa nje ya mji wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini. Sehemu hii ya Injili inaitimisha hivi: “Lakini yeye alipitia katikati yao akaenda zake”.

Hadhi ya Yesu:

Ukimya wake unashinda sauti za mbwa mwitu hao na kwenda zake. Kwasababu ilikuwa haijatimia saa yake. Na ndilo tendo litakalo tokea Siku ya Ijumaa Kuu; Dominika ya Matawi watu hao  walikuwa wamefanyia sikukuu Yesu na kumwambia, Mbarikiwa, wewe Mwana wa Daudi, na Ijumaa kuu wote wanasema Asulibiwe; Ni shetani alikuwa wamewabadili kwa hila za uongo katika mioyo yao na Yesu alikuwa kimya!

Ukweli ni  upole

Ukweli ni upole kwa sababu Baba Mtakatifu anathibitisha,  hali hiyo inatufundisha kwa namna ya ketenda hasa inapojitokeza hali ya kutoona ukweli, ni kubaki kimya. Ukweli unashinda, lakini pia kwa njia ya msalaba. Kwa maana hiyo ndiyo maana ya  ukimya wa Yesu, lakini je ni mara ngapi katika familia wanapoanza mabishano juu ya siasa, michezo, fedha na wakati mwingine familia nyingine inaisha kuharibika kwasababu ya mabishano hayo, ambayo shetani anaonekana kuwatengenisha na kuwaharibu…  Hiyo inahitaji ukimya…anadhibitisha Papa.  Ni vema kusema  linalohusu na kukaa kimya: kwasababu ukweli ni upole, ukweli ni ukimya, ukweli hauna kelele. Pampja na hayo Papa anathibitisha kuwa, “siyo rahisi kutenda kama alivyo fanya Yesu; lakini kuna hadhi ya kikristo ambayo bado imesimikwa katika nguvu ya Mungu”. Watu wasio kuwa na mapenzi mema;  watu wanao tafuta kashfa tu , ambao wanatafuta migawanyiko tu  na kutafuta uharibifu tu, hata katika familia, inahitajika ukimya na maombi,  anasisitiza Baba Mtakatifu !

Hadhi ya ushindi wa ufufuko:

Baba Mtakatifu amehitimisha mahubiri yake kwa sala hii: “Ee Bwana utupatie neema ya kung’amua hasa tunapotaka kuzungumza na tunapotaka kunyamaza. Hii ni katika maisha yot: katika kazi, nyumbani,na katika jamii na kwa njia hiyo tutakuwa ni kumeiga  zaidi Yesu”.

03 September 2018, 16:24
Soma yote >