Misa katika Kanisa la Mtakatifu  Marta Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa:Katika historia,Kanisa limeteswa na wanafiki!

Katika Misa ya Papa Francisko amesema kuwa shetani ni mwenye nguvu na anaitumia kuharibu watu, kuharibu jamii na kuharibu Kanisa. Ngamia wa mapambano ya shetani ni unafiki kwa sababu yeye ni muongo. Anajifanya kuonekana ni mfalme wa nguvu, mzuri na wakati huohuo ni muuaji

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Tuombe Yesu alinde daima kwa huruma na msamaha wake Kanisa lake ambalo ni Mama na Takatifu, lakini lililojaa wadhambi kama sisi”. Ndiyo sala ya Baba Mtakatifu iliyosikika wakati wa mahubiri ya Misa Takatifu ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 20 Septemba 2018, akitafakari juu ya Somo la Kwanza la Barua ya Mtakatifu Paulo kwa wakorinto na Injili ya siku ya Mtakatifu Luka ambayo imejikita katika maneno ya Yesu: “Dhambi zako nyingi zimeondolewa kwakuwa ulipenda sana”.

Yesu anatazama ishala ndogo ya upendo: Katika kutafakari Baba Mtakatifu ametazama kwa haraka hali halisi na kuwagawa watu katika makundi matatu katika masomo ya hayo: Yesu na wafuasi wake; Paulo na mwanamke, yule ambaye mwisho wake Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa alikuwa anataka kumtembelea  akiwa amejifucha kwa mafarisayo, au alikuwa na hatari ya kupigwa mawe; na kundi la tatu ni lile la walimu na waandishi.

Papa Franciskoko ameonesha jinsi gani mwanamke huyo alionesha upendo wake mkubwa kwa Yesu kwa maana hakuficha kuwa yeye ni mdhambi. Ni pamoja pia na Paulo anayethibitisha kuwa: “ kwenu ninyi nimewaonesha hawali ya yote kile nilichokipokea, yaani kwamba, Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu”. Kwa pande zote mbili, walikuwa wanamtafuta Mungu kwa upendo, lakini upendo huo kwa nusu. Kwa maana Paulo anaeleza wazi kuwa, alikuwa anafikiria upendo kama sheria na alikuwa na moyo uliofungwa kulezea hata kutokewa kwa Yesu Kristo. Aliwatesa wakristo, lakini kwa sababu ya kufuata sheria na ndiyo maana haukuwa upendo mkomavu. Na mwanamke alikuwa anatafuta upendo, ulio mdogo. Ndiyo maana wafalisayo walianza manung’uniko, lakini Yesu anawakatisha na kuwaeleza.

Yeye amesamehewa dhambi zake nyingi kwa sababu amependa sana. Lakini je  ni jinsi gani ya kupenda? Hawa hawakujua kupenda. Wanatafuta upendo. Siku moja Yesu akizungumza walifasayo alisema watu hao watakuwa mbele ya Ufalme wa Mungu ... Lakini mafalisayo wakaanza kunung’unika tena ni, kwa  jinsi gani, kwa maana  hii ni kashfa! Baba Mtakatifu amebainisha kuwa mara nyingi, Yesu anatazama ishala ndogo ya upendo, ishala ya utashi mwema na anamchukua na kumpeleka mbele. Na hiyo ndiyo huruma ya Yesu, kwa maana yeye daima anasamehe na anapokea.

Kashfa ya wanafiki:  Kwa mtazamo wa walimu wa sheria, Papa Francisko amesisitiza juu ya mtindo na tabia ya wanafiki watumiazo mara kwa mara, yaani ni kukashifu na kusema “ tazama, hiyo ni kashfa ! na haiwekani kuishi hivyo… tumepoteza thamani. Kwa sasa wote hawana haki ya kuingia katika Kanisa, hata wanye talaka wote. Lakini Baba Mtakatifu anauliza je tuko wapi?

Baba Mtakatifu akifafanua juu ya Kashfa ya wanafiki anasema: Hayo ndiyo mazungumzo kati ya upendo mkubwa ambao unasamehe yote, upendo wetu ni nusu nusu  kama wa Paulo, na wa mwanamke yule, ambao ni upendo usio mkamilifu kwa maana hakuna yoyote aliyetangezwa mtakatifu, na tusema ukweli Baba Mtakatifu ameongeza.   Kadhalika akifafanua unafiki anasema: upo unafiki wa kujamini wenye  haki, unafiki wa kuamini ni  wasafi na ambao wanaamini wamekombolewa kwa ajili ya manufaa yao kijujuu.

Katika historia,  kanisa linateswa na wanafiki: Yesu anatambua watu hao wanaoishi kijuu juu na kujionesha wazuri na ambao anawafananisha na  makaburi  yaliyopakwa rangi nyeupe, wakati ndani kumejaa mawe na mifupa. Kanisa linapotembea katika historia daima limeteswa na wanafiki hawa, na  ni wanafiki kutoka ndani na nje. Shetani hana kazi na wadhambi waliotubu, kwa maana wanamtazama Mungu na kusema “ Bwana mimi ni mdhambi nisaidie”. Shetani ni mwenye nguvu, lakini mwenye nguvu kwa wanafiki. Ni mwenye nguvu na anaitumia kuharibu watu, kuharibu jamii na kuharibu Kanisa. Ngamia wa mapambano ya shetani ni unafiki kwa sababu yeye ni muongo.  Anajifanya kuonekana ni mfalme wa nguvu,mzuri na wakati huo huo ni muuaji.

Kutokana na hilo Papa Francisko ametoa ushauri, wasisahau kuwa Yesu anasamehe, anapokea, anatumia huruma, neno moja ambalo mara nyingi limesahuliwa, hasa  tunapoanza kuwasengenya wengine. Kwa maana hiyo wito ni kuwa na huruma kama Yesu na tusiwahukumu wengine. Yesu awe kitovu. Yesu kwa hakika anasamehe  na hata Paulo aliyekuwa anatesa, lakini kwa upendo wake hata kwa mwanamke mdhambi aliye kuwa na upendo usio mkamilifu. Ni kwa njia hiyo tu, inawezekana kukutana na upendo wa kweli ambao ni Yesu na wakati huohuo wanafiki hawana uwezo wa kukutana na upendo kwani mioyo yao imefungwa.

20 September 2018, 14:31
Soma yote >