Misa ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (� Vatican Media)

Papa: mchungaji ni mtiifu, anateseka,anasali na kujishutumu!

Papa Francisko, katika mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta, amekumbusha kuwa Yesu ni picha ya Mchungaji, alikuwa na madaraka kwa sababu ya unyenyekevu na huduma ambayo ilijieleza kwa utiifu na upole. “ Hata sisi wachungaji” lazima tuwe karibu na watu na si kwa wenye nguvu au wenye itikadi” mambo yanayotia sumu roho”

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

 “Jambo ambalo lilimpatia mamlaka Yesu kama mchungaji ilikuwa ni unyenyekevu wake, ukaribu wa watu, huruma ambayo ilijieleza kwa utii na upendo. Iwapo mambo yalimwendea vibaya kama vile akiwa juu ya Kalvario, alibaki kimya na kusali”. Ndiyo ufafanuzi uliopo katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa Misa ya asubuhi tarehe 18 Septemba 2018, kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, ambapo Papa anapendekeza kwa upya juu ya Yesu kama Picha na mfano wa uchugaji kwa madaraka ambayo ni neema ya Roho Mtakatifuna madaraka hayo yalitokana na uwepo karibu na watu, si katika kujiingiza katika vikundi vidogovidogo vya wenye nguvu na wenye itikadi.”

Ufufuko wa mwana wa pekee wa mama mjane: Baba Mtakatifu akitafakari Somo la Injili ya Siku ya Mtakatifu Luka, inayoonesha miujiza ya ufufuko wa Mwana wa pekee wa Mama mjane, amesisitiza: “Yesu alikuwa na madaraka mbele ya watu, si kwa ajili ya mafundisho aliyokuwa akihubiri, na ambayo karibu yalikuwa kama ya wangine, bali yeye alikuwa ni “mnyenyekevu na mpole wa moyo”. “Yeye hakuwa anapiga kelele na kusema mimi ni Masiha, au mimi ni Nabii; Yeye hakuwa anapiga tarumbeta wakati akiponya mtu au katika kuhubiri watu, au kufanya miujiza kama vile miujiza ya mikate. Hapana, Yeye alikuwa ni mnyenyekevu na alikuwa hivyo na kuwa karibu na watu”.

Yesu ni karibu na watu na walimu wa sheria hapana: Baba Mtakatifu akiendelea, anawatazama hata walimu wa sheria kwamba, wao hawakuwa karibu kwa maana walikuwa wanafundisha juu ya madhabahuni na walikuwa mbali na watu”. Hawakujihusisha na watu, bali walikuwa ni kutoa amri na ambazo walizidi kuongeza hadi   kufikia zaidi ya 300”; hawakuwa karibu kabisa na watu amesisitiza.

Katika Injili, Baba Mtakatifu anasema, Yesu kama hakuwa na watu, alikuwa na Baba anasali. Na sehemu kubwa ya muda wa maisha yake Yesu, katika utume wake, Yeye alitumia akiwa njiani na kukaa na watu. Huo ndiyo ukaribu, anasisitiza na kuongeza papa: “unyenyekevu wa Yesu ni ule unaotoa mamlaka na kwamba  na unampeleka awe karibu na watu.Yeye alikuwa anagusa watu , anawakumbatia na kuwatazama machoni, kadhalika alikuwa anawasikiliza.  Hiyo ndiyo ilikuwa inamfanya awe na mamlaka!.

Alikuwa na uwezo wa kuteseka na, alifikiri kwa moyo:  Mtakatfu Luka katika Injili anasisitiza juu ya “huruma kubwa” aliyokuwa nayo Yesu, alipo mwona mama mjane akiwa peke yake na mtoto aliyekufa. Yesu alikuwa na uwezo wa kuseseka na hakufanya hivyo kinadharia. Kwa maana hiyo unaweza kusema kuwa alikuwa akifikiri kwa moyo  na moyo wake haukutengana  kamwe na kichwa chake”. Kuna aina mbili za huruma katika hatua hiyo. Baba Mtakatifu amependa kusisitizia kuwa ni  “Upole na unyenyekevu”. Yesu anasema, “Jifunze kwangu maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo”.

Unyenyekevu: Yeye alikuwa ni mnyenyekevu kwa maana hakupiga kelele. Hakutoa adhabu kwa watu, kwa maana alikuwa ni mnyenyekevu na  daima. Je Yesu alikuwa anakasirika? Baba Mtakatifu amethibitisha, Ndiyo!  “ Tufikiri alipoona nyumba ya Baba yake imegeuka kuwa soko, wakiuza vitu na kubadilishana fedha… hapo alikasirika na akachukua mjeledi kuanza kutawanya vitu hovyo na kuwafukuza wote mbali. Lakini hiyo ni kwa sababu alikuwa anampeda Baba,na alikuwa ni mnyenyekevu mbele ya Baba yake na ndiyo maana alikuwa na nguvu.

Huruma ambayo ni ya upendo na upole: Akifafanua juu ya upole: Yesu hakusema “usilie mama, ukiwa mbali… Hapana. Yeye alimkaribisa, labda hata alimgusa mabega au hata kumpa pole. “Usilie”. Huyo ndiye Yesu.  Na Yesu anafanya hivyo kwetu sisi, kwa maana yuko karibu,na yuko katikati ya watu na ni mchungaji”.

Ishara nyingine ya huruma ni “ile ya kumchukua mtoto na kumrudishia mama yake. Katika maana  hiyo, unyenyekevu na upole wa moyo, ukaribu wa watu, kuwa na uwezo wa kuteseka na kuwa na huruma, hata matendo hayo mawili ya upole na unyenyekevu, ndiyo tabia ya Yesu na ndiyo Yesu Mwenyewe”.  “Anafanya matendo hayo kwetu sisi anapotukaribia, kama alivyo fanya kwa mtoto huyo na mama yake mjane”.

Yesu ni picha ya mchungaji ambaye tujifunze kutoka kwake: Hiyo ndiyo picha ya mchungaji, Baba Mtakatifu ametilia mkazo na kuongeza kusema, ishara hiyo ndiyo lazima sisi wachungaji tujifunze: “kuwakaribia watu, na siyo kukaribia vikundi vya wenye nguvu na wenye itikadi…Kwa maana hivyo  vinatia sumu roho,na hatuwezi kufanya vizuri!”. Mchungaji kwa namna hiyo lazima awe na nguvu na madaraka ambayo Yesu alikuwa nayo ya unyenyekevu, upole na ukaribu, uwezo wa kuteseka na kuwa na huruma”.

Mchungaji anayeshutumiwa hujeruhiwa, hutoa maisha na kuomba: Wakati Yesu mambo yalimwenda vibaya, alimuomba baba, je umefanya nini? Watu walipokuwa walimshutumu na kumlaumu siku ya Ijumaa Kuu Takatifu, wakipiga kelele asulibiwe, Yeye alibaki kimya, kwani alikuwa na huruma ya watu wale walio danyanywa na wenye nguvu ya fedha, ya madaraka … lakini Yeye alikuwa kimya na kusali.

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anabainisha: “ katika hali hiyo, Mchungaji wakati wa kipindi kigumu, katika kipindi ambacho shetani anaingilia kati, mahali ambapo mchungaji anashutumiwa, lakini kwa kushutumiwa na Washitaki Wakuu, ambao ni kwa njia ya watu wengi, wenye nguvu wengi”, ina maana “mchungaji  anateseka, anatoa maisha na kusali. Yesu alisali”. “Na sala hiyo limpeleka hata msalabani akiwa na nguvu; hata pale alikuwa na uwezo wa kukaribia na kuponya roho ya mwizi mkuu”.

Neema ile ile ya mamlaka kwa ajili ya wachungaji leo hii: Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha akitoa mwaliko wa kurudia kusoma somo la Injili ya Mkatifu Luka, katika  Haya ya VII, na  ili kuona mahali palipo na mamlaka ya Yesu. Na kwa maana hiyo ni kusali kwa kuomba neema ili “ wachungaji wote tuweze kuwa na mamlaka hayo; mamlaka ambayo ni neema ya Roho Mtakatifu”.

18 September 2018, 12:18
Soma yote >