Tafuta

Misa ya Papa katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican Misa ya Papa katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican  (� Vatican Media)

Katika moyo wa mtu,Roho wa Mungu na roho ya dunia zinapambana!

Katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, Papa Francisko wakati wa Misa tarehe 4 Septemba amekumbusha kuwa, ndani ya moyo wa binadamu kila siku roho mbili yaani, Roho wa Mungu na roho ya dunia zinapambana.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Moyo wa binadamu ni kama uwanja wa mapambano, mahali ambapo wanakabiliana wawili katika roho tofauti; moja ukiwa ile ya Mungu, ambayo inatupelekea katika kutenda matendo ya upendo na katika udugu, na  nyingine ni ile ya dunia, ambayo inatusukuma kulekea katika ubatili, kiburi, kujitosheleza na masengenyo. Huo ni ufafanuzi wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 4 Septemba 2018.

Baba Mtakatifu katika mahubiri yake ameanzia na tafakari ya Somo la Kwanza ambalo Mtakatifu Paulo anawawakabidhi wakorinto,ile njia ya kuwa na wazo la Kristo, njia ambayo ni mwendo unaotakiwa kujikabidhi kabisa katika Roho Mtakatifu. Ni Roho Mtakatifu kwa hakika anayetufanya kumtambua Yesu na kuwa na hisia kama za kwake zitokazo ndani ya moyo amethibithibitisha Papa Francisko!

Mapambano yasiyo ya mwisho kati ya wema na ubaya

Mtu anayejiaminisha nguvu zake, hawezi kutambua mambo ya Roho, Baba Mtakatifu anabainisha na kwamba, kuna aina mbili za Roho, kwa maana ya namna mbili ya kifikiria, kuhisi na kutenda.  Ni ile ambayo inakupeleka katika Roho ya Mungu na ile ambayo inakupeleka katika roho ya dunia.  Mara nyingi inatokea katika maisha yetu: kwani sisi wote tunazo aina mbili za roho kwa namna ya kusema. Roho wa Mungu  ambaye anakufanya ujikite katika matendo mema, kama vil upendo, udungu, kuabudu Mungu, kumjua Yesu na kufanya mambo mengi ya upendo, wakati huohuo na kusali.

Na roho mwingine wa dunia, ndiyo anayetupeleka kuelekea njia ya ubatili, ukiburi, kujitosheleza na kusengenya: hiyo ni njia nyingine fofauti na ya kwanza Baba Mtakatifu amesisitiza.  Akiendelea na ufafanuzi  anasema, katika moyo wetu, alisema Mtakatifu mmoja kwamba ni kama kambi ya mapambano, kambi ya vita mahali ambapo roho mbili zinapambana.

Kushinda vishawishi  kama Yesu

Katika maisha ya kikristo, kwa hakika ni lazima kupambana ili  kuacha nafasi ya Roho wa Mungu na kumfukuzia mbali Roho wa dunia,anashauri Baba Mtakatifu na kuendelea; na katika kujitafakari dhamiri, kila siku inasaidia kutambua vishawishi na kuweka wazi  kwa kuona kwa jinsi gani nguvu hizi zinapingana kati yao.

“Hili ni jambo rahisi kwa maana tunayo zawadi kubwa ambayo ni Roho wa Mungu lakini pia sisi ni wadhaifu na wadhambi, tunavyo vishawishi vya roho wa dunia. Katika mapambano ya kiroho na katika vita hivi vya kiroho ni lazima kuwa washindi kama Yesu amethibitisha!

Sisi sio wanyama bali ni Wana wa Mungu

Kila siku usiku, anongeza kutoa ushauri, kila mkristo anapaswa kufikiria siku ambayo anamalizia. ili kutazama na kuhakikisha kama imetokea hali ya ubatili na ukiburi au kama imejitokea ile hali ya kumuiga Mwana wa Mungu

Ni kutambua kipi kinatukia ndani ya moyo. Na iwapo hatufanyi hivyo na hatujuhi kipi kinatukia ndani ya moyo, Baba Mtakatifu anasema, si yeye anatoa jibu bali ni Biblia inasema kuwa, sisi ni kama wanyama wasio jua kitu, wanakwenda tu kwa hisia. Lakini sisi sio wanyama bali ni Wana wa Mungu, wabatizwa kwa Roho Mtakatifu. Kwa maana hiyo ni muhimu kujua  lipi kwa siku limetukia ndani ya moyo wetu. Na Bwana atufundishe kufanya siku zote tafakari ya dhamiri zetu daim!

04 September 2018, 14:06
Soma yote >