Cerca

Vatican News
Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (ANSA)

Askofu ahisi kuchaguliwa,kuwa karibu na watu na mtu wa sala!

Katika nyakati hizi utafikiri mashtaki makubwa yako kwa upande wa askofu ili kuwatufa kashfa. Maaskofu kwa maana hiyo lazima misingi ya kuwasaidia: wawe watu wa sala na unyenyekevu, wajue wamechaguliwa na kuwa karibu na watu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu awe ni mtu wa sala, ahisi kuchaguliwa na kuwa karibu na watu wake, ndiyo  mantiki tatu za Baba Mtakatifu alizojikita nazo kutazama sura ya Askofu, wakati wa mahubiri yake kwenye Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Mjini Vatican Tarehe 11 Septemba 2018.

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake, amesema katika nyakati hizi utafikiri mashtaki makubwa yako kwa upandde wa askofu ili kuwatufa kashfa. Maaskofu kwa hiyo, lazima wakumbuke dhana tatu msingi za kuwasaidia: kwanza nguvu zao zitokane na kuwa watu wa sala, kuwa na unyenyekevu na kwamba watambue  kuwa wamechaguliwa na Mungu na kubaki karibu na watu.  Amesisitiza hayo Papa kutokana na msukumo wa Injili ya Siku iliyosomwa kutoka kwa Mtakatifu Luka (Lk 6,12-19). Katika somo la liturujia Yesu kwa dhati anaonekana  kusali usiku mzima kabla ya kuchagua mitume kumi na mbili, kwa  maana hiyo ni maaskofu wa kwanza na hivyo alitelemka chini ya kilima na kukaa katikati ya watu ambao waliokuwa wanakuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao Baba Mtakatifru amethibitisha.

Semina kwa ajili ya maaskofu: Akisisitiza zaidi juu ya maaskofu amefikiria kufanya tafakari hii kuhusiana na Maaskofu kama Yesu alivyofanya kwa mara ya kwanza, hasa  katika mwanga ambao kwa  kipindi hiki mjini Roma, ipo semina inayoendelea ya maaskofu:  mojawapo ilikuwa ya usasishaji kwa maaskofu waliotimiza miaka 10 tangu kuchanguliwa  kuwa maaskofu, iliyo malizika kwa siki za hivi karibuni, na nyingine ambayo inawaunganisha maaskofu 74 ambao wanaongoza majimbo  ya maeneo ya kimisionari, katika semina iliyo andaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, unaendelea hadi tarehe 15 Septemba kadhalika semina nyingine kwa maaskofu kati ya 130-140 ambao wanajikita huduma yao katika Baraza la Kipapa la Maaskofu. Kwa namna hiyo ni maaskofu zaidi ya 200 wapya wanaofanya semina mbili sambamba.

Mtu wa sala: Dhana ya kwanza  ni ile ya kuwa mtu wa sala. Sala kwa hakika ni faraja ambayo askofu anaipata katika  kipindi kigum, anasisitiza Baba Mtakatifu na kwamba ni kutambua kuwa katika kipindi hicho Yesu anasali kwa ajili yangu, anasalia kwa ajili ya maaskofu wote.  Katika utambuzi huo maaskofu wanapata ile faraja na ile nguvu ambayo inampeleka kwa mara nyingine kusali kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wa Mungu. Hiyo ndiyo zoezi la kwanza ya kwamba Askofu awe mtu wa sala  na kuthibitisha hata Mtakatifu Petro:”, “Kwetu sisi sala ni Kutangaza Neno, na hasemi kwamba, “ kwetu sisi ni shirika la kuandaa mipango ya kichungaji , amesisitiza Baba Mtakatifu!

Mtu anahisi kuchaguliwa na ni mnyenyekevu:Tabia ya pili Papa Francisko anabainisha kuwa, Yesu alichagua mitume na askofu aliye mwaminifu anatambua kuwa hakujichagua yeye binafsi:Askofu anayempenda Yesusi mkweaji ambaye anakwenda mbele na wito wake tu, utafikiri ni mfanyakazi mwingineo, au labda anatazama uwezekano mwengine wa kwenda mbele au juu: hapana: Askofu anahisi kuchaguliwa na ndiyo udhati wa kuchaguliwa.  Huo unampelekea kuwa na mazungumzo na Bwana kwa kumweleza “ wewe umenichagua mimi aliye kitu bure  na mdhambi…”: na  askofu ni mnyenyekevu. Kwa maana yeye anahisi amechaguliwa na mbaye yuko chini ya mtazamo wa Yesu juu ya maisha yake na kumpatia nguvu.

Usibaki mbali na watu: Hatimaye, kama Yesu katika maelezo ya Injili ya siku, Askofu anatelemka katika maeneo ya chini ili kuwa na watu wake karibu na si kuwa mbali nao: Baba Mtakatifu amefafanua ya kuwa, Askofu  kamwe hakai mbali na watu, na ni asiye kuwa na tabia ambayo inafanya watu wawe mbali naye: Askofu anawagusa  na kuwaacha waty wamguswe. Haendi kutafuta kinga kwa wenye nguvu, au kutoka kwa wasomi: hapana. Labada watakuwa ni wasomi watakao mshutumu Askofu; Lakini Watu waaminifu  wanatabia  ya upendo kwa  maaskofu kwa maana  wao wana upako maalum, kwani  askofu katika wito wake  anaimarisha

Mshtaki Mkuu anataka kuwadharau watu: Mara nyingi Baba Mtakatifu amesisitizia juu ya nguvu ya Askofu na kwamba ni mtu wa sala, mtu ambaye anahisi kuchaguliwa na Mungu na mtu katikati ya watu. Na hiyo ni vema kukumbusha, hasa katika nyakati hizi ambazo zinaonekan kwamba mshiktakiwa mkubwa ameachiliwa na hivyo kuna maaskofu. “Ndiyo wapo kwani  wote tu wadhambi, sisi maaskofu” Baba Mtakatifu amesema, Mshiktaki mkubwa hutafuta kuoenesha dhambi  zinazo onekana ili aweze kutoa kashfa kwa watu.

Mshitaki mkuu kama yeye ambaye Mungu mwenyewe katika Kitabu cha Ayubu anasema kuwa: “anazunguka ulimwengu mzima ili apate wa kushitaki”.  Nguvu ya Askofu, dhidi ya mshtaki Mkuu ni sala  ambayo Yesu aliitoa yeye binafsi; unyenyekevu wa kuhisi umechaguliwa na kubaki karibu na watu wa Mungu, bila kwenda katika utajiri ambao huondoa upako huo. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amehimiza kusali leo kwa ajili ya maaskofu wetu: kwa ajili yake, kwa ajili ya hao waliokuwa mbele yao na kwa ajili ya maaskofu duniani.

12 September 2018, 09:46
Soma yote >