Tafuta

Watu watafuta hifadhi kufuatia kwa mapigano kushika kasi kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo,huko Goma. Watu watafuta hifadhi kufuatia kwa mapigano kushika kasi kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo,huko Goma. 

Wito kutoka CEI kwa DRC:vurugu zinatosha!Milioni moja ya dharura!

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia(CEI)kupitia taarifa kutoka Ofisi ya Kitafa kwa ajili ya Mawasiliano ya kijamii limetoa wito kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC)‘ili mauaji ya watu huko Goma na katika maeneo mengine yaliyogubiwa na vurugu yakome.Tunaeleza ukaribu wetu kwa wakazi wa eneo hilo na wale walio nchini ambao wamejitolea kukabiliana na janga la kibinadamu ambalo halijawahi kushuhudiwa.’

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Tunazindua ombi letu la dhati kukomesha mauaji huko Goma na maeneo mengine ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaliyokumbwa na ghasia: inatosha! Ndivyo taarifa kutoka Ofisi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu wa Italia(CEI) tarehe 3 Februari 2025 imechapisha Ujumbe wa Baraza hilo kuhusiana na vurugu katika taifa la Bara la Afrika. Katika taarifa hiyo CEI inabainisha kuwa “Kwa mawasiliano ya karibu na Makanisa mahalia na wamisionari waliopo katika eneo hili, tunapokea habari za kila siku na picha za mauaji, ukeketaji, uharibifu na kuhama kwa watu wengi, ambayo hufanyika katika ukimya wa karibu wa vyombo vya habari.”

Baraza la Maaskofu Italia wanasisitiza kuwa “Mauaji ambayo yanadai waathriwa zaidi kati ya raia, bila kuacha watoto, hata watoto wachanga, wanawake na watu wasio na ulinzi. Hatuwezi kukaa kimya mbele ya mauaji haya, maangamizi ya ubinadamu. Tunaeleza ukaribu wetu kwa wakazi wa eneo hilo na wale walio nchini ambao wamejitolea kukabiliana na janga la kibinadamu ambalo halijawahi kushuhudiwa.” Kwa njia hiyo “Hebu tufanye maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kuwa yetu ambaye siku ya Jumatano tarehe 29 Januari, mwishoni mwa katekesi yake, alihimiza " pande zote zinazozozana zijitolee katika kukomesha uhasama na kulinda raia wa Goma, na maeneo mengine yaliyoathiriwa na operesheni za kijeshi” na kutoa wito kwa “mamlaka mahalia na jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi kubwa kutatua hali ya migogoro kwa njia za amani.”

Maaskofu wa Italia kadhalika wanasema kuwa “Kama Kanisa nchini Italia, tumekuwepo nchini kwa miaka mingi na wafanyakazi na wamisionari na hatuachi kusimama karibu na idadi ya watu na Kanisa la mahali, ambalo linaendelea kuwa shabaha ya vurugu na mashambulizi. Tangu 1991, Baraza la Maaskofu wa Italia limeunga mkono uingiliaji kati katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa euro milioni 136. Kupitia Huduma ya Afya za Misaada kwa Maendeleo ya Watu na shukrani kwa fedha za Mfuko wa ‘ 8xmille, msaada wa Euro 1,236 zilifadhiliwa. Hii ni miradi ya kukabiliana na dharura, kama vile, kwa mfano, kwa waliokimbia makazi yao huko Goma, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika sekta mbalimbali.”


Kwa kuhitimisha Maaskofu wa Italia wanasema kuwa “Ili kushughulikia dharura hii zaidi, Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia (CEI)liliamua kutenga euro milioni moja kutoka katika Mfuko wa fedha za 8xmille ambazo wananchi hutenga kwa Kanisa Katoliki. “Ahadi yetu ya kukuza hadhi na mustakabali wa amani haitashindwa.”

Maaskofu wa Italia watoa wito Congo na msaada

 

03 Februari 2025, 13:06