Martinelli:Kati ya Emirates,Oman na Yemen,Makanisa ya Wahamiaji yanaungana katika Utofauti
Na Joseph Tulloch – Abu Dhabi.
Makanisa yalikuwa yamejaa, imani ilionekana kama nguvu ya uzima na sio tu kama thamani ya ziada. Ushuhuda unaotoka kwa Askofu Paolo Martinelli, Balozi wa Vatican Kusini mwa Arabia, aliyepo Abu Dhabi kwa ajili ya utoaji wa Tuzo ya Zayed la Udugu wa Kibinadamu, ni ile ya jumuiya ya kikanisa hai na ya makabila mbalimbali kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman na Yemen, yenye waamini kutoka zaidi ya nchi mia moja, wenye uwezo wa kuishi kwa kina uzoefu wa umoja katika utofauti.
Mazingira magumu na tofauti
Akihojiwa na vyombo vya habari vya Vatican na mwandishi wetu Askofu Mkuu Martinelli alisisitiza miktadha tofauti sana ambayo inaitwa kufanyia kazi. Hali ile ngumu sana ya Yemen, iliyochoshwa na miaka kumi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo wamesalia Wakristo wachache, lakini jumuiya ya kikanisa inaungwa mkono na uwepo wa watawa wa Mama Teresa wa Calcutta, ambao wanafanya kazi kubwa ya upendo. Kisha jumuiya ya wahamiaji kabisa ya Oman na ile kubwa zaidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Lugha tofauti, tamaduni, mila na desturi za kiroho, lakini sherehe za Kikristo huhisiwa sana kiasi kwamba inakuwa vigumu kuwakaribisha waamini wote katika parokia tisa zinazoenea katika eneo lote, ushiriki wa dhati katika katekisimu na ushiriki sawa wa dhati wa wazazi, ambao wanatamani sana kuwasilisha na kurithisha imani kwa watoto wao. Wahamiaji, na jumuiya za kikanisa, kwa hiyo, ambapo imani inasaidia watu katika safari zao za kila siku, kuwakaribisha wale ambao wameacha kila kitu nyuma katika nchi yao ya asili. Unyenyekevu, lakini pia uvumilivu, ni tunu za wale wanaoshiriki katika maisha ya Kanisa mahalia kuwa mashahidi wa kuaminika wa Injili katikati ya jamii hii.
Kujuana katika magumu
Tukigeukia matukio ya sasa, Askofu Martinelli alikumbuka sherehe za miaka sita tangu kusainiwa, kwa Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa ajili ya Amani Ulimwengini na Kuishi Pamoja, mnamo tarehe 4 Februari 2019 kati ya Papa Francisko na Imamu Mkuu wa Al-Azhar, Muḥammad, al-Tayyeb. Hati ya uhusiano unaokua, ambao mapokezi yake yamejumuishwa katika Nyumba ya Familia ya Ibrahim, yaani jumba la kidini linalojumuisha Kanisa katoliki, lililotolewa kwa Papa Francisko na Rais wa Falme za Kiarabu, msikiti na sinagogi. Pia ni kituo cha mikutano ya kiekumene inayosaidia kutembea pamoja, kujua, kuheshimu na kuthamini mapokeo mbalimbali ya kidini, alielezea. Kuishi Hati kwa bidii kwa hivyo sio jambo la kufikirika tu bali ni kitu halisi, kukabiliana na shida pamoja na kuishi uzuri wa safari ya pamoja.
Maono ya Ulimwengu ya Zayed
Mfumo ambao Tuzo ya Zayed ya Udugu wa Kibinadamu inafaa, iliyozaliwa mnamo 2019 kufuatia kutiwa saini kwa Hati wakati wa safari ya kitume ya Papa kwenda Falme za Kiarabu. Tuzo ambayo mwaka huu 2025 ilikwenda kwa Shirika lisilo la Kiserikali la World Central Kitchen, kwa kazi yake ya kutoa msaada wa chakula kwa jamii zilizoathiriwa na majanga ya kibinadamu; kwa Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley kwa hatua yake madhubuti juu ya mabadiliko ya hali ya tabianchi na mvumbuzi mwenye umri wa miaka 15 kutoka Ethiopia na Marekani Heman Bekele. Tuzo hiyo imechochewa na Zayed bin Sultan Al Nahyan, anayechukuliwa kuwa baba wa taifa, mwenye uwezo wa kuhamasisha uumbaji wa Umoja wa Falme za Kiarabu. Mtu wa kuvutia sana, mwenye maono ya nia na maslahi yanayokutana na anayeweza kuunganisha falme saba na kuwa na mwanzo wa nia ya kuunda taifa la wazi, la kiutamaduni, ambalo wahamiaji wengi, wabeba tamaduni na dini, wanakaribishwa bila utofauti.