Paris:wito wa viongozi wa dini:tafuteni njia za amani hata katika giza la vita
Francesca Sabatinelli na Angella Rwezaula – Vatican
Kufanya kazi kwa ajili ya mabadiliko ya kweli, katika kutafuta njia za amani ambazo zipo hata kama zimefichika katika giza la vita, ndiyo wito na sala ya amani iliyoinuliwa katika Uwanja wa Notre-Dame(Mama Yetu)Kanisa ambalo hivi karibu litazinduliwa tena, baada ya kukarabatiwa kwa sababu ya kuungua vikali kwa moto mnamo tarehe 15 Aprili 2019. Kwa njia hiyo ni eneo lililochaguliwa kuwa kiini cha maombi kuelekea viongozi wa kidini, wahusika wa kisiasa, mabwana wa vita, watu wote, ili kwamba wajibidishe kila mmoja kwa ajili ya kukumboa dunia katika moto wa vita na kujenga upya dunia hiyo iweze kuwa ya amani na haki zaidi.
Kujiuzulu mbele kukabiliwa na vita
Mkutano wa kimataifa huko Paris nchini Ufaransa ulianza tarehe 22 na kuhitimishwa tarehe 24 Septemba 2024, kwa kuhamasishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, kwa ushirikiano na Jimbo Kuu la Mji Mkuu wa kifaransa, kwa kuongozwa na mada: “Kufikiria amani”imewaalika wanawake na wanaume wa dini tofauti, ambao wameunganika na ubinadamu wasomi na watu wengi kwa kubeba katika moyo wa dunia kwa watu wengi kwa ajili ya vita vinanavyondelea. Katika siku za mkutano na mazungumza, watu hao hao walijaribu kwa pamoja kufikiria wakati ujao wa amani katika ulimwengu huu, na wazo lililoelekezwa kwa wale ambao wamegubikwa na vita, kwa wale ambao wamekumbwa na ugaidi. Kwa bahati mbaya ni malalamiko makubwa kwani kuna kuenea kwa kujiuzulu katika uso wa migogoro ya wazi, ambayo inahatarisha kuzorota kwa vita kubwa zaidi na hii pia kwa sababu katika ulimwengu, ikiwa ni pamoja na Ulaya, kumbukumbu ya kutisha ya vita, urithi wa dunia mbili, kwa migogoro ya karne ya ishirini. Urithi huo unaoonesha jinsi ambavyo amani pekee ni mbadala wa kibinadamu na wa haki!”
Hatari kwa vizazi vijana
Swali ambalo viongozi wa dini za ulimwengu waliuliza zaidi ya yote ni juu ya aina gani ya jamii ambayo inapitishwa kwa vizazi vichanga, inayojulikana na ugaidi na vurugu? "Hofu ni kwamba ukarabati wa vita kama chombo cha kutatua migogoro au kudai maslahi ya mtu inaweza kuhamishiwa kwa watoto. Kwa hiyo dini zinabainisha kuwa zinafahamu kwamba ulimwengu unapata maisha yake katika amani na kwamba vita kwa jina la Mungu ni kufuru." Zaidi ya hayo, licha ya kuwa na nguvu dhaifu na unyenyekevu, na licha ya kutokuwa na uwezo wa kutegemea nguvu ya kijeshi au kiuchumi, dini zinajua kwamba ni kutokana na mazungumzo kwamba amani inaweza kufikiriwa, ambayo inabaki kuwa hali bora zaidi ya kuwepo kwa watu, wa kipekee mwanadamu wa kweli na anayestahili."
Maandamano ya kupinga chuki
Kilichosikika mjini Paris katika siku za hivi karibuni katika mkutano ni kilio cha upinzani mbele ya ghasia na vita, ambavyo si mustakabali wala hatima ya ubinadamu na ambao waathiriwa, wakati mwingi wasio na hatia, walikumbukwa kwenye jukwaa wakati wa kufunga tukio na rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Bwana Marco Impagliazzo. Katika hotuba yake, Impagliazzo alikuwa msemaji wa maandamano ya kidini dhidi ya chuki na wageni, kwa nia ya kuishi kwa amani kwa wanaume na wanawake wengi. Kile ambacho nyakati ngumu za historia zinaomba, alionesha, ni umoja wa lazima kuona upeo unaoshinda chuki, vurugu na vita na kukusanya urithi wa vita ambavyo kamwe visitendeke tena Ulaya vya nyuma ambavyo walitafuta njia za amani wakati na baada ya janga la Vita vya Kidunia. Ombi lilikuwa kujibu wasiwasi wa amani ya kawaida kwa wote, na kutoka nje ya nafasi zilizozuiliwa, kwa sababu hata kama kuna vita, ni muhimu kufikiria juu ya amani ya kesho na ni hekima.
Ahadi ya kujenga mahusiano ya kidugu
Huko Paris, Askofu Mkuu Laurent Ulrich wa jiji hilo alikumbuka, jinisi ambavyo majuma machache yaliyopita yaliwekwa alama na Michezo ya Olimpiki na Paralympic na kuonesha fadhila za mashindano ya michezo, ambayo husukuma mtu kujishinda na ambayo hupitisha hamu ya kukutana kati ya watu. Paris hiyo hiyo, ambayo katika historia yote imepitia mazungumzo ambayo yamesababisha makubaliano ya amani na heshima kwa kila mtu, kwa hiyo imepitia Mkutano wa Kimataifa wa Amani, ambao pia unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 38 ya Siku ya Assisi mwaka 1986, pamoja na kujitolea upya kwa dini, kujenga mahusiano ya uchangamfu, ya kindugu na rahisi."