Tafuta

Mama Maria wa Rozari:"Bikira Maria,Mama wa matumaini,ijalie zawadi ya amani Nchi Takatifu iliyokuzaa wewe na dunia nzima." Mama Maria wa Rozari:"Bikira Maria,Mama wa matumaini,ijalie zawadi ya amani Nchi Takatifu iliyokuzaa wewe na dunia nzima." 

Kard.Pizzaballa:wito,Oktoba 7 siku ya sala,kufunga&kuomba amani kwa Nchi Takatifu

Kardinali Pizzaballa,Patriaki wa Yerusalemu,ameomba kusali ili kuomba amani tarehe 7 Oktoba 2024."Mungu Mwenyezi Mtukufu,mikononi mwako, yako matumaini ya watu na haki za kila watu:wasaidie kwa hekima yako wale wanaotuongoza,ili kwa msaada wako wawe na hisia kwa mateso ya maskini na waendeleze manufaa ya wote na amani ya kudumu katika eneo letu na duniani kote."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ya SALA, TOBA na KUFUNGA ili kuomba ZAWADI ya AMANI katika NCHI TAKATIFU, mara baada ya mwaka mmoja wa mzozo kati ya Israel na Palestina kutawala. Mpango huo ulizinduliwa na Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Yerusalemu ya Kilatini, Nchi Takatifu  kupitia barua aliyoandika kwa ajili ya Jimbo zima la Upatriaki wa  Kilatini wa Yerusalemu. Kardinali Pizzaballa aliandika kwamba: "Mwezi Oktoba unakaribia na pamoja na ufahamu kwamba kwa mwaka sasa Nchi Takatifu, na sio hivyo tu, imetumbukizwa katika wimbi la vurugu na chuki ambayo haijawahi kuonekana au kupatikana hapo awali. Katika miezi hii kumi na mbili tumeshuhudia majanga ambayo, kutokana na ukubwa wake na athari zake, yameharibu sana dhamiri zetu na hisia zetu za ubinadamu."Akiendelea kuandika  Patriaki huyo anakumbuka kuwa "kwa mara nyingine tena ni  serikali na wale ambao wana jukumu kubwa la kufanya maamuzi kujitolea kwa haki na kuheshimu haki ya kila mtu ya uhuru, utu na amani."

Wito wa siku ya maombi 7Oktoba

Kardinali Pizzaballa kwa njia hiyo anatoa Wito kwa Taifa zima kuwa: “Ninawaalika, kwa hiyo, katika siku ya maombi, kufunga na toba, tarehe 7 Oktoba ijayo, tarehe ambayo imekuwa ishara ya janga tulilolipata. Mwezi wa Oktoba pia ni mwezi wa Maria na tarehe 7 Oktoba 7 tunaadhimisha kumbukumbu ya Bikira Maria Malkia wa Rozari. Kila mmoja, akiwa na rozari au kwa namna anavyoona inafaa, binafsi lakini bora zaidi katika jumuiya, kupata muda wa kusimama na kusali, na kumpelekea ‘Baba mwenye huruma na Mungu wa faraja yote’ (2Kor 1:3)hamu ya amani na upatanisho."Kwa kufanya hivyo, Kardinali Pierbattista ameambatanisha sala hiyo iliyotungwa kwa ajili ya siku hiyo kwamba inaweza kutumika kwa uhuru.

Ifuatayo ni sala hiyo kwa Mungu kuomba amani:

Bwana Mungu wetu, Baba wa Bwana Yesu Kristo na Baba wa wanadamu wote, ambaye kwa msalaba wa Mwanao na kwa zawadi ya maisha yake mwenyewe kwa gharama kubwa alitaka kuharibu ukuta wa uadui na uadui unaotenganisha watu na kutufanya sisi kuwa adui: tupelekee kipaji cha Roho Mtakatifu mioyoni mwetu, ili atusafishe na kila hisia ya jeuri, chuki na kisasi; utuangazie kuelewa hadhi isiyozuilika ya kila mwanadamu, na ututie moto hadi kumezwa na ulimwengu wenye amani na kupatanishwa katika ukweli na haki, katika upendo na uhuru. Mungu Mwenyezi Mtukufu, mikononi mwako, yako matumaini ya watu na haki za kila watu: wasaidie kwa hekima yako wale wanaotuongoza, ili kwa msaada wako wawe na hisia kwa mateso ya maskini na wale wanaoteseka, matokeo ya vurugu na vita; waendeleze manufaa ya wote na amani ya kudumu katika eneo letu na duniani kote. Bikira Maria, Mama wa matumaini, ijalie zawadi ya amani Nchi Takatifu iliyokuzaa wewe na dunia nzima. Amina.

27 September 2024, 12:57