Nicaragua,Gambera wa Seminari ya Matagalpa amewekwa gerezani
Vatican News
Padre mwingine alikamatwa Jumatatu tarehe 5 Agosti katika Jimbo Katoliki la Matagalpa, nchini Nicaragua. Huyo ni Gambe wa Seminari Kuu yaya Falasafa ya Mtakatifu Aloys Gonzaga na paroko wa Kanisa la Mtakatifu María de Guadalupe, katika kitongoji cha Guanuca cha Matagalpa. Kwa njia hiyo Padre Jarvin Tórrez, alipelekwa gerezani, kulingana na kile ambacho waamini waliambia vyombo vya habari.
Kukamatwa kwa padre huyo kulishutumiwa na wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini huo, yaliyonukuliwa na gazeti la kitaifa la “La prensa,” ambalo pia ilifahamika kuwa Lesbia Rayo Balmaceda, mhudhumu wa parokia ya Sébaco Mlei pia yuko kizuizini.
Mapadre tayari kumi na watatu wamefungwa katika muda wa Juma moja huko Nicaragua. Wao kwa kiasi kikubwa ni wa Jimbo la Matagalpa, ambapo Askofu wao, Rolando Álvarez, tayari alifukuzwa mbamo tarehe 14 Januari 2024. Mnamo Machi 2023, Jamhuri ya Nicaragua iliomba Vatican kufunga ofisi zao za kidiplomasia, bila kuvunjia kabisa uhusiano wao.