Equipes Notre-Dame:“Tutembee pamoja na Kanisa kwa mtindo wa sinodi”
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Takriban washiriki elfu nane, kutoka zaidi ya nchi 86 ziliwakilishwa na Brazil, Ufaransa, kutoka Italia hadi Botswana, na kupitia New Zealand nyingine. Bila kusahau watu 400 wa kujitolea, ambao muhimu katika harakati ya kuvutia. Mkutano wa Kimataifa wa XIII wa Equipes Notre-Dame, ulianza tangu tarehe 15 Julai na kumalizi Jumamosi 20 Julai 2024 ulifanyika Turino, mji wa mlezi wa Sanda na mama wa watakatifu wa kijamii, kama vile Mtakatifu Don Bosco, Giuseppe Cottolengo na Mwenyeheri Giuseppe Allamano ambaye atatangazwa kuwa mtakatifu mnamo tarehe 20 Oktoba 2024. Chaguo la mji mkuu wa Piemonte kwa hakika si la kubahatisha kama ilivyo fafanuliwa na wahusika wa Haraka hiyo wenyewe kwa neno hilo la Kifaransa wana fursa ya kurejea ratiba za kiroho na kidini ambazo zilizua maisha hayo ya ajabu ya utakatifu.
Kusikiliza na kushiriki
Mada ya toleo la mwaka 2024 ilizama katika roho ya kimisionari na ilirudia Injili ya Luka ambayo inawaambia wanafunzi wa Emau: Twendeni kwa moyo unaowaka. Ushauri ulioonesha katika siku zote tano za kazi kwa kutafakari, maadhimisho ya Ekaristi, sala za pamoja, mikutano, makongamano na maonesho. “Mbali na haya yote, pia kulikuwa na vipindi vya kusikiliza: shuhuda za kaka na dada wanaoishi katika mataifa ambayo ni magumu kuishi kwa sababu ya umaskini na vita,” Alieleza Mercedes Perez ambaye pamoja na mumewe Alberto waliteuliwa kama Wakuu wa ulimwengu ujao wa Equipes Notre-Dame. Familia ya Perez Wahispania asili yao ni kutoka Valencia, ni sehemu ya harakati ya walei ya kiroho ya ndoa waliozaliwa Paris mwishoni mwa miaka ya 1930 kutokana na angavu na kujitolea kwa Padre Hanri Caffaril ambaye aliitikia wito wa baadhi ya wanandoa ambao walitaka kupata kikamilifu sakramenti ya ndoa.
Wapo katika nchi 93
Albero alikumbusha kuwa “Tangu wakati huo, hasa tangu 1947, mwaka ambao hati ya mwanzilishi ilizinduliwa harakati imeendelea, kwanza kufikia nchi zingine za Ulaya na kisha kuvuka Bahari ya Atlantiki na hata kufika Brazili. Leo tupo katika nchi 93.” Hali ya kiroho ya ndoa ambayo inawahusu wanandoa wanaofuata harakati - washiriki wa timu, kwa kweli - ni "njia ya sala inayofanywa kama wanandoa ambayo inatusukuma kutoka nje ili kukutana na wengine, ikiwa ni pamoja na washiriki wa timu za mitaa ambayo sisi ni washiriki na ambao kwa kawaida wanajumuisha wanandoa 5 au 6 pamoja na Padre ambaye huwasindikiza nao kama mshauri wa kiroho,” aliongeza Alberto.