Tafuta

KANISA KUU LA  NIAMEY, NCHINI NIGER KANISA KUU LA NIAMEY, NCHINI NIGER 

Niger,Siku za Vijana Kijimbo-Niamey:Vikao vilikuwa vizuri sana kwa kila mtu

Vijana wa Jimbo Kuu la Niamey wamejifunza juu ya jukumu la msingi kwao katika Jumuiya za Kikristo kwa ajili ya jimbo lao.Ni katika muktadha wa Siku za vijana zilizofanyika hivi karibuni kuanzia tarehe 24-26 Novemba 2023 katika Chuo cha Maria huko Niamey,Niger.Vijana zaidi ya mianane waliudhuria mafunzo hayo.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Vijana wana jukumu muhimu katika jumuiya ya Kikristo ya Dosso, kama katika jumuiya zote ambako kuna vijana, alisema hayo Padre Rafael Casamayor mmisionari wakati akizungumza na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisonari Fides kuhisiana na afla ya Siku za Vijana kijimbo zilizowaleta pamoja karibu vijana mia nne kutoka utume mbalimbali wa mji mkuu wa Niger kuanzia tarehe 24 hadi 26 Novemba 2023 katika Chuo cha Maria huko Niamey.

Matatizo katika ukanda wa Sahel

Kwa mujibu mmisionari wa Shirika la Utume wa  Afrika katika maelezo yake alibainisha kuwa: “Takriban vijana thelathini walifika kutoka parokia ya Dosso ambao walishiriki nyakati za furaha, walivunja vizuizi, hofu na haya. Katika jamii ya Kiafrika ya nchi hizi za ukanda wa Sahel, mabadiliko muhimu yanafanyika kutokana na shinikizo za  itikadi  kali za kiislamu, ghasia ambazo zimejidhihirisha katika makundi mengi ya wanaharakati, na kukataliwa kunakojidhihirisha kila mara katika ulimwengu wa Magharibi ambao umeona ukoloni na mapinduzi mwengi.” Alisisitiza Mmisionari huyo.

Watoto na vijana kutoka Benin walifika

Padre Casamayor kwa hiyo alisema: “Na ni katika hali hii ya kutokuwa na utulivu ambapo Siku za Vijana kijimbo ziliitishwa na vijana waliweza kufika huku wakihusisha tamaduni nyingine na asili tofauti. Ilikuwa mikutano ya mafunzo, kubadilishana maoni, kujitolea kwa ajili ya utunzaji wa nyumba ya wote, mazungumzo, uhuishaji na maombi. Watoto na vijana wengi kutoka Benin walikuja ili kujifunza  uuguzi na afya huko Dosso.

Vikao vimeweza kuwa muhimu kwa kila mtu

Akiendelea kufafanya alisema: “Katika jumuiya yetu ya Kikatoliki, vikundi vya Caritas, vikundi vya kitume, vikundi vya utambuzi, shule ya sala, masomo ya lugha ya Songhay-Zarma na historia yake vimeundwa. Pamoja na shughuli za michezo na muziki ambazo hupangwa kulingana na uwezekano na wakati unaopatikana.” Kwa kuhitimisha katika mazungumzo na Fides alisema  kuwa anafikiri kwamba: “vikao hivi vimekuwa muhimu sana kwa kila mtu.”

15 December 2023, 14:19