Nigeria:Jubilei ya CEPACS imefunguliwa kwa Misa Takatifu na ya kupendeza
Na Paul Samasumo, – Vatican.
Maaskofu Katoliki barani Afrika wakiwa na waamini wa Lagos Nchini Nigeria wamekusanyika katika Kanisa Kuu Katoliki la Msalaba Mtakatifu, pengine jambo la mwisho walilotarajia lilikuwa ni kukaribishwa na Askofu Emmanuel Badejo akiwaongoza kwa muda mfupi kuimba na kwaya ya wimbo wa kipekee wa Michael Jackson, “Heal the World” yaani, ponye Ulimwengu," jambo la kushangaza zaidi ni kwamba kwaya na mkusanyiko mzima wa Lagos ulionekana kujua maandishi ya wimbo huo wa Michael Jackson kwa moyo.
Katikati ya mahubiri ya Dominika tarehe 19 Novemba 2023, ya Askofu Emmanuel Adetoyese Badejo, wa Jimbo katoliki la Oyo nchini Nigeria aliingilia kwa hiari katika wimbo wa Michael Jackson, uitwao Heal the World. Hii ilikuwa katika Misa ya ufunguzi wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya Kamati ya Mawasiliano ya Kijamii ya Maaskofu wa bara la Afrika (CEPACS).
Katika mahubiri yake Askofu Badejo alisema inapoonekana kama zawadi, mawasiliano yanaweza kuleta ushirika, maelewano na uponyaji katika jamii, na Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi anapendekeza Msamaria Mwema kuwa mfano wa kuigwa na Wakristo ili kuuponya ulimwengu na jamii zetu. Mfano huo, ni mfano mzuri wa kuwasikiliza wengine-hata kama hawasemi-na unatutia moyo tusimwache mtu yeyote nyuma. Kumwiga Msamaria Mwema popote tunapojikuta kunaweza kubadili jinsi tunavyomwona mgeni, jinsi tunavyowaona maskini, jinsi tunavyowatendea waliotengwa, na jinsi tunavyowatendea wasiostahili hata usikivu wetu. Unaweza kutusaidia kutengeneza ulimwengu wenye haki na akili timamu kwa kila mtu…Hata baadhi ya waimbaji wetu wazuri wanatambua hilo,” alisema Askofu Badejo alipokuwa akiingia katika kwaya ya Michael Jackson. Na kwa hiyo kusanyiko liliimba pamoja: “Kuna njia za kufika huko, Ikiwa unajali vya kutosha kwa walio hai. Tengeneza nafasi kidogo, Fanya mahali pazuri zaidi .... Uponye Ulimwengu…”
Askofu Badejo aliendelea, katika mahubiri yake kwamba, “Hii ni Misa ya shukrani kwa Mungu kwa miaka hii 50 ya CEPACS pamoja na misukosuko, mafanikio na mapungufu yake tangu kuanzishwa kwake Ibadan … ninajua kuwa kama Mwenyekiti na Rais wa CEPACS, ninasimama mabegani mwa watu wengi waliojibidiisha sana katika Kanisa ili kukuza na kueneza Habari Njema ya Injili ya Yesu Kristo kati ya watu kwa kila njia,” Askofu wa Jimbo la Oyo aliwaambia waamini wa Lagos na wajumbe wa CEPACS.
Mkutano wa siku mbili wa CEPACS unamalizika Jumanne tarehe 21 Novemba 2023. Maaskofu kadhaa na wataalam wa kimataifa wa vyombo vya habari vya Kanisa wanatarajiwa kuwasilisha mada zao zinazokusudiwa kujitolea tena kwa utume wa vyombo vya habari vya Kanisa barani Afrika.
Wimbo wa Michael Jackson
Wimbo wa "Heal the World" wa Michael Jackson ni wimbo ambao mwimbaji huyo alitunga na kurekodi mnamo mwaka 1991 na kutolewa mnamo 1992. Wimbo huo unahusu matakwa ya Jackson kwa ubinadamu kufanya ulimwengu kuwa mahali bora. Baadaye angesema kwamba "Ponya Ulimwengu"ndio wimbo ambao alijivunia kuutunga. Wimbo huo ulipigwa na kuchezwa kwenye mazishi yake mnamo 2009.