Mgogoro kati ya Israel na Gaza hauna mfano Mgogoro kati ya Israel na Gaza hauna mfano  (AFP or licensors)

Mkuu wa Shirika la Kaburi Takatifu:Ni vigumu kupeleka msaada huko Gaza

Leonardo Visconti di Modrone anasimulia uhamasishaji wa taasisi ya kikanisa katika kupeleka misaada kwa watu waliochoka na fedha:‘Fedha zipo lakini ni ngumu kuzifikisha.Wakati huohuo,Wakristo wamekusanyika kaskazini mwa jiji,wakitumaini kutotoweka kabisa.’

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika vita ambavyo vimegawanyika vipande vipande duniani, hali halisi siyo shwari kuanzia kaskazini, kusini, mashariki na magharibi, kila kona kuna vita! Na sasa tangu tarehe 7 Oktoba 2023  kumezuka vita kati ya Israel na Palestina ambapo ni maelfu ya binadamu yamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wengine kuwa mateka. Ni katika mkutadha huo “Mahali pasipofikika ambapo ni vigumu kupata mahitaji ya kimsingi ni hali ya kushangaza ya Gaza inayosimuliwa na balozi Leonardo Visconti di Modrone, Mkuu wa Shirika la Kaburi Takatifu. Yeye anayajua vyema matukio ya Nchi Takatifu kwa sababu moja ya kazi kuu ya taasisi ya kikanisa ambalo yeye mwenyewe ni Mkuu wa sehemu yake ni kulisaidia Kanisa Katoliki katika sehemu hiyo yenye mateso ya dunia, hasa kwa kuunga mkono Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu.

Watu 500 wamekimbilia Parokia ya Familia Takatifu na 400 ya Kiorthodox

Katika maelezo yake Mkuu huyo wa Shirika anabainisha kuwa "Katika jiji  ​​haiwezekani kupeleka chakula, maji au madawa". Hi ni janga la kibinadamu. Wakristo, wanapoweza, wakimbia.  Kwa mujibu wa Visconti di Modrone alisema kwamba wengi wamekusanyika kaskazini mwa Gaza,  karibu watu 500 katika parokia ya Kilatini ya Familia Takatifu,  na wengine 400 katika parokia ya Kiorthodox. Walifanya hivyo kwa sababu huko kusini hakuna taasisi za Kikristo zilizo tayari kuwakaribisha na utoaji wa misaada ya kibinadamu ni mgumu zaidi." Miongoni mwa Wakristo hawa pia kuna wazee ishirini, takriban watoto sitini, ambao baadhi yao ni walemavu na hawawezi kuhama.

Kusambaza misaada, shida halisi

Kuna sababu kwa nini Wakristo walikimbilia kusini. "Ni chaguo ambalo linajibu hamu ya kuweka uwepo wa Wakristo hai huko Gaza, kufikiria juu ya siku zijazo," alisema Mkuu huyo ambaye pia hakusita kuakisi kitendawili cha kimsingi katika utaratibu wa misaada kwa watu: "Kiukweli hakuna shida katika kutafuta pesa, ipo na inaweza pia kuongezeka. Ugumu halisi ni usambazaji wa bidhaa hizo kwa idadi ya watu," kuweza kuwafikia.

Katika mawasiliano ya karibu na Upatriaki

Shirika la Kaburi Takatifu  Yerusalemu  halikati tamaa, halikujiruhusu kutawaliwa na woga. Mara moja liliwachangamotisha  wanachama wake wote, hasa wale wa  Marekani ambao ni karibu nusu ya jumla  yao. Mkuu huyo alibainisha kuwa “Mtandao wa mshikamano ulianza kufanya kazi mara moja” pia “kwa Tume yetu ya Nchi Takatifu ambayo inawasiliana kila siku na utawala wa Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu. Ili kufidia gharama tutatumia mfuko wa misaada ya kibinadamu, moja ya fedha kuu na kubwa katika bajeti yetu." Na ikiwa itakuwa lazima, aina zingine za ukusanyaji pia zitahitajika kufanywa,” alithibitisha.

Ugumu wa kufikia maeneo ya Gaza kusaidia watu

 

20 October 2023, 11:10