Ukraine:Ujumbe wa maaskofu wa Australia watembelea Lviv,Kiev,Bucha na Irpin
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Wawakilishi wa Kanisa la Australia kuanzia tarehe 8 hadi 11 Agosti 2023, walitembelea miji kadhaa ya Lviv, Kiev, Bucha na Irpin, nchini Ukraine, maeneo yaliyopata uharibifu wa kutisha na ukatili dhidi ya maisha ya binadamu. Wajumbe hao ni Askofu Mkuu Peter A. Comensoli wa Melbourne; Askofu Mkuu Julian Porteous wa Hobart, Askofu Karol Kulczycki wa Port Pirie, Padre Simon Cjuk, Mkuu wa Kanisa la Kigiriki-Katoliki la Kiukreni nchini Australia, na Annie Carrett, Kansela wa Jimbo kuu la Melbourne. Wakiwa huko, Ujumbe huo ulikutana na viongozi wa Kanisa, familia, askari na maafisa wa kiraia. Kutazama mkasa huu kwa mbali na kutoa msaada wa kifedha ni jambo moja, lakini ni muhimu kusikia na kushiriki sauti za wale walioathirika moja kwa moja,” alisema Askofu Mkuu Porteous.
Akiendelea Askofu Mkuu Porteous alisema alivyoguswa na ukaribu wa maaskofu na mapadre kwa watu wao. “Sio tu kwamba walikuwa na bidii katika kutoa msaada wa kimwili, lakini walikuwepo kichungaji na kiroho kati ya watu. Naye Askofu Mkuu Kulczycki alitoa pongezi kwa kazi iliyofanywa katika kituo cha ukarabati kisichovunjika cha Lviv, kilichojengwa na kufadhiliwa na ukarimu wa watu na mashirika kutoka pande zote za ulimwengu. “Vituo kama vile Visivyovunjika ni muhimu kwa kujenga upya maisha. Wanakaribisha watu waliojeruhiwa wa rika zote kwa kutoa huduma kutoka kwa upasuaji, upasuaji wa viungo bandia, ukarabati na, zaidi ya yote, usaidizi wa kisaikolojia na kijamii.
Kwa mkazo zaidi alibainisha kuwa "Mengi yamepotea na kuharibika. Maisha haya ya vijana na familia hizi changa zinahitaji kujifunza upya jinsi ya kuishi maisha ya kila siku.” Kwa mujibu wa ujumbe wao washiriki wa ziara hiyo walithibitisha kwamba “Ziara hiyo, ingawa fupi ni kujitolea kwa udugu wa Kanisa la Australia katika kuunga mkono watu wa Ukraine. Baada ya kurejea, maaskofu wanapanga kuunganisha uhusiano ulioanzishwa na kuwahimiza waamini huko Australia kuendelea kuwaweka wale wanaoteseka katika sala zao”.