Tafuta

Hospitali ya Mtakatifu Gemma Galgani huko Dodoma,Tanzania itasaidiwa na Baraza la Maaskofu Italia(CEI) katika ujenzi wa Wodi ya Mama wajawazito. Hospitali ya Mtakatifu Gemma Galgani huko Dodoma,Tanzania itasaidiwa na Baraza la Maaskofu Italia(CEI) katika ujenzi wa Wodi ya Mama wajawazito. 

Tanzania:Wodi ya wazazi itajengwa Hospitalini Mt.Gemma,Dodoma kwa msaada wa CEI

Wodi ya wazazi ya hospitali ya Mtakatifu Gemma mjini Dodoma Tanzania itapanuliwa kwa msaada wa Baraza la Maaskofu Italia(CEI) na Ushirikiano wa Mkoa wa Toscana Italia.Katika jengo jipya pia kutakuwa na wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati,(njiti)ambayo hadi sasa hakuna na watoto wanakimbizwa katika vituo vingine.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tarehe 7 na 8 Julai 2023, Kamati ya uingiliaji kati ya upendo kwa maendeleo ya watu ya Baraza la maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI)ilidhinisha miradi mipya 72 ambayo itatekelezwa katika bara la Afrika, Amerika ya Kusini, Asia na Ulaya Mashariki. Katika Mkutadha huo, shughuli hizo za usaidizi wa upendo zinaendelea na hivyo Baraza hilo litatoa msaada wa ujenzi wa Wodi ya wajawazito katika  hospitali ya Mtakatifu Gemma mjini Dodoma, Tanzania.  Hospitali ya Mtakatifu Gemma huko Dodoma, Tanzania, ilipojengwa kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya watoto 300/400 waliotarajiwa kuwapo  kwa mwaka, lakini  hadi leo hii ni  watoto 1700, na kuna siku ambazo pia kuna wanawake 10/15 wanaojifungua kwa wakati mmoja.

Ushirikiano wa CEI,Chuo Kikuu Katoliki,Mkoa wa Toscana na CMSR

Kwa hivyo wodi ya wajawazito haitoshi tena na  kwa njia hiyo Kituo cha Maendeleo ya Kuheshimiana cha Livorno, ambacho kimefuatilia miradi kila wakati katika eneo hilo, kimewasilisha na kupata msaada wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) ili kupanua jengo hilo. Taarifaha hizi zimetolewa katika Gazeti la Juma la Livorno (Livorno Week). Katika taarifa hiyo inabanisha kwamba mbani na Kituo cha Zana za Kimatibabu (Rehabilitation Instrumental Medical Center CMSR)  na watawa wa Mtakatifu Gemma huko Dodoma, washirika wa mpango  huo pia ni Hospitali Kuu ya Agostino Gemelli, Roma pamoja na Chuo Kikuu Katoliki, shukrani hasa kwa kufuatilia Msimamizi wa kikanisa wa Chuo Kikuu Katoliki, Askofu  Claudio Giuliodori na Mkoa wa Tuscana, Italia  ambao utachukua jukumu la  huduma ya kutuma vyombo vya  chumba cha upasuaji.

Wodi ya watoto Njiti itajengwa

Katika jengo jipya pia kutakuwa na wodi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, ambao  hadi sasa hawapo kwa sababu hakuna namna ya kuwasaidia kwani, ili  kuweza kupata vifaa vinavyofaa, wanapaswa kusafiri maili za barabara kufikia hospitali nyingine, na wakati huo bila kusafirishwa bila ambulensi, zaidi ya nusu yao watoto hufia  njiani. Kwa kujenga  wodi mpya wataweza kuhudumiwa mara moja. Aidha katika maelezo hayo, Gazeti libainisha kuwa “Upanuzi wa wodi ya wazazi imekuwa ndoto ya Sista Gemma Kitiku, ambaye alikuwa ni  rafiki mkubwa wa Jimbo la  Livorno nchini Italia na ambaye aliyefariki mnamo  Machi 2021, ambaye alifuatilia kwa karibu ujenzi wa hospitali hiyo na kupata fursa ya kuja kusomea taalumu ya matibabu  nchini Italia.

Wodi ya wajawazito katika Hospitali ya Mt.Gemma, Dodoma Tanzania.
24 August 2023, 16:24