Pakistan:Mshikamano na umakini kwa viongozi wa kiislamu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika tukio la vurugu dhidi ya Wakristo huko Jaranwala, eneo la Punjab ya Pakistan ambapo nyumba na makanisa yalichomwa moto hivi karibuni jambo lisilofikirika hadi miaka michache iliyopita lilitokea, ambalo linashuhudia matunda mazuri yanayotolewa na kazi ya subira ya ukaribu, urafiki, uhusiano na mazungumzo ya kidini ambayo waanzisha huko Punjab, Lahore na majimbo mengine. Alisema hayo katika Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari (Fides), Askofu Mkuu Sebastian Shaw, wa Jimbo Kuu la Lahore nchini Pakistan, ambaye alikwenda Jaranwala katika siku chache zilizopita na kundi la viongozi wa Kiislamu. “Nilifuatana na wajumbe watatu tofauti wa viongozi wa Kiislamu, alisema Askofu Mkuu kuwa walianzisha uhusiano mzuri nao na ambao wanashiriki njia ya mara kwa mara ya kukutana na mazungumzo. Walikuwa Sunni na Shia, kutoka shule tofauti za mawazo ya Kiislamu. Wote wametaka kuwa pale na walitaka kuona kwa macho yao wenyewe. Wengi wao waliguswa moyo, wote walionesha mshikamano na ukaribu wa kibinadamu kwa familia za Kikristo zilizotishwa na vurugu, wakasali nao wakapeana mikono na kuwafariji watu, waliowakaribisha kwa wema, kuthamini ishara hizi.
Askofu Mkuu alisema kuwa kwao huko Kwao huko Pakistani, ni ishara za umuhimu mkubwa kwa sababu zinachangia kubadilisha utamaduni na mawazo, pia kutokana na utangazaji wa vyombo vya habari ambavyo wamekuwa nao. Mmoja wa wajumbe watatu alikuwa Abdul Kabir Azad, imamu wa msikiti wa kifalme wa Lahore, mkubwa na muhimu zaidi nchini Pakistan ambaye Askofu Mkuu alisema “Ni mtu anayejulikana sana kwa huduma anayoifanya. Kusikia maneno yake ya kulaani vikali kile kilichotokea inatia moyo na matumaini. Kabir Azad na viongozi wengine wamesema kwa nguvu na uwazi kwamba ukatili dhidi ya watu wasio na hatia sio mafundisho ya Uislamu, ni wa kulaumiwa na haupaswi kuhalalishwa na dini. Katika ujumbe mwingine, Askofu Mkuu aliripoti, kuwa kulikuwa na Tahir Mehmood Ashrafi, kuhani muhimu wa Pakistan, mkuu wa Baraza la Ulamaa Wote wa Pakistan, chombo chenye ushawishi mkubwa sana katika ngazi ya kidini na kisiasa. Kwa hiyo hata Ahrafi aliguswa moyo, kiasi cha kutokwa machozi. Kwa niaba ya Waislamu wote nchini Pakistan, aliwaomba Wakristo msamaha. Alifanya hivyo faraghani, akiongea na watu aliokutana nao, na alifanya hivyo hadharani, kwenye mkutano huo mbele ya vyombo vyote vya habari, vilivyorekodi na kutangaza maneno yake, kwa manufaa ya umma wote. “Tulithamini sana maneno yake, tuliwakaribisha kwa urafiki”, alibainisha Askofu Mkuu Shaw.
Na aliendelea kusema kuwa “Nilipigwa na butwaa niliposikia viongozi wa Kiislamu wakiwaambia akina mama wa Kikristo waliokuwa wakilia: 'Watoto wenu ni watoto wetu. Msiwe na wasiwasi. Tutawatunza'. Mshikamano huo haukuwa wa maneno tu lakini thabiti: Viongozi wa Kiislamu watachukua jukumu la kugharamia elimu ya watoto kutoka katika familia zilizoathiriwa na unyanyasaji huko Jaranwala, kutoa ufadhili wa masomo yao hadi chuo kikuu. Inashangaza sana, hii inaonesha tabia ya dhati, ukaribu na nia njema ya wale ambao hawakubaliani na aina za vurugu baina ya jamii, na maimamu wa Kiislamu ambao walichochea kwa kuendeleza chuki na vurugu za kidini,” alisisitiza Askofu Mkuu Shaw. Uangalifu wa pekee pia ulioneshwa kwa makanisa yaliyoharibiwa kwani Viongozi wa Kiislamu wameita vurugu dhidi ya makanisa kwa majina, yaani, kufuru na wakibainisha kuwa Mtume Muhammad analaani vurugu zote dhidi ya alama za kidini. Watatusaidia kujenga upya, pamoja na taasisi za raia kama serikali ya Punjab inavyofanya mara moja kwa makanisa yaliyoharibiwa huko Jaranwala."Askofu Mkuu wa Lahore pia anathamini maneno na matendo ya wawakilishi wa vyama vya siasa vya Kiislamu, kama vile Seneta Siraj ul-Haq, mkuu wa Pakistan Jamaat-e-Islami. (JI), chama kikuu cha kidini nchini: Shirika la ustawi wa jamii linaloshirikiana na JI, Al-Khidmat Foundation, liliahidi kusaidia kujenga upya nyumba za Wakristo zilizoharibika.
Askofu Mkuu Shaw alisema “Katika saa za kwanza baada ya matukio na katika mkutano wa wa tarehe 25 Agosti 2023 Seneta Siraj-ul-Haq, akielezea uchungu wake wote, kuwa "kuchoma moto makanisa na nyumba kwa kujibu kesi ya madai ya kufuru ni dhidi ya mafundisho ya Uislamu." Akiendelea alisema kuwa chama chake cha JI kinaamini katika kanuni za kuheshimu ubinadamu, uvumilivu na kuishi pamoja kwa amani, na kutoa wito kwa wahusika wa ghasia kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.” Chama cha Kiislamu cha JI kimetangaza kuwa mwezi Septemba kitaitisha mkutano wa kitaifa, wakiwemo wa kidini walio wachache nchini Pakistan, ili kutekeleza mpango wa Msafara wa amani, wakisisitiza kwamba Pakistan ni ya raia wake wote, ambao wataishi pamoja na watalinda maisha na mali ya kila mmoja. Tunataka kuwasilisha ujumbe kwamba Pakistan ni nyumbani kwa dini zote na kwamba mustakabali wake mzuri unategemea amani. Yeyote anayeharibu amani ya nchi ni adui wa taifa, alisema Siraj-ul-Haq. Kiongozi huyo pia amehimiza, katika ngazi ya kisiasa, kuanzishwa kwa tume ya kitaifa inayojihusisha na masuala ya wachache, kwa lengo la kulinda haki.ya Wahindu, Wakristo, Wasikh na vikundi vingine vya kidini.
Askofu Mkuu wa Lahore alihitimisha kuwa “Mtazamo huu mpya wa ukaribu na mshikamano si wa bahati mbaya, bali ni matokeo ya kujitolea kwa muda mrefu na kwa subira katika uwanja wa mazungumzo ya kidini, ambayo tumekuwa tukifuatilia kwa angalau miaka 15. Sasa tuna kutia moyo. Tuliwaambia viongozi wa Kiislamu kwamba ni muhimu kuendelea na njia hii.Mara nyingi tunawaambia kwamba Wakristo nchini Pakistani, jumuiya ndogo, wanaheshimu Uislamu na alama zote za kidini na hawana sababu ya kuudhi Uislamu, Mtume au Korani. wamekiri kuwa madai ya kukufuru yanatungwa kwa sababu tofauti, kwa ugomvi wa kibinafsi.Wakristo na Waislamu nchini Pakistan hawana budi kubaki na umoja katika kukabiliana na changamoto hizi na masuala haya.Mazungumzo na umoja ni njia za kuleta maboresho madhubuti katika hali hii, ili kuzuia hali mbaya. matukio ya vurugu kutoka mara kwa mara, ili kutoa faida halisi za kuishi pamoja katika jamii yote.”